Mazishi Naibu Meya Morogoro yasitishwa, mwili warejeshwa mochwari

Mazishi Naibu Meya Morogoro yasitishwa, mwili warejeshwa mochwari

Hivi sampuli huko dar zinatumwa kwa njia ya mtandao au zinapakiwa kwenye gari na kusafirishwa?

Kama ni kwa gari, basi madereva wa serikali huu ndio mwaka wenu wa kupaua na kufanya finishing kubwa kubwa.
 
Rip kada!
SINTOFAHAMU ya mazishi ya aliyekuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro, marehemu Isihaka Sengo imesababisha mganga mkuu wa manispaa hiyo, Ikaji Rashid kuwatawanya waombolezaji nyumbani kwa marehemu mpaka mwili wa mrehemu utakapofanyiwa uchunguzi wa kitabibu.

Utata huo ulijitokeza punde baada ya Mganga Mkuu Manispaa ya Morogoro, Ikaji Rashid kufika nyumbani kwa marehemu majira ya mchana jana na kuwakuta ndugu na jamaa wakijindaa kwenda kuzika kisha kuwataka kusitisha zoezi hilo na mwili kupelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kwa uchunguzi.

Mganga huyo alisema, baada ya ofisi yake kupata taarifa kutoka hospitali aliyokuwa akitibiwa kwa mara ya mwisho kuna viashiria vya marehemu kuwa na maabukizi ya virusi vya Corona (COVID-19).

“Serikali inasitisha mazishi hadi itakapotangazwa vinginevyo na mwili unakwenda kuhifadhiwa chumba cha maiti, mwili huu katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na hapo tutachukua sampuli leo (jana) na kuzituma Dar es Salaam kwa uchunguzi,”alisema Mganga Rashid.

Source, TimesMajira

Soma >>>> Diwani wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Morogoro Afariki dunia,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuendelee kuchukua tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu wa Afya kuhusu kupambana na corona
Viongozi wa afya hawajatoa tahadhari saaizi wanatambaa na biti ya jiwe kutoka chato....
UTAALAMU TUPA KULEEE
 
Jana nimeona kwenye taarifa ya habari Aljazeera

Wanasansi wa Senegal,ndio Senegal nchi iliyoko Afrika ya Magharibi wameanza kutengeneza kifaa Cha kupia Covid19 kilicho fanana na kile wanachotumia wanawake kupima uja uzito,kwahiyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua na kujipima

Wanyaruanda nao Hawako nyuma,wametengeneza Ventilation yao mwenye badala ya kuagizia nje ambayo Bei yake ni €170000 kwa kila moja

Swali la kichokozi, wasomi na Wanasayansi wetu wako wapi,au ndio wanakimbilia kuwa wanasiasa na kuacha fani zao??
Kwani Ventilator PUMUA AID iliyobuniwa Tanzania hujaiona au unafanya maksudi kujifanya unajua sana ya RWANDA na Senegal, na ile Dawa ya NIMRI je hujaiskia hata??Au hata NIMRI Hujui ni nini? Anywaya USITUKANE MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO yaaani usijifanye kukashfu wataalam wa afya ilhali bado Corona Ippo utakuja kuomba pooo au uende ahela! Tema mate chini.
 
Tulifundishwa kukariri na kufaulu tu
 
Kwani Ventilator PUMUA AID iliyobuniwa Tanzania hujaiona au unafanya maksudi kujifanya unajua sana ya RWANDA na Senegal, na ile Dawa ya NIMRI je hujaiskia hata??Au hata NIMRI Hujui ni nini? Anywaya USITUKANE MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO yaaani usijifanye kukashfu wataalam wa afya ilhali bado Corona Ippo utakuja kuomba pooo au uende ahela! Tema mate chini.
Mkuu,siyajui hayo uliyoyasema, kusema ukweli nimeona ndoo ya kuoshea mikono yenye bomba ambalo linafunguliwa kwa kutumia miguu,.

Ni ubunifu mzuri kwani mtu hawazi kugusa Bomba kwa mikono,hii inasaidia kupunguza uambukizaji wa Covid19

Hiyo dawa ya NIMRI sijasikia,hivi hao NIMRI ndio akina Nani

Kama hiyo dawa unaijua wewe na watu wachache tu , Basi hiyo dawa haina lolote

Hizo PUMUA AID zimetengenezwa ngapi,zimesambazwa Hospitali ngapi, ziko wapi?

Mkuu,Ahela =Akhera ....boresha kiswahili chako kwa kusoma kamusi ya kiswahili
 
Jana nimeona kwenye taarifa ya habari Aljazeera

Wanayansi wa Senegal,ndio Senegal nchi iliyoko Afrika ya Magharibi wameanza kutengeneza kifaa Cha kupia Covid19 kilicho fanana na kile wanachotumia wanawake kupima uja uzito,kwahiyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua na kujipima

Wanyaruanda nao Hawako nyuma,wametengeneza Ventilation yao mwenye badala ya kuagizia nje ambayo Bei yake ni €170000 kwa kila moja

Swali la kichokozi, wasomi na Wanasayansi wetu wako wapi,au ndio wanakimbilia kuwa wanasiasa na kuacha fani zao??
Mkuu, nilishasema na Narudia kusema: Tanzania ina Wasomi Uchwara wa Kukariri tu ili kufaulu.

Hakuna Wasomi Wabunifu..HAKUNA

Sio madaktari, Sio Wahandisi, Sio Wakulima, Sio Wanasheria.

Ni watu wa Copying and Pasting

Hata wakipewa hivyo Vifaa wanavyosingiziaga na muda wa kufanya tafiti bado Hamna kitu.

Misingi ya nchi na jamii iliyowakuza imekaa kimaneno zaidi, kimajungu na kivivu.

Take it from me.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa ipo wazi amekufa kwa corona naalikua natibiwa SUA. swali la kujiuliza ni kwanini wakimbilie kutawanya watu kabla ya vipimo mambo mengine si ya kuficha.
 
Kwani Ventilator PUMUA AID iliyobuniwa Tanzania hujaiona au unafanya maksudi kujifanya unajua sana ya RWANDA na Senegal, na ile Dawa ya NIMRI je hujaiskia hata??Au hata NIMRI Hujui ni nini? Anywaya USITUKANE MAMBA KABLA YA KUVUKA MTO yaaani usijifanye kukashfu wataalam wa afya ilhali bado Corona Ippo utakuja kuomba pooo au uende ahela! Tema mate chini.
Kama hayo yapo na watu hawajui kama yapo basi kuna mtu mahali hafanyi wajibu wake....., Ingawa kila mtu anayejitahidi kufanya lolote inabidi apewe moyo na kupongezwa atleast he/she is trying..,
 
Back
Top Bottom