Mazishi ya Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu kuleta utata baada ya serikali kusitisha maombolezo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ametangaza kusitisha ghafla kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu, kufuatia mvutano unaoendelea kati ya serikali na familia ya marehemu kuhusu mipango ya mazishi yake

Akihutubia taifa Alhamisi usiku, Rais Hichilema alisema kipindi cha maombolezo kimefikia mwisho na taifa linapaswa kurejea kwenye maisha ya kawaida. “Serikali imefanya kila jitihada kuzungumza na familia ya Rais wetu wa sita,” alisema Hichilema

Awali, kipindi cha maombolezo kilipangwa kuanza Juni 8 hadi 14 lakini baadaye kikaongezwa hadi Juni 23, huku bendera zikipandishwa nusu mlingoti na vituo vya redio vikicheza nyimbo za huzuni. Uamuzi wa kuongeza muda huo ulifikiwa baada ya mkutano kati ya viongozi wa serikali na familia ya Lungu kwa lengo la kutatua mvutano juu ya ratiba ya mazishi

Mipango yote ya mazishi ilikuwa imekamilika, na mwili wa marehemu ulikuwa umepangwa kurejeshwa nchini Jumatano kwa ndege ya kukodi, ambapo ungepokelewa kwa heshima zote za kijeshi kabla ya kuagwa rasmi nyumbani kwake siku ya Jumapili na kuzikwa siku iliyofuata

Hata hivyo, familia ya Lungu ilisitisha urejeshaji huo ikisema serikali haikuheshimu makubaliano yao kuhusu ratiba ya mazishi. Familia hiyo ilisema bado inatarajia mwili wa kiongozi huyo utarejeshwa “siku moja” na kuzikwa Zambia

Serikali ilieleza masikitiko yake kuhusu uamuzi huo wa familia na ikaomba radhi kwa serikali na jeshi la Afrika Kusini ambao walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kukabidhi mwili huo. “Ni jambo la kusikitisha kwamba juhudi zao zimekuwa bure,” alisema Hichilema

Chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF), ambacho Lungu alikiongoza hadi kufariki, kimesimama na familia, kikishutumu serikali kwa kugeuza msiba huo kuwa wa siasa

Serikali imetoa wito kwa wananchi kuwa watulivu na imesisitiza utayari wake wa kuendelea na mazungumzo na familia kuhusu suala hilo

Soma pia: Familia na Serikali zakubaliana Lungu kuzikwa Juni 22 Lusaka, Zambia
====
Zambia's President Hakainde Hichilema has abruptly ended the national mourning period of former President Edgar Lungu in an escalating stand-off between the family and the authorities about his burial plans.
It follows the last-minute cancellation of the return of Lungu's body from South Africa by his family on Wednesday, leaving the country uncertain about when and where the former leader will be buried.
In his address on Thursday evening, President Hakainde Hichilema announced an immediate end to the mourning period, saying the country needed to "resume normal life".

"The government has done everything possible to engage with the family of our departed sixth president," said Hichilema.

The national mourning period initially ran from 8 to 14 June but was later extended until 23 June, with flags flying at half-mast and radio stations playing solemn music.
The extension followed a meeting between government officials and Lungu's family in an attempt to resolve the deadlock over his funeral programme.

Burial arrangements had been finalised and his remains were due to be flown back home on Wednesday on a private charter plane.

123.png

​
Source: BBC
 
Kuna shida hapo, HH na Lungu walikuwa hawapikiki jungu moja !!

Mimi nadhani suluhu ingekuwepo tu mwili uzikwe maisha yaendelee !
 
Wangemsikiliza Samia. Kifo ni kifo tu. Maombolezo mpaka mzozo ya nini?
 
Waafrika ndiyo kazi tunayoiweza (kugombana misibani) aibu kubwa
Hapana sio kugombana msibani Bali unafiki kwenye misiba.

Binafsi naona familia Iko sahihi imagine serikali ilimcheleweshea kumpa ruhusa kwenda South kutibiwa alafu Leo ndio wanajifanya mstari wa mbele kuhudumia mazishi au Leo hii Tundu Lissu afie gerezani alafu eti Samia atangaze kugharamia shughuli za msiba nonsense!!
 
Malipo ni hapahapa duniani mkuu. Huyo Lungu alimtesa sana mpinzani wake HH.
 
Uongozi ni dhamana,wakati wowote inaisha, tusijifanye miungu watu ipo siku vyeo hatutakuwa navyo na tukumbuke duniani tunapita.

Wathamini wote wanaokuzunguka.
Nimeandika haya kwa uchungu mno
 
Hapana sio kugombana msibani Bali unafiki kwenye misiba.

Binafsi naona familia Iko sahihi imagine serikali ilimcheleweshea kumpa ruhusa kwenda South kutibiwa alafu Leo ndio wanajifanya mstari wa mbele kuhudumia mazishi au Leo hii Tundu Lissu afie gerezani alafu eti Samia atangaze kugharamia shughuli za msiba nonsense!!
Ndio keshakufa hakuna namna itasaidia kumrejeshea uhai wake.
 
Hawa nao wafukie tu, hata kama matakwa yao yatafanyiwa kazi, bado yataibuka tu na mengineyo.

Hapo kuna political affairs, haiwezekani ishu ichukue mda hivi
 
Serikali nayo sii iwaachie familia wazike watakavyo
Naona ndo serikali ilichoamua kufanya.

Ila shida ni kwamba familia hiyo ina mdomo sana. Serikali itawaacha waratibu mazishi kama watakavyo ila baada ya mazishi utawasikia tena wanalalamika "serikali ilitususia msiba.".
 
Back
Top Bottom