Mazoezi ya Ndani: Zoezi la kuruka kamba

Mazoezi ya Ndani: Zoezi la kuruka kamba

castongo

Member
Joined
Mar 16, 2008
Posts
57
Reaction score
74
Tangu nilipogundua umuhimu wa mazoezi kwenye mwendo wa kawaida wa maisha, nimejaribu hili na lile, kuona linalonifaa zaidi. Katika jaribujaribu mara kwa mara nimeongeza vikolezo mbalimbali kwenye mazoezi yangu na kuyaboresha kidogo. Nimeongeza vikolezo hivyo kwa malengo ambayo binafsi nayaona ni ya muhimu kwenye zoezi langu.

Kwa mtazamo wangu lazima nijue kiasi cha mazoezi niliyofanya. Hivyo natafuta namna ya kupima mazoezi yangu. Basi hapo nimejaribu kutumia fitness bands, na apps kama vile Endomondo pia Google fit kwa kutembea na kukimbia nk. Napenda pia kujiburudisha ndani ya zoezi. Napenda kutumia muziki ambao sio tu unaniburudisha wakati wa zoezi, lakini pia mwendo wa muziki unanipa msukumo wa pekee na wakati mwingine rhythm ya kwenda na zoezi langu. Napenda kuwa na zana sahihi, vitu ambavyo havitaleta usumbufu kwenye zoezi. Napenda kufanya zoezi ndani ya muda sahihi niliochagua, na mara nyingi nakwepa usumbufu wakati wa zoezi. Kuna suala la usalama ambalo pia linaniondolea wasiwasi wakati wa zoezi.

Pamoja na hayo yote nimegundua pia kuwa mambo mengine mengi yanaweza kuathiri mazoezi yangu. Kwa mfano, kuwa kwenye mood mbaya, ninapokua nimezongwa na mawazo, nashindwa kabisa kufanya mazoezi, sijui kwa nini. Hali ya hewa wakati mwingine umenikwamisha. Pengine mvua, kuna madimbwi, joto kali nk. Pia nahitaji kuwa katika hali njema kimwili. Kwa mfano wakati mwingine nimeshiba, au nina kinywaji tumboni, mwili unawasha, naumwa na kichwa, goti nk

Baada ya kujaribu mazoezi ya aina nyingi kama vile jogging kutembea kunyanyua mawe nk, hatimaye nikagundua kuwa zoezi la kuruka kamba linazingatia vigezo vyangu. Hivyo nikajaribu kwa namna mbalimbali kuliboresha zaidi, kwa kuyapunguza yanayoweza kuliathiri, na kuyaongeza yale yanayoboresha zoezi, nikatokea na mtindo huu.

20200329_1336315.jpg
  1. KAMBA: ya kawaida kabisa. Mwanzoni nilikua natumia kamba fulani ambayo ina counter, yaani inahesabu yenyewe wakati kamba inapozunguka. Niliipenda sana hiyo, lakini baadae nikagundua kuwa ina mapungufu. Mara nyingi inakua na ubovu, na inaruka namba, inahesabu vibaya na wakati mwingine haiesabu kabisa. Kamba hizo zenye counter zinakua nyembamba sana na hazina uzito ninaohitaji kwenye zoezi. Hivyo nilipogeukia kamba nyingine za kawaida, nikaona lazima nitafute namna nyingine ya kuhesabu kamba zangu.
  2. SIMU: yangu ya Tecno nimekua nikiitumia kwa mazoezi mengine kama kukimbia na kutembea. Nilipoanza zoezi la kuruka kamba, nikaanza kujaribu kutafuta apps mbalimbali ambazo zinaweza kuhesabu kuruka kwangu Mwaanzo nilitumia app inajulikana kama skeepjumping, ambayo baadae niliona ina mapungufu, wakati mwingine katikati ya shughuli inaacha kuhesabu, au inaanza mwazo. Baadae nikawa natumia nnyinggine inayojulikana kama Jumpro na hii ndio ninayoitumia wakati huu. Hii ni nzuri, isipokua wakati wa kuanza kuitumia lazima ufanye calibration kulingana na mtikisiko wa mwili wako unaporuka. Inaweza ikawa inahesabu mara mbili kwa mruko mmoja au isihesabu kabisa, inategemea umeifanyia calibration namna gani.
  3. ARMBAND: yangu ya kiyeboyebo, lakini inayonisaidia. Haka kamkoba nachomeka simu ndani yake, kisha nafungia kwenye mkono, ili ninaporuka, mruko uweze kuregister kwenye simu. Pengine hapa unaweza kuona inavyo valiwa Awali nilikua natumia kwa jogging, lakini sasa natumia kwa kuruka kamba.
  4. HEADPHONES: za bluetooth, nilinunua sabasaba. Awali nilikua natumia headphones zenye waya, zinafaa, lakini niliona kama vile waya unasumbua kidogo. Sipendi kabisa viheadphone vya kuchomeka masikioni havinipi raha, napenda hizi za kufunika masikio. Baada ya kuzi-pair na simu yangu, naweza kuisikia vizuri “Jumpro” inavyohesabu, kwahiyo najua nipo wapi katika round yangu ya kuruka, na pia nasikia muziki. Kwenye simu nimeinstall pia App ya kuchezesha muziki inayoitwa Musicolet hii ni app nzuri ya kuorganise miziki kwenye simu na kuichezesha. Unaweza kutengeneza playlists na queues ambapo kwa haraka unaweza kuchagua aina ya miziki unayotaka kusikia.
  5. BLUETOOTH KEYBOARD: Hii nilinunua kwa malengo mengine, lakini kwasababu inaunganisha vizuri sana na simu, naitumia moja kwa moja ku-control muziki wangu wakati wa zoezi. Inaniwezesha kuongeza sauti au kupunguza kwa miziki yenye namna tofauti za volume. Pia inaniwezesha kuskip forward au backward, ku-pause na kuendelea. Ku-mute nk. Hivyo nikisha ifungia simu kwenye Armband sihitaji kuitafuta kwaajili ya kurekebisha mambo, natumia keyboard hii.

  6. SOKSI: pamoja nanguo nyingine ndogo ambayo kimaadili si vizuri kuiweka hapa. Zoezi langu nafanyia chumbani. Nafunga mlango kisha nang’oa nguo zote nabaki na hizo ndogo za aina mbili. Hii inanipunguzia mambo ya kufua nguo zenye majasho ya mazoezi. Jasho kwa kweli linatoka sana, linaenda sakafuni na soksi hizi zinazuia kuteleza nk.
Zoezi nalipeleka namna hii. Naruka kamba 1,000 kwa dakika 11 au hata mpaka 15. Natumia round 5, ambapo kila round moja naruka kamba 200. Hiyo ni miziki 4 au 5 mizuri. Sifanyi zoezi kila siku, wakati mwingine nashindwa kwasababu ya shughuli, lakini ikipatikana nafasi nafanya. Hapa nina screenshot ya rekodi ya mazoezi
Screenshot_20200401-005729.png
Baada ya hapo nafanya mazoezi mengine madogomadogo kama vile push-ups, squats stretch mbalimbali na kucheza muziki. Kisha naoga maji ya moto.

Natamani sana kupata maneno ya kukuelezea ninavyojisikia baada ya hapo.

Mtindo huu wa mazoezi ni mzuri sana, maana unakuzuia kutokatoka hasa wakati huu wa Covid 19

Hapa nimeona wadau wengine wanaoelezana kuhusu zoezi hilo.

202003219_133825.jpg
 
Kukata miti ya mkaa na kusomba mkaa kwangu Mimi naona zoezi tosha maana si kwa kuchoka huku kila Siku..
Kazi zoezi tosha
 
Kukata miti ya mkaa na kusomba mkaa kwangu Mimi naona zoezi tosha maana si kwa kuchoka huku kila Siku..
Kazi zoezi tosha
Mazoez ya ain nyingi mzeee. Hilo nalo zoez ila akil haitafsir kama zoezi. Mazoez huleta raha na burudani flan amazing, beba mkaaa maliza, harafu siku piga tizi kama mwana hapo juuu then compare feelings zinazo ambatana.
 
Ok!..
Naona kabisaa ngumu ngoja labda kunawakati nitaacha hii kazi ndo nitaanza mazoezi
 
Mwandishi umenikumbusha kitu cha msingi chenye matokeo chanya katika maisha ya kila siku, ngoja na mimi nianze kidogo kidogo maana mwili unataka kuni-control badala ya mimi kuu-control.
 
Mkuu mimi nataka kujua jinsi hiyo arm band inavyofanya kazi kwa mtu anae jogging, na inapatikana vipi

Maana mimi napenda jogging, ila inaniwia ngumu kujua nmekimbia km ngap

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bas wewe ni kama mimi. Nilikua nafanya jogging pia, lakini bila kujua nimekimbia km ngapi ilikua inaniwia ngumu sana. Kwakweli hiyo arm band haifanyi chochote, maana ni kamkoba tu kenye velcro patches ka kuvaa sehemu ya juu ya mkono na ndani ya hako kamkoba unaweka simu yako. Click hapa uone picha mzungu alivyovaa Kinachohesabu shughuli yako ya kukimbia ni simu iliyo ndani ya armband. Wakati nilipokua nfanya jogging mwanzoni nilikua naiweka simu mfukoni, ila nikaona inakua kero sana maana kwenye mfuko wa track inacheza sana. Baadae nikanunua kapochi fulani nafunga kiunoni, lakini nayo ikawa hainogi sana, hadi nilipopata hii armband.
Sasa kwenye simu - android, nili-install app inaitwa Endomondo unaweza kuclick hapa kuiona. Kunaweza kuwa na app nyingine lakini hii niliipenda sana. Kama nakimbia nikiwa na headphones naskia muziki lakini mara kwa mara endomondo inapause muziki inanitangazia taarifa muhimu za mazoezi yangu, kwa mfano kwamba sasa nimetimiza kilometer moja, au mbili nk. muda niliotumia na speed yangu ipo namna gani. Wakati mwingine nilikimbia kuzunguka uwanja, na kama nataka kukimbia km 4, nakimbia hizo namaliza nimetosheka. Au nakimbia km 4 kwenye eneo fupi kwenda na kurudi hadi nakamilisha. Pia inatunza record za mazoezi yako, na inakupa pia ramani ya eneo ulilokimbia pengine siku nyingine utataka kulirudia au kushirikisha wengine, na taarifa nyingine nyingi za zoezi lako.
Armband yenyewe hii nilipewa na mtu aliyekua na mbili. Kuna wakati nilienda kariakoo, duka fulani la vifaa vya michezo mtaa wa Muhonda, wakaniambia walikua nazo zimeisha. Siku nyingine nikaingia maduka ya vifaa vya simu. Kutokea Juction Msimbazi na Uhuru, sambamba na Msimbazi nikaingia kushoto Aggrey, halafu maduka hapa upande wa kushoto Aggrey, nikaona moja pale bei chini kidogo ya elf kumi lakini rangi ya pink. Nikang'ang'ania kabisa kuichukua, (sielewi sana mambo ya rangi) wadau wakanigomea kabisa pale wakidai ni rangi ya akina dada, ikabidi niwe mpole.
 
Asante sana mkuu. Nimeelewa vizuri mno yani, ngoja nifanyie kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom