Mazishi ya hayati Mzee Edwin Mtei, Muasisi wa Chadema, Januari 24, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure, Mzee Mtei alituasa haki inatangulia ndipo amani inafuata

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure amesema kuwa enzi za uhai wake, Hayati Edwin Mtei aliwausia kuwa “haki inatangulia, amani inafuata,” na hivyo kuendelea kuwa dira ya chama hicho katika kudai demokrasia na utawala bora.

“Tunaiomba Serikali itende haki kwa Watanzania. Tumekuwa tukimtembelea mara nyingi Mzee Mtei, na mara zote alikuwa akituambia haki ndiyo msingi wa amani,” amesema Mungure.

Ashura Masoud: Mtei hakukumbatia madaraka halihitaji mabadiliko

Katika Ibada ya mazishi ya Muasisi wa CHADEMA, Hayati Mzee Edwin Mtei, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Masoud, amesema wamefika kutoa heshima zao kwa kutambua uzito wa mchango aliouacha ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

Amesema Mzee Mtei hakuwa mtu wa kukumbatia madaraka, bali kiongozi aliyeamini katika misingi ya demokrasia na alikubali kuyaachia madaraka kwa hiari kwa ajili ya ustawi wa taifa.

Ashura ameweka wazi kuwa utawala wa nchi haulazimiki kuwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee, bali ni wa Watanzania wote wanaotamani mabadiliko yenye tija, akisisitiza kuwa bado wananchi wanahitaji huduma bora za afya, hasa kina mama wajawazito.

Amesema haiwezekani kuendelea kusisitiza amani pekee ilhali wananchi wanafariki kutokana na ukosefu wa huduma stahiki za afya, akiongeza kuwa hayo ndiyo mambo ambayo viongozi wanapaswa kuyatolea majibu.

Sugu: Rekodi ya mzee Mtei haiwezi kufutika Mbeya, ameondoka hatujachukua nchi

Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi, ametoa pole kwa familia ya marehemu mzee Edwin Mtei, ambaye alikuwa muasisi wa chama hicho, akieleza kuwa pamoja na huzuni waliyonayo kufuatia kifo chake, bado wanayo sababu ya kusherehekea mchango mkubwa aliouacha kwa taifa na kwa CHADEMA.

Mbilinyi amesema mzee Mtei ameacha alama isiyofutika, hususan kwa mkoa wa Mbeya na kanda ya Nyasa kwa ujumla, akibainisha kuwa mbegu aliyoipanda miaka mingi iliyopita imeendelea kuota na kuzaa matunda, hali iliyoifanya Mbeya kuwa ngome imara ya CHADEMA hadi leo.

Aidha, amemshukuru marehemu Mtei kwa misimamo yake thabiti ya kisiasa tangu enzi za uongozi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, akisema misimamo hiyo imeendelea kuwa dira kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA.

Mbilinyi ameyasema hayo leo Januari 24, 2026, wakati wa salaam za chama cha CHADEMA kanda ya Nyasa katika ibada ya mazishi ya marehemu mzee Edwin Mtei wakati wa hatua ya Chama hicho kutoa kumbukizi.

"Mzee Mtei ameondoka hatujachukua nchi, lakini ameondoka akiacha chama alichokianzisha kuwa chama kikuu cha siasa hapa nchini." - Joseph Mbilinyi (Sugu), Mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Nyasa

John Mnyika ataka wananchadema kutimiza ndoto ya Mzee Mtei yakuhakikisha CHADEMA inashika Dola

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema alimfahamu Hayati Mzee Edwin Mtei kama kiongozi aliyesimamia misimamo yake na aliyelipenda chama kwa dhati, akilizingatia na kulikumbuka wakati wote wa uhai wake.

Akizungumza katika Ibada ya Mazishi Tengeru, Jijini Arusha, wakati CHADEMA ikitoa kumbukizi zake, Mnyika amesema moja ya mambo aliyoyashuhudia ni msimamo thabiti wa Mzee Mtei kuhusu alama ya chama, akieleza kuwa marehemu hakuwahi kukubali pendekezo lolote la kubadilisha alama ya vidole viwili kwenye nembo ya CHADEMA.

Amesisitiza pia kuwa sasa ni wakati wa taifa kwenda kwenye Katiba Mpya, jambo alilosema ni sehemu ya maono na mapambano ambayo Mzee Mtei aliyapigania tangu enzi za uhai wake.

Aidha, Mnyika amewataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuendelea kushikamana ili chama hicho kushika dola na kuongoza serikali, kama sehemu ya kutimiza ndoto na urithi wa kisiasa ulioachwa na Hayati Mtei.

Msemaji wa Familia ya Mzee Mtei, Freeman Mbowe, amewaomba waandishi wa habari kuepuka kupiga picha za mwili wa marehemu

Mbowe amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kupiga picha za matukio yanayoendelea badala ya kupiga picha za mwili wa marehemu, hatua ambayo inalenga kulinda faragha ya familia na heshima ya mzee wetu.

Ameeleza kuwa kwa sasa ni muda wa waombolezaji kupita mbele ya jeneza ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Mtei. Ratiba ya kutoa heshima za mwisho inatarajiwa kumalizika saa 6:50 mchana wa leo.

Msemaji wa familia pia amesisitiza waombolezaji kuzingatia muda uliopangwa, kwani idadi ya watu ni kubwa kuliko muda uliopo.

Aidha Mbowe amesema kuwa Mzee Mtei alikuwa na kiwango cha ajabu cha uadilifu

Dorothy Semu: Tunajivunia mzee Mtei katika kupigania Haki

Kiongozi wa Chama cha Act Wazalendo, Dorothy Semu, amesema kwamba wao kama sehemu ya wapigania demokrasia ya kweli na mabadiliko wana mengi ya kujifunza kutoka kwa Hayati Mzee Edwin Mtei.

Ameyasema hayo leo Januari 23, 2026, wakati akitoa salamu za rambirambi katika Ibada ya Mazishi ya Mzee Mtei, Tengeru Jijini Arusha.

"Hili ni darasa kubwa kwetu sisi viongozi, ikiwemo wa vyama vya siasa. Leo hii tunajivunia kusimama katika maeneo mbalimbali tukiendelea kudai haki, demokrasia na maendeleo ya watu."

CHAUMMA: Tutamuenzi Mzee Mtei kwa kupigania Haki

Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema Taifa litamuenzi Hayati Edwin Mtei kwa uhuru wa mawazo, jambo ambalo kama asingesimama imara kuamini katika uhuru huo, ingekuwa vigumu kwa wanasiasa kusimama na kutamba.

"Tutaendelea kupigania uhuru wa mawazo katika kufikia Taifa lenye umoja, ambapo demokrasia itatamalaki, na haki pamoja na uhuru wa mawazo vitaheshimiwa."

Ujumbe wa Lissu wenye kura 9 kusomwa msibani kwa mzee Mtei

"Tumepokea salamu za kurasa tisa kutoka kwa Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu, ambazo tutaziweka hadharani kwa wanachama na vyombo vya habari ili umma usikie namna ambavyo Mheshimiwa Tundu Lissu amemuomboleza Mzee wetu, Edwin Mtei"-Naibu katibu mkuu Chadema

Jenerali Ulimwengu, Mtei alibishana na Mwalimu kutaa 'Uswahili katika Uongozi'

Mwanahabari mkongwe nchini, Jenerali Ulimwengu, amesema marehemu Mzee Edwin Mtei, muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alikuwa kiongozi aliyekataa vikali vitendo alivyoviita “Uswahili” katika uongozi, hususan tabia ya viongozi kukiuka ahadi walizozitoa kwa wananchi.

Waziri mkuu Mwigulu Lameck Nchemba amefika katika katika msiba wa Mtei

Waziri mkuu amwesali katika msiba huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, tayari ameshaawasili na amesahi kitabu cha wageni.
 
Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure, Mzee Mtei alituasa haki inatangulia ndipo amani inafuata

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Elisa Mungure amesema kuwa enzi za uhai wake, Hayati Edwin Mtei aliwausia kuwa “haki inatangulia, amani inafuata,” na hivyo kuendelea kuwa dira ya chama hicho katika kudai demokrasia na utawala bora.

“Tunaiomba Serikali itende haki kwa Watanzania. Tumekuwa tukimtembelea mara nyingi Mzee Mtei, na mara zote alikuwa akituambia haki ndiyo msingi wa amani,” amesema Mungure.

Ashura Masoud: Mtei hakukumbatia madaraka halihitaji mabadiliko

Katika Ibada ya mazishi ya Muasisi wa CHADEMA, Hayati Mzee Edwin Mtei, Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kati, Ashura Masoud, amesema wamefika kutoa heshima zao kwa kutambua uzito wa mchango aliouacha ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

Amesema Mzee Mtei hakuwa mtu wa kukumbatia madaraka, bali kiongozi aliyeamini katika misingi ya demokrasia na alikubali kuyaachia madaraka kwa hiari kwa ajili ya ustawi wa taifa.

Ashura ameweka wazi kuwa utawala wa nchi haulazimiki kuwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee, bali ni wa Watanzania wote wanaotamani mabadiliko yenye tija, akisisitiza kuwa bado wananchi wanahitaji huduma bora za afya, hasa kina mama wajawazito.

Amesema haiwezekani kuendelea kusisitiza amani pekee ilhali wananchi wanafariki kutokana na ukosefu wa huduma stahiki za afya, akiongeza kuwa hayo ndiyo mambo ambayo viongozi wanapaswa kuyatolea majibu.

Sugu: Rekodi ya mzee Mtei haiwezi kufutika Mbeya

Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi, ametoa pole kwa familia ya marehemu mzee Edwin Mtei, ambaye alikuwa muasisi wa chama hicho, akieleza kuwa pamoja na huzuni waliyonayo kufuatia kifo chake, bado wanayo sababu ya kusherehekea mchango mkubwa aliouacha kwa taifa na kwa CHADEMA.

Mbilinyi amesema mzee Mtei ameacha alama isiyofutika, hususan kwa mkoa wa Mbeya na kanda ya Nyasa kwa ujumla, akibainisha kuwa mbegu aliyoipanda miaka mingi iliyopita imeendelea kuota na kuzaa matunda, hali iliyoifanya Mbeya kuwa ngome imara ya CHADEMA hadi leo.

Aidha, amemshukuru marehemu Mtei kwa misimamo yake thabiti ya kisiasa tangu enzi za uongozi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, akisema misimamo hiyo imeendelea kuwa dira kwa wanachama na viongozi wa CHADEMA.

Mbilinyi ameyasema hayo leo Januari 24, 2026, wakati wa salaam za chama cha CHADEMA kanda ya Nyasa katika ibada ya mazishi ya marehemu mzee Edwin Mtei wakati wa hatua ya Chama hicho kutoa kumbukizi.

John Mnyika ataka wananchadema kutimiza ndoto ya Mzee Mtei yakuhakikisha CHADEMA inashika Dola

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema alimfahamu Hayati Mzee Edwin Mtei kama kiongozi aliyesimamia misimamo yake na aliyelipenda chama kwa dhati, akilizingatia na kulikumbuka wakati wote wa uhai wake.

Akizungumza katika Ibada ya Mazishi Tengeru, Jijini Arusha, wakati CHADEMA ikitoa kumbukizi zake, Mnyika amesema moja ya mambo aliyoyashuhudia ni msimamo thabiti wa Mzee Mtei kuhusu alama ya chama, akieleza kuwa marehemu hakuwahi kukubali pendekezo lolote la kubadilisha alama ya vidole viwili kwenye nembo ya CHADEMA.

Amesisitiza pia kuwa sasa ni wakati wa taifa kwenda kwenye Katiba Mpya, jambo alilosema ni sehemu ya maono na mapambano ambayo Mzee Mtei aliyapigania tangu enzi za uhai wake.

Aidha, Mnyika amewataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kuendelea kushikamana ili chama hicho kushika dola na kuongoza serikali, kama sehemu ya kutimiza ndoto na urithi wa kisiasa ulioachwa na Hayati Mtei.

Msemaji wa Familia ya Mzee Mtei, Freeman Mbowe, amewaomba waandishi wa habari kuepuka kupiga picha za mwili wa marehemu

Mbowe amesisitiza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kupiga picha za matukio yanayoendelea badala ya kupiga picha za mwili wa marehemu, hatua ambayo inalenga kulinda faragha ya familia na heshima ya mzee wetu.

Ameeleza kuwa kwa sasa ni muda wa waombolezaji kupita mbele ya jeneza ili kutoa heshima zao za mwisho kwa Mzee Mtei. Ratiba ya kutoa heshima za mwisho inatarajiwa kumalizika saa 6:50 mchana wa leo.

Msemaji wa familia pia amesisitiza waombolezaji kuzingatia muda uliopangwa, kwani idadi ya watu ni kubwa kuliko muda uliopo.

Thanks for this
Rip Edwin Mtei
P
 
HUyu mchungaji/askodu anatema madini.

Kama Taifa tutoke katika matope tutafute njia ya kwenda mbele.

Tuzungumze haki na kweli.
 
Mchunga/asko.
Kunywa maji ya kutosha maana ni dawa

Fanya mazoezi

Lala usingizi wa kutosha

Achaneni na stress.
 
24 January 2026
Tengeru, Arusha
Tanzania

HECHE AWASHA MOTO VIKALI MBELE YA WAZIRI MKUU" WATU WANAPOTEA UKIWA NA HOJA TOFAUTI UNAPOTEZWA"​

Awasilisha salamu za mwenyekiti wa chama cha CHADEMA aliye gerezani Tundu Lissu kwa umma katika msiba wa mwazilishi wa CHADEMA mzee Edwin Mtei ...

View: https://m.youtube.com/watch?v=OhafNlDlL8w
 
24 January 2026

MBOWE AMCHANA WAZI WAZI WAZIRI MKUU MWIGULU "WALIO MAGEREZA WAACHIWE, SERIKALI MKIRI MAKOSA / CHADEMA WAMEONEWA"​

View: https://m.youtube.com/watch?v=RIxYqRqd5p8
Uhuru wa watu ni kitu muhimu kuliko maendeleo ya watu

Freeman Mbowe asisitiza viongozi wetu wa CHADEMA watakuwa tayari kufanya nazungumzo pale tu serikali ya chama dola kongwe itapokuwa inatekeleza kwa vitendo hatua za haki

Mwenyekiti mstaafu Freeman Mbowe asisitiza CHADEMA siyo wakorofi ila pale inapoonewa hatuwezi kupoa, hakiwezi kukaa kimya .. na ujumbe huu Mwigulu Nchemba umpelekee mkubwa wako.... serikali CCM ndiyo tatizo la mkwamo wa kupatikana haki, kesi za kutunga zifutwe, ...
 
Back
Top Bottom