Nimekuwa nikisikia kutoka kwa watu mbalimbali kuwa pindi hutumiapo dawa zozote basi itakupaswa usitumie maziwa aina yoyote kwasababu matumizi ya maziwa hupunguza au kuondoa kabisa ufanisi wa dawa hizo hivyo kupelekea kutotibu ugonjwa uliokusudiwa.
Kwa uelewa wangu ni dawa mbili tu ambazo hushauriwi kutumia maziwa pindi ukiwa unazitumia ambazo ni
Nawasilisha.
Kwa uelewa wangu ni dawa mbili tu ambazo hushauriwi kutumia maziwa pindi ukiwa unazitumia ambazo ni
- Tetracycline
- Antacids
Nawasilisha.
- Tunachokijua
- Maziwa ni kimiminika kinachozalishwa na tezi za wanyama wanaopatikana kundi la mamalia, ikiwa ni pamoja na wanadamu.
Ingawa maziwa ya maziwa yanaweza kutoka kwa wanyama wote wa kundi la mamalia, ng'ombe, mbuzi, nyati na kondoo ni wazalishaji wa kawaida.
Maziwa yote huundwa na karibu 87% ya maji. 13% iliyobaki ina protini, mafuta, wanga, vitamini na madini.
Dawa za Tetracycline na Antacids
Maana ya kifamakolojia inaitaja dawa kama kemikali, au zao la kemikali (isipokuwa chakula) ambayo hutumiwa kuzuia, kutambua, kutibu, au kupunguza dalili za ugonjwa au hali isiyo ya kawaida. Pia, zinaweza kuathiri jinsi ubongo na mwili wote unavyofanya kazi na kusababisha mabadiliko katika hisia, ufahamu, mawazo au tabia.
Tetracycline, dawa iliyogunduliwa miaka ya 1940 ni antibayotiki (Viuavijasumu) inayotibu aina mbalimbali za maradhi ya binadamu yanayosababishwa na Bakteria.
Aidha, Antacids ni kundi kubwa la dawa za kupambana na asidi mwilini, hutumika kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo kiungulia na vidonda vya tumbo.
Matumizi ya maziwa wakati wa kumeza dawa
Maji ni kimiminika cha kidunia na chaguo namba moja katika kumeza dawa. Uwezo wake wa kuyeyusha dawa unathibishwa na tafiti kuwa mkubwa zaidi kuliko vimiminika vingine vyote.
Maziwa huwa na viambato vinavyoweza kuathiri ufanisi wa baadhi ya makundi ya dawa hasa antibayotiki, Tetracycline ikiwemo. Baadhi ya viambato hivyo ni madini ya calcium, magnesium na protini ya casein.
Mathalani, madini ya calcium yanayopatikana kwenye maziwa huungana na dawa ya Tetracyline kutengeneza muunganiko usio wa kawaida ambao huathiri ufyonzwaji wa dawa kwenye damu kwa 50%-90%.
Baadhi ya dawa ambazo ufanisi wake hupungua zikimezwa na maziwa, au mhusika akitumia maziwa muda mfupi baaada ya kuzimeza ni ciprofloxacin, norfloxacin, alendronate, etidronate, na risedronate.
Kwa dawa za antacids kama Aluminum hydroxide Al(OH)3, Magnesium carbonate, Gaviscon (alginic acid) and Pepto-Bismol (bismuth subsalicylate) huwa na baadhi ya viambato vinavyofanana na vile vinavyopatikana kwenye maziwa.
Hali hii inaweza kuathiri ufanisi wa dawa husika pamoja na kuleta madhara kwenye afya ya mhusika.
Maziwa huathiri ufanisi wa dawa zote?
Hapana, maziwa hayaathiri aina zote za dawa isipokuwa chache ambazo mfano wake umefafanuliwa kwenye aya za juu. Pia, baadhi ya dawa (dawa nyigi) zinaweza hata kumezwa pamoja na maziwa pasipo kuleta athari yotote.
Wataalam hushauri kutumia maji badala ya maziwa kwa kuwa maji hayana viambato vinavyoweza kuingiliana na dawa wakati wowote ule, na mtu yeyote anaweza kutumia pasipo kujali hali ya ugonjwa wake tofauti na maziwa ambayo huangalia pia historia ya uwepo wa magonjwa mengine mfano magonjwa ya moyo na shinikizo kubwa la damu.
Hivyo, maziwa yanaweza yasiathiri ufanisi wa dawa lakini yakaamsha changamoto mbalimbali za kiafya zinazoweza kuwa na madhara makubwa kwa mhusika.
Ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya kabla ya kumeza dawa na maziwa ili kujiweka salama wakati wote.