Maziwa haya(Lakes) yanaweza kuua watu wengi sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hii inatokea kwenye maziwa yaliyopo kwenye maeneo yenye volkano, hasa crater lakes. Maeneo ya volkano huwa na gesi nyingi sana ikitoka chini, hasa hasa carbondioxide.

Gesi hiyo inaweza zama kwenye maji kama ambavyo gesi huzama kwenye soda.

Sasa maziwa kama ziwa Ngozi Mbeya, ziwa Nyos huko Cameroon na ziwa Kivu mpakani mwa Rwanda na Congo yana gesi nyingi sana ndani yake.

Sasa. Kama ilivyo kwenye soda, ukitingisha soda au ukitumbukiza kitu gesi inalipuka. Hata kwenye maziwa yenye gesi.

Ziwa likitingishika labda kwa tetemeko la ardhi au kitu kikiingia labda kwa maporomoko ya ardhi gesi hulipuka kutoka humo ziwani.

Na sababu gesi ya carbon dioxide ni nzito kuliko hewa ya kawaida. Inachofanya inapotoka inatuama chini kama blanketi na hii hewa nyepesi tunayovuta inapaa juu. Hapo watu na wanyama na wadudu wote wanakufa kwa kukosa hewa.

Kuna mwaka Ziwa Nyos huko Cameroon maporomoko ya udongo yaliingia ziwani. Humo yalisababisha hewa ilipuke ambapo watu karibu 1800 na mifugo elfu kadhaa walikufa.

Ziwa kivu ndiyo hatari zaidi. Ikitokea gesi ya mule imelipuka, malaki ya watu wanaweza kufa.

Pengine mababu walijua habari ya maziwa haya, pengine ndiyo maana jina Nyos na Ngozi/Ngosi yanafanana.

Ziwa Nyos na Ziwa Ngos

View attachment 2440473View attachment 2440475
 
Badala ya kusema malaki sema mamia ya maelfu
 
Mmeshaanza kututia hofu sasa,,,kwa hiyo unawapa ushauri gani wale wanaoishi mazingira hayo??
 
Lkn hayo maziwa Yana potential Sana yakitumika kikamilifu,kwa yule jamaa tolu mwembamba wa hapo lilipo ziwa Kivu wao wanazalisha umeme wa MW 56 kwa ku-extract hio gas ziwani,na mwaka huu wamesaini contract ya kuchimba gas zaidi kwa ajili ya kutumia kujaza mitungi ya gas ya kupikia ili waache kabisa kuagiza kutoka nje ya nchi gas ya kupikia.
 
Back
Top Bottom