Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ametangaza kusitisha ghafla kipindi cha maombolezo ya kitaifa kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Edgar Lungu, kufuatia mvutano unaoendelea kati ya serikali na familia ya marehemu kuhusu mipango ya mazishi yake
Akihutubia taifa Alhamisi usiku, Rais Hichilema alisema kipindi cha maombolezo kimefikia mwisho na taifa linapaswa kurejea kwenye maisha ya kawaida. “Serikali imefanya kila jitihada kuzungumza na familia ya Rais wetu wa sita,” alisema Hichilema
Awali, kipindi cha maombolezo kilipangwa kuanza Juni 8 hadi 14 lakini baadaye kikaongezwa hadi Juni 23, huku bendera zikipandishwa nusu mlingoti na vituo vya redio vikicheza nyimbo za huzuni. Uamuzi wa kuongeza muda huo ulifikiwa baada ya mkutano kati ya viongozi wa serikali na familia ya Lungu kwa lengo la kutatua mvutano juu ya ratiba ya mazishi
Mipango yote ya mazishi ilikuwa imekamilika, na mwili wa marehemu ulikuwa umepangwa kurejeshwa nchini Jumatano kwa ndege ya kukodi, ambapo ungepokelewa kwa heshima zote za kijeshi kabla ya kuagwa rasmi nyumbani kwake siku ya Jumapili na kuzikwa siku iliyofuata
Hata hivyo, familia ya Lungu ilisitisha urejeshaji huo ikisema serikali haikuheshimu makubaliano yao kuhusu ratiba ya mazishi. Familia hiyo ilisema bado inatarajia mwili wa kiongozi huyo utarejeshwa “siku moja” na kuzikwa Zambia
Serikali ilieleza masikitiko yake kuhusu uamuzi huo wa familia na ikaomba radhi kwa serikali na jeshi la Afrika Kusini ambao walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kukabidhi mwili huo. “Ni jambo la kusikitisha kwamba juhudi zao zimekuwa bure,” alisema Hichilema
Chama cha upinzani cha Patriotic Front (PF), ambacho Lungu alikiongoza hadi kufariki, kimesimama na familia, kikishutumu serikali kwa kugeuza msiba huo kuwa wa siasa
Serikali imetoa wito kwa wananchi kuwa watulivu na imesisitiza utayari wake wa kuendelea na mazungumzo na familia kuhusu suala hilo
Soma pia:
Familia na Serikali zakubaliana Lungu kuzikwa Juni 22 Lusaka, Zambia
====
Zambia's President Hakainde Hichilema has abruptly ended the national mourning period of former President Edgar Lungu in an escalating stand-off between the family and the authorities about his burial plans.
It follows the last-minute cancellation of the return of Lungu's body from South Africa by his family on Wednesday, leaving the country uncertain about when and where the former leader will be buried.
In his address on Thursday evening, President Hakainde Hichilema announced an immediate end to the mourning period, saying the country needed to "resume normal life".
"The government has done everything possible to engage with the family of our departed sixth president," said Hichilema.
The national mourning period initially ran from 8 to 14 June but was later extended until 23 June, with flags flying at half-mast and radio stations playing solemn music.
The extension followed a meeting between government officials and Lungu's family in an attempt to resolve the deadlock over his funeral programme.
Burial arrangements had been finalised and his remains were due to be flown back home on Wednesday on a private charter plane.
Source: BBC