Mazoezi ni siri kubwa ya urembo na tambo zuri

Mazoezi ni siri kubwa ya urembo na tambo zuri

Aahahahahahahaaa looh

Umenipa kiu ya kula prawns, halafu wako mbali na upeo wa miguu yangu...!

Hivi ilikiwaje nikakusimulia fungu la elf 5...!?? 🤔🤔🤔😅
Mkiwa na raha na furaha mnajikuta TU mnafunguka. Irudiweeee irudiweee
 
Ni kweli kabisa... Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Mbona sioni watu wakilisema zoezi la kuruka kamba? Nadhani ni zuri kwa sbb linainvolve kila kiungo
 
Naungana na wewe kwa 100%
Binafsi mazoezi yameniweka vzr sana hakuna ninachojutia kwenye mazoezi. Faida ni nyingi mno.
Oct nafikisha 40yrs lkn hapo ofcn nashangaa madogo wa field wanakomaa kuwajaza shimakoo washkaji ambao kwangu ni wadogo kwa miaka 5 na zaidi.

Siku moja nikawauliza hv mbona mm hamniamkiii mnaishia na salamu ya Mambo au za asbh. Mmoja akajibu kuwa wewe tupo sawa tu mbona. Nachekaga sana.

Lkn kuna sehemu nilisoma kuwa mazoezi katika ubora wake yanakurudisha young to 8 years na zaidi. Pia mchango wa tunavyokula ni 80% ya afya za miili yetu wakati 20% ni kwa ajili ya mazoezi. So tule kwa afya + tufanye mazoezi.

Ngoja nilale kesho naendelea naendelea na Running challenge yangu ya July ya 200km ambapo sasa bdo nipo Km ya 112. Nadaiwa hizo 88km

Tufanye mazoezi jamani.

Check hiyo kwa ajili ya record keeping ya workout zako

Uzuri hata uonekane kijana... umri unabakia uleule na mwisho wa siku sote tunarudi mavumbini...

Yaani niache kupiga mvinyo nihangaike na mazoezi?

Raha jipe mwenyewe bhana.... maisha ni hayahaya
 
Naomba hiyo kilauri nikuwekee K Vant ya mwisho nikupeleke ukalale.

Leo zamu ya bibi kubwa.
1626726444598.png
 
Mazoezi ya lisaa limoja kwa siku yanatosha kukufanya upate mwili unaopendeza. Mwili unaokubali kila nguo. Mazoezi yanasaidia kukuepusha na magonjwa mengi ya muda mrefu, mfano kisukari, magonjwa ya moyo, stroke, na matatizo ya miguu.

Inapendeza ukiwa na miaka 70+au 80+ bado unaweza kwenda sokoni kununua matunda fresh, kuyaandaa na kula kila siku bila kuwategemea wajukuu. Haya yanawezekana ukianza kufanya mazoezi mapema.

Katika nyumba yako, ukiwa na uwezo unaweza kuweka chumba cha gym. Kusiwe store bali ni chumba cha mazoezi chenye trade mill, exercise by cycle, punching bag, exercise mat kwaajili ya yoga. Kama hali yako ni kama yangu tu weka trade mill chumbani. Hii itakusaidia kutokukosa mazoezi hata mvua ikiwa inanyesha nje.
huwa unaandika sana point
 
Uzuri hata uonekane kijana... umri unabakia uleule na mwisho wa siku sote tunarudi mavumbini...

Yaani niache kupiga mvinyo nihangaike na mazoezi?

Raha jipe mwenyewe bhana.... maisha ni hayahaya
Mkuu suala siyo kuonekana kijana, suala lipo kwenye ubora wa afya kwa ujumla wake. Leo hii ukiumwa ukalala zaidi ya mwezi hilo tayari ni tatizo kwa uchumi wako na waregemezi pia. Tunachozungumzia hapa ni kujitahidi kuondokana na risk ya kutopata magonjwa yasiyo ambukiza ambayo kama tungefanya mazoezi tungeepukana nayo.

Kuonekana kijana ni moja ya faida chache sana kwenye mazoezi.

Ninao marafiki ambao walikuwa wabishi kama wewe lkn baada ya mmoja wao kupigwa stroke na kubaini kuwa imetokana na hypertension ambavyo aghalabu imetokana na style ya maisha yake hasa kula unhealth na kutofanya mazoezi, wengi wa wale marafiki sasa wameunga juhudi na tunaendelea nao kwenye mazoezi yetu.

Nakukumbusha:-
80% ya afya yako ni vile unavyokula+Kunywa
20% ni mazoezi.
#Eatwellhealthy #Trainsmart
 
Back
Top Bottom