Mazungumzo ya Alfu Lela Ulela au Siku Elfu na Moja - Kitabu cha Pili

Mazungumzo ya Alfu Lela Ulela au Siku Elfu na Moja - Kitabu cha Pili

Sasa hatukuwahi hata kuvuta pumzi uzuri mara jiwe lingine liliporomoshwa, na hilo lilianguka kwa mshindo mkuu katikati ya jahazi yetu, ikavunjika vipande vipande. Abiria na mabalharia wote waliokuwamo wakazama baharini pamoja na mimi mwenyewe; walakini nilipata bahati nzuri ya kuibuka tena bila ya kuumia mahali. Nikashika kipande cha ubao kilichokuwa kikielea nikapata kuogelea, na mara ile ile nikapigwa na wimbi kunipeleka kisiwani. Pwani zake zilikuwa zimechongoka sana tena zilikuwa na mawe mawe, lakini nikapanda hivyo hivyo kwa kutamba taratibu mpaka nikafika juu salama, nikajilaza penye majani mororo, nikapumzıka.



Nilipoondoka nikaanza kwenda huku nikikichungua kisiwa, hata mwisho nikajiona nimefika kwenye bustani nzuri kulikokuwa na miti iliyozaa matunda na maua kochokocho, na kijito cha maji safi meupe kama kioo yakipita chini ya vivuli vyao. Hata usiku ulipoingia nikachagua mahali pazuri nikalala; lakini nilikuwa nikigutuka mara kwa mara na kuangalia huku na huku kwa woga, na hasa nikikumbuka kuwa ni peke yangu katika nchi ya ugeni, nikatamani sana niweko kwetu. Lakini huo usingizi nilioupata ulikuwa mtamu tena wa raha. Sasa kulipokucha nikawa mwana mume kamili na uwoga wote ukanitoka nikaanza kuzungukazunguka katika miti mara ingine, lakini kila nikizunguka hivyo nafsi yangu ilikuwa kama nitakayeona kitu. Basi nikazidi kuendelea mbele ndani ya kile kisiwa hata mwisho nikaja nikamtokea mzee mmoja aliyejikunja, tena mnyonge sana amekaa ukingoni pa mto. Kwanza nilimdhania kuwa ni baharia aliyevunjikiwa jahazi kama mimi. Nikamwendea kumwamkia lakini hakunijibu neno ila aliinamisha kichwa chake kuniitikia. Kisha nikamwuliza anafanya nini hapo. Ndipo akanifanyia ishara kuwa anataka kuvuka ule mto aende akachume matunda, na katika kumwangalia kwangu nikaona kama aniambiaye nimbebe nimvushe. Basi nikahuhurumia uee na unyonge wake nikambeba mabegani kumvusha, hat a nilipofika naye ng’ambo ya pili nikainama kusadi ashuke kwa urahisi, nikamwambia, ‘Sasa shuka.’ Lakini badala ya kushuka na kusimama kwa miguu yake mwenyewe (nh'u, hata sasa nikikumbuka hucheka!) kiumbe yule niliyemwona kuwa mkongwe akazidi kuniganda mabegan1 mwangu, tena akanifunga na miguu yake shingoni mwangu ikanibana sana hata nilikuwa siwezi kutoa pumzi. Na hivyo nilishindwa nguvu kwa woga, nikaanguka chini

nikazimia.

Hata nilipopata fahamu nikaona adui yangu bado yuko pale pale mahali pake, ijapokuwa alinilegezea kidogo ili nipate pumzi. Basi alipoona kuwa naanza kufufuka, akanipiga mateke hata ikanilazimu kuondoka na kwenda naye chini ya miti huku aende akichuma matunda ayatakayo akila. Mambo hayo yalikuwa yakiendelea mchana kutwa, na usiku nikilala huwa kama mfu kwa kuchoka, na yeye alikuwa akilala karibu yangu huku amenibana barabara shingoni. Na asubuhi kukicha haachi kunipiga mateke mpaka niamke, nianze tena mwendo wangu kwa hasira na uchungu.

Siku moja nikatukia kupita chini ya mti ambao chini yake kulikuwa na mamumunye makavu, nikatwaa moja nikatoa mbegu zake nikafanya kibuyu. Halafu yake nikakichukua na kukikamulia maji ya zabibu zilizokuwa zikilewalewa vichakani. Hata kilipojaa nilikiacha nikakiegemeza katika panda ya mti, na baada ya siku chache nilimchukua yule mzee nikaenda naye njia ile ile, na nilipofika huko nilichukua kile kibuyu changu nikanywa kiasi, na hivyo nilipata kuusahau uzito wa mzigo wangu niliouchukia, nikaanza kuimba na kuchezacheza. Basi siku hiyo yule mzee aliyeniganda

allpoona kwamba nikinywa maji yale ya zabibu huchangamka tena huweza kumchukua kwa urahisi zaidi ya siku zote, akanyosha mikono yake iliyo ngozi tupu na kushika kibuyu. Kwanza akaonja kidogo kwa hadhati, lakini halafu yake akagugumia yote hata tone lisibaki.



Hicho kibuyu nacho kilikuwa kikubwa, na mvinyo nao uilikuwa mkali sana hata naye pia akaanza kuimba na kuchezacheaza na nikiwa furaha sana kuona zile kucha za chuma zilizo katika vidole vya miguu yake ya kijini zilianza kulegea. Na kwa nguvu zangu zote nikamtupa chini na kutwaa jiwe nikamwua. Nilifurahi mno kutokana na balaa la shetani huyo mzee, nikaenda Kutukaruka mpaka pwani, ambako kwa bahati kubwa, nikakutana mabaharia waliotia nanga kusudi waje kule kisiwani kwa kula matunda na kuteka maji.

Wakasikiliza habari zangu kwa kustaajabu sana, nao wakasema ‘Uliangukia mikononi mwa Mzee wa Bahari, naye alikuhurumia sana kwa kutokunyonga kama vile anavyomnyonga kila mtu anayemchukua mabegani mwake. Kisiwa hiki chajulikana sana kwa visa vyake viovu, wala hapana mfanyaji biashara au baharia ateremkaye pwani akawa mbali na mwenziwe. Basi tulipokwisha kusema wakanichukua kunipeleka jahazini mwao, na huyo nahodha wao alinipokea kwa uzuri, na mara tukang’oa nanga kusafiri Baada ya siku kadha wa kadha tukafika katika bandari ya mji mkubwa uliostawi sana, ambao majumba yake yalijengwa kwa mawe, tukatia nanga. Basi mmoja katika wale wafanyaji biashara, ambaye alikuwa rafiki yangu sana humo njiani, akanichukua pwani; akaenda kunionyesha nyumba za kupanga wafanyaji biashara wageni zilizojengwa kando ya mji. Halafu akanipa na gunia moja kubwa, na akanionyesha watu wengine waliokuwa na magunia yao sawasawa na mimi. Akaniambia, ‘Nenda pamoja nao, ukafanye kama hivyo watakavyofanya, ila tahadhari usiwapotee, kwani ukipotea maisha yako yatakuwa katika hatari.

Baada ya hivi akanipa na chakula cha njiani, akaniaga. Nami nikatoka nikaenda pamoja na wale wenzangu wapya hata tukafika mahali penye minazi mingi iliyoshikana. Sasa nikafahanmu maana ya safari ile kuwa tumekwenda kujaza nazi magunia yetu. Nikiitazama ile minazi jinsi ilivyo mirefu mno na katikati miembamba, kisha yateleza sana, sikujua kabisa la kufanya. Na tena juu ya vilele vya minazi yote mlikuwa na manyani na matumbiri, wakirukaruka upesi upesi kwa kufadhaika kutoka mnazi huu hata mnazi ule; wakituchukulia wageni tu kisha twawaudhi mno kwa sura zetu. Basi wale wenzangu kwa hekima yao wakaokota mawe kuwarushia, na wale nyani walisumbuliwa mno hata nao wakapenda kujilipiza, ndipo wakaanza kukata nazi wakitutupia kwa hasira na chuki, na kwa njia hiyo tukapata kujaza magunia yetu, na kama si hivyo hatungalizipata. Basi tulipokwisha, kupata kadiri tulizoweza kuchukua tukarudi mjini. Rafiki yangu akanunua zile nazi zangu na kunishauri nizidi kuendelea kufanya kazi hiyo, mpaka nipate fedha za kutosha kunipeleka kwetu. Nami nikafanya hivyo, na baada ya si siku nyingi nikapata fedha za kitita. Sasa nikasikia kuwa kuna jahazi ya biashara ilivo tayari kuondoka, nikamuaga rafiki yangu nikaenda kujipakia pamoja na magunia ya nazi nyingi nilizokuwa nazo. Kwanza tukapitia katika kisiwa kilichopandwa pilipili, kutoka hapo tukaenda kisiwa cha Komari kilichoko Bara Hindi, ambako hupatikana udi mzuri. Hapo nikabadilisha nazi zangu kwa pilipili na udi. Kisha nikaenda mahali panapozamiwa lulu nikaajiri wazamiaji lulu. Hao wazamiaji lulu wangu walikuwa na bahati sana, na kwa muda mchache nikapata lulu nyingi mno, tena kubwa kubwa na safi. Nikarudi kwa furaha Baghdadi pamoja na mali hizi zote, nikaziuza kwa fedha nyingi mno na sikusahau kamwe kutoa fungu la kumi kuwapa masikini. Na baada ya hivi nikakaa kupumzika na kujifurahisha kwa anasa zote nilizoweza kupata kwa utajiri wangu.



Sindbad alipokwisha kutoa hadithi yake, akaamuru kwamba Hindbad apewe reale mia za dhahabu, na halafu wale wageni wote wakaaga, wakatoka. Lakini siku ya pili yake baada ya kuliwa karamu, Sindbad akaanza kutoa habari za safari yake ya sita, kama hivi ifuatavyo.
 
SAFARI YA SITA​



BILA ya shaka mtastaajabu kuwa baada ya kuvunjikiwa na jahazi mara tano na kupatikana na hatari zisizo hesabu, nikataka tena kusafiri. Hata mimi mwenyewe nikiangalia sana pia hustaajabu. Lakini nifanyeje kwani naona ilikuwa ni majaaliwa yangu kuzungukazunguka hivyo. Basi baada ya kupumzika mwaka mmoja nikatengeneza safari ya sita, na kusihiwa kote nilikosihiwa na ndugu nikae nisisafiri tena, sikusikia. Sasa, badala ya kusafıri kwa njia ya bahari ya Ajemi nkasafiri kwa nchi kavu, lakini mwisho wake nikajipakia katika jahazi, katika bandari moja ya Bara Hindi,

ya nahodha aliyeazimia kusafiri safari ya mbalii. Na hivyo ndivyo alivyofanya. Siku moja tulishukiwa na tufani kuu ambayo ilituvuta na kututoa kabisa katika mkondo wa njia yetu. Kwa muda wa siku kadha wa kadha si sarahangi wala si mshika sukani, hakuna aliyejua utokako waa’a twendako. Hatimaye tukaona kisiwa kidogo tukawa tunafurahi, lakini yule nahodha alivua kilemba chake na kukitupa chini, kisha akashika na ndevu zake akizing’oa, akasema kuwa katika bahari yote pale ndipo palipo na hatari sana, na ndiyo sababu ule mkondo wa maji ukatuvutia huko kusudi tuangamie. Na hivyo ilikuwa ni kweli! Na ijapokuwa mabaharia walifanya yote wawezayo ili tuepukane na hatari hiyo, lakini wapi! Jahazi yetu ikavutwa kwa nguvu kuelekea upande wa majabali yaliyoinuka na kuchongoka tokea baharini, na mara jahazi yetu ikapanda mwamba na kuvunjika vipande vipande. Walakini, ingawa ni kwa shida, tuliwahi kuchukua vyombo vyetu vya thamani tukashuka navyo pwani.
Basi tulipokwisha kufanya hivyo, nahodha akatuambia, ‘Maadam sasa tuko hapa na tuanze upesi kuchimba makaburi yetu, kwani hapana hata baharia mmoja aliyevunjikiwa na jahazi mahali hapa pabaya akarudi.’ Maneno haya yakatuvunja moyo sana. Yale majabali kwa upande wa baharini yaliumbika kama mpaka wa kisiwa kikubwa, na pwani yake tuliyosimama ilikuwa nyembamba yenye kutapanyika majahazi yaliyovunjika, na chungu za mifupa ya mabaharia waliokufa maji iking'aa myeupe kwa jua. Kuona hivyo tukatetemeka sana kwa kufikiri mifupa yetu karibu itaongeza chungu hizi! Tena, pwani ile yote ilitapakaa mali nyingi za thamani zilizokuwa ndani ya majahazi yaliyovunjika, na hazina nazo zilijaa tele tele katika vijipango vya miamba. Lakini Juu ya hayo, vitu hivyo vyote viliongeza ukiwa wa mahali hapo. Tena niliona jambo moja la ajabu sana ambalo lilinistua: nalo ni mto wa maji safi ya baridi yaliyokuwa yakichuruzika kwa nguvu kutoka katika mlima ambao haukuwa mbali sana na pale tuliposimama; badala ya maji kupita kwenda baharini kama vile inavyofanya mito mingine, yakawa yanazunguka kuingia katika pango la asili ndani ya ule ule mlima yasionekane yalikokwendea.
Hata nilipokwenda karibu kuchungulia ndani ya pango nikaona kuta zake ni nene kwa johari na almasi, na mawe mengi yanayon’ aa kama vioo, na sakafuni pametawanyika ambari. Basi hapo pwani ndipo tulipoziacha bahati zetu maana ule mlima ulikuwa haupandiki, na hata kama ingalikuja jahazi ingine nayo pia ingalighariki.
 
SAFARI SABA ZA SINDBAD, BAHARIA




KATIKA enzi ya Khalifa Harun Rashid, paliondokea mchukuzi mmoja masikini aliyekuwa akikaa katika mji wa Baghdadi, jina lake Hindbad. Siku moja jua lilipokuwa kali mno alitumwa kuchukua mzigo toka mwanzo wa mji mpaka mwisho wa mji, basi kabla hajafika nusu ya safari yake, akatokea katika njia moja iliyonyunyizwa marashi na upepo mzuri ulikuwa ukimpiga usoni,

akatua mzigo wake na kukaa kitako kando ya njia karibu na jumba

kubwa, ili kujiburudisha.

Alipokuwa amekaa hapo, akafurahi sana kusikia harufu za udi na ambari zikitokea mle ndani ya ile nyumba, na zaidi ya hayo alisikia ngoma na sauti za ndege zikiimba vizuri. Pia alisikia harufu ya vyakula vizuri na akafahamu kuwa ndani ya nyumba ile mna karamu. Basi kwa vile alivyokuwa hapiti njia ile mara kwa mara wala hana habari za mtu anayekaa katika jumba lile, akafanya hamu kupeleleza ili ajue, basi alipomwona mtumishi aliyekaa mlangoni akamwendea, na kumwuliza jina la bwana wake.

Mtumishi akajibu akistaajabu, 'Oh! Wewe umekaa hapa Baghdadi kwa siku kadha wa kadha, nawe hata leo hujajua kuwa jumba hili ni la Sindbad Baharia, msafiri mkubwa aliyezunguka dunia?

Mchukuzi aliposikia hivi akakumbuka maneno aliyoyasikia zamani kuhusu utajiri wa Sindbad; akiifikiri hali yake na hali ya Sindbad alimwonea kijicho. Akawaza kuwa kiasi cha furaha ya Sindbad ni sawasawa na kiasi cha taabu zake, naye akajinung’unikia sana hata moyo ukamchafuka, ndipo akainua macho yake mbinguni na kunena kwa sauti kuu, 'Ewe Mwenyezi Mungu, muumba wa vitu vyote, angalia tofauti kati ya Maisha yangu mimi na Maisha ya Sindbad! Kila siku naumia kwa taabu na mashaka hata ule mkate wa kula mimi na watoto wangu ni shida kuupata, huku kumbe Sindbad anatumia atakavyo na maisha yake ni furaha tupu! Amefanya nini hata ukampa raha hii, na mimi nimefanyaje hata nikastahili taabu hizi?'

Alipokwisha kusema hivi akainamisha kichwa kama mtu anayekata tamaa kabisa.



Basi mara ile ile nmtumshi akaja kutoka kwenye ile nyumba kumshika mkono akimwambia ‘Nifutuate, kwani bwana wangu, Sindbad, anataka kusema nawe.’

Hindbad akastaajabu sana maana hakujua analoitiwa, hata alipokumbuka yale maneno aliyokuwa akisema akaogopa sana akifikiri kuwa labda Sindband amesikia na sasa anaitwa kusudi kwenda kuadhibiwa. Kwa hivyo akatoa udhuru na kusema,

‘Siwezi kuacha mzigo wangu njiani’

Lakini watumishi wa Sindbad wakamwambia, ‘Sisi tutakutunzia

mzigo wako’, kisha wakazidi kumshurutisha mpaka akakubali. Basi wale watumishi wakamchukua kumpeleka katika chumba kikubwa ambamo aliona watu waliokaa juu ya meza iliyoandaliwa vyakula vizuri vya kila namna, na mwisho wa ile meza kulikuwa na mtu mmoja mwenye sura nzuri amekaa, naye alikuwa na ndevu nyingi nyeupe. Nyuma yake walisimama watumishi wengi tayari kufanya watakaloambiwa. Mtu huyo alikuwa ndiye Sindbad maarufu. Basi yule mchukuzi alipoona watu wengi kama wale akafanya hofu: akawaamkia huku anatetemeka, lakini Sindbad mwenyewe akamkaribisha akaa upande wa mkono wake wa kulia, kisha akamgawia chakula na mvinyo kwa mkono wake mwenyewe.

Walipokwisha kula Sindbad akawa anaongea naye kama watu waliojuana zamani, akamwuliza jina lake na habari zake. Mchukuzi akajibu, ‘Bwana wangu, Jina langu naitwa Hindbad.’

Sindbad akasema, 'Nimefurahi kukuona, nami nawasemea wote waliopo kuwa nao pia wamefurahi kukuona. Na sasa napenda uniambie yale maneno uliyokuwa ukisema kule njiani,’ maana Sindbad mwenyewe alimsikia akisema chini ya dirisha lake ndiyo sababu akamwita na kumkaribisha.

Alipoambiwa hivi, Hindbad akainamisha kichwa kwa haya, akajibu, 'Bwana wangu, wakati nilipokuwa nikisema maneno hayo nilikuwa nimechoka sana, na sasa naomba uniwie radhi.’

Sindbad akamwambia, ‘Usidhani kuwa raha hii na vitu hivi vya anasa nilivyo navyo sasa, nimevipata bure bila kusumbuka kwa taabu na mashaka ya dunia, la! Osifikiri hivyo, imefika hali hii niliyo, baada ya kuteseka miaka mingi kwa taabu za kiwiliwili na moyo pia.’ Kisha akawageukia watu waliokuwapo akawaambia, ‘Rafiki zangu, matajiri wako wengi-lakini kama wangalipata taabu namna nilivyopata mimi, wangalikata tamaa ya kupata utajiri tangu mwanzo, tena wangalikuwa radhi kurudi makwao katika hali ya umasikini. Labda hamjasikia habari za safari zangu saba za ajabu! Na hatari zilizonipata. Basi maadam leo nimepata nafasi ya kukwambieni habari za safari hizo, nitakwambieni.’ Na kwa kuwa Sindbad alitaka yule mchukuzi naye asikilize habari hizo, akamwamuru mtumishi wake aende kumchukulia ule mzigo wake ampelekee huko alikotaka kuupeleka, kusudi yeye akae kusikiliza hadithi.



SAFARI YA KWANZA​



BASI Sindbad akaanza kutoa hadithi yake hivi: -Babaangu alipokufa aliniachia mali mengi mno isiyo idadi; na fungu kubwa la mali hiyo nililitumia katüka starehe za ujana wangu, lakint halafu yake nikaona kuwa napoteza mali na hali pia, tena nikakumbuka kwamba mtu kuwa mzee kisha masikini ni mashaka makubwa mno. Baada ya kuingiwa na fikira hii, nikakusanya mali yangu yote iliyosalia nikaondoka na kwenda kujipakia chomboni pamoja na wafanyaji biashara, nikaenda Basra.

Tukasafiri kuelekea upande wa Mashariki kupita ghuba ya Ajemi. Awali ya safari yetu nilitaabika sana kwa bahari jinsi ilivyonilevya lakini baadaye nikaizoea, wala sikutaabika tena. Katika kusafiri kwetu tukapita visiwa vingi, tukawahi kuuza bidhaa zetu kidogo na zingine tukazibadılisha kwa vitu visivyopatikana katika nchi yetu. Hata siku moja tukafika katika kisiwa kingine kidogo kilichokuwa kimeinuka kidogo tu juu ya bahari. Basi baada ya kutua matanga, nahodha akatoa ruhusa kwa watu watakao kushuka pwani, washuke, na mimi nilikuwa mmoja wao.

Basi wakati tulipokuwa katika furaha zetu za kula na kunywa, na kujisahaulisha taabu za bahari, mara kile kisiwa kikaanza kuti- kisika sana hata wale wenzetu waliokuwa wamebaki chomboni wakakiona kikitikisika, nao wakatwita turudi upesi ili tujipakie tujiponye, kwani kile tulichodhani kuwa ni kisiwa hakikuwa kisiwa, ila ni mgongo Wa nyangumi. Waliokuwa wepesi wakangia mashuani tulioshukia pwani na wengine wakajitosa baharini kuogelea, na mimi kabla sijawahi kujiponya, kwa ghafla nyangumi akajizamisha baharini na kuniacha nikitapatapa majini kukimbilia kipande cha mti tulichokileta kutoka chomboni kwa kufanya kuni.
Lkn ndefu, japo ni nzr!
 
Jambo la kwanza alilofanya nahodha wetu ilikuwa kutugawanyia sawasawa vyakula tulivyokuwa navyo na kila mtu ilimwajibikia kutumia chakula chake taratibu, maana aliyetumia kidogo kidogo sana ndiye aliyeishi sana. Walakini katika siku ya mwisho niliyomzika mwenzangu mmoja, chakula changu kilichobakia kilikuwa kidogo sana, wala sikudhani kuwa kitaweza kunichukua hata nimalize kuchimba kaburi langu mwenyewe nililolianza kuchimba. Basi wakati huo nikajuta na kuilaani sana ile tabia yangu ya kuzungukazunguka ambayo siku zoote ilikuwa ikiniletea balaa. Lakini kwa bahati nzuri nikapenda nisimame kando ya mto kwa pale palipokuwa na pango lile linaloingilia maji hata yasionekane yanakokwenda. Basi niliposimama nikawaza: Mto huu unaojificha chini ya ardhi, sidhani kuwa hautokezei kweupe. Kwa nini siundi mtumbwi nikajisalimisha nao katika maji haya yanayopita kasi? Na kama nkiangamia kabla sijatokea huko kweupe haitakuwa vibaya kuliko hivi ilivyo sasa, kwani naona kifo chanikodolea macho usoni, na maadam siku zote yasemwa kuwa nilizaliwa na nyota ya bahati, pengine huenda nikawasili katika nchi nzuri. Mradi nikakusudia kubahatisha. Nikaunda upesi upesi mtumbwi madhubuti kwa mbao zilizokuwa zimepwelewa huko pwani na kuufunga barabara kwa kamba ili usichukuliwe na maji. Halafu nikakusanya mali nyingi za thamani, ambari, johari na zinginezo, nikazifunga mitumba na kuipakia mtumbwini, na zile zilizonishinda kuchukua nikazikusanya na kuziweka vema. Kisha nikaingia mtumbwini na kutwaa namna ya kafi mbili ndogo nikashika mikononi tayari, ndipo nikailegeza ile kamba iliyozuia. Mara mtumbwi wangu ukachukuliwa upesi na mkondo wa maji ndani kwa ndani katika pango la gıza, hata mwisho nikajiona niko katikati ya giza totoro. Na nilipofıka mbele kidogo ambako ule mto ulikuwa umepanuka nikawa nakokotwa polepole na maji yapitayo kasi. Nikaenda kwa siku nyingi mchana na usiku. Mahali pengine mlango wa maji ulikuwa mwembamba sana, hata ilikuwa ni bahati yangu kutopondwa na miamba. Basi kwa kule kujihadhari kwangu nikalala kifudifudi juu ya mitumba yangu ya mali. Tena, ijapokuwa nilikula kile kilichokuwa haja kula ili nisife, lakini baada ya kula hicho chakula changu cha mwisho nikaanza kuwaza, kuwa mwisho wa yote sina budi kufa kwa njaa. Haya basi! Nikawa nimechoka sana kwa wasiwasi huo nikalala usingizi mzito, hata milipoamka nikajiona nimetokea kweupe kwenye nchi nzuri, na baada ya kuufunga ule mtumbi wangu ukingoni pa mto, wakaja watu weusi kuuzunguka. Nikawaamkia nao wakanijibu, lakini lugha yao sikuifahamu. Ila nilijiona nafadhaika tu kwa kule kufufuka kwangu na kwa kule kutokea kweupe ghafla. Nikajiambia mwenyewe kwa mwenyewe kwa Kiarabu: Fumba macho yako, na wakati ulalao Mwenyezi Mungu ataibadilisha bahati yako mbaya iwe njema. Mmoja wa wale wenyeji, aliyekuwa anafahamu Kiarabu akanijia akasema, ‘Ndugu yangu, usistaajabu kutuona; hii ni nchi na hivi tulivyokuja kuteka maji tuliona mtumbwi wako mtoni. Na mmoja wetu aliogelea kwenda kuuleta pwani. Na tulivyokuona umelala, tumekungojea mpaka umeamka na sasa tuambie umetoka na wapi unakokwenda kwa njia hii ya hatari?’

Nikawajibu, 'Hapana jambo litakalonipendeza sana kama kuwambia habari zangu, lakini nina njaa ya Kufa nami naona nitazirai basi kwanza nipeni chakula.

Mara hiyo hiyo nikaletewa kila kitu nilichohitajia nikala nikashiba ndipo nilipowaambia yote yaliyonipata. Nao walistaajabu sana walipofasiriwa habari zangu, wakasema, Mambo yanayostaajabisha kama hivi yapasa kwenda kuambiwa mfalme na yeye mwenyewe. aliyepatikana na mambo hayo.

Basi wakaleta farasi, wakanipandisha, tukatoka kwenda kwa mfalme, huku tumefuatana na watu wengi wenye nguvu waliochukua mtumbwi wangu. Tukafika na kuingia ndani ya mji uitwao Serendib, ndipo wale wenyeji wakanipeleka mbele ya mfalme wao ambaye nilimwamkia kwa namna ya Kihindi, kwa kujiangusha miguuni pake na kusujudu na kuibusu ardhi. Lakini mfalme akaniambia niinuke nikae kitako karibu yake. Kwanza akaniuliza jina langu, nikajibu, Mimi ndiye Sindbad, niitwaye na watu Baharia, kwa kuwa nimesafiri sana baharini.

Mfalme akauliza, ‘Umefikaje hapa?’ Basi nikaanza kumweleza habari zangu zote wala sikumficha hata neno. Ama kustaajabu kwake na furaha aliyokuwa nayo ilikuwa kubwa mno hata akamuru kwamba masaibu yangu yaliyonipata yaandikwe kwa herufi za dhahabu, yawekwe kuwa kumbukumbu ya ufalme wake.

Punde si punde mtumbwi wangu ukaletwa pamoja na ile mitumba yangu na ikafunguliwa mbele yake, na mfalme akanena kuwa katika hazina yake hamna mawe ya thamani kama yale yaliyomiminwa chungu mbele yake. Kumwona anayatazama kwa kuyapenda nikabahatisha kumwambia kuwa, mimi mwenyewe na vyote nilivyonavyo vimo katika mamlaka yake, lakini akanijibu huku akicheka, 'La! Sindbad, Mwenyezi Mungu anakataza mtu kutamani mali isiyokuwa halalı yake; ila nitakuongezea, maana sipendi uondoke katika milki yangu bila kukuonyesha dalili ya wema wangu.

Ndipo akamwamuru akida wake kunipangia nyumba kwa gharama zake, na watumishi wakachukua mtumbwi na mitumba yangu mpaka katika hiyo nyumba yangu mpya. Basi fikiria mwenyewe jinsi nilivyosifu ukarimu wake. Nikampa ahsante na shukrani nyingi, wala kila siku sikuacha kwenda katika chumba cha baraza yake.

Katika kisiwa hicho cha Serendib, majira ya usiku na mchana yalikuwa sawasawa. Mji mkubwa anaokaa mtalme mwenyewe, ulijengwa mwisho wa bonde zuri ililopambika kwa mlima ulio mrefu sana katika dunia, ambao u katikati ya kisivwa hicho. Nikafanya hamu ya kuupanda juu kileleni, kwani hapo ndipo alipokimbilia Adamu alipotoka peponi. Mahali hapo huonekana mawe mengi ya thamani: kama johari na almas1 na mengineyo, na miti mingi bora bora inamea hapo, tangu mierezi hata mitende. Pwani yake na katika nidomo ya mito, wazamiaji lulu huenda wakitafuta lulu, na katika mabonde mengine hupatikana almasi. Basi baada ya kukaa huko siku kadha wa kadha nikawa namsihi mfalme aniruhusu kurudi kwetu, naye akaniridhia kwa wema. Na Zaidi ya hayo alinisheheneza kwa zawadi za mali, hata nilipokwenda kumuaga akanipa zawadi ya kifalme pamoja na barua kumpelekea Jemadari wa Uaminitu, yaani, ftalme wetu mwenye enzi, akiniambia, 'Nataka umpelekee Harun-al-Rashid zawadi hizi, tena umhakikishie urafiki wangu.' Basi nikazipokea kwa heshima, kisha nikajipakia ndani ya chombo alichonichagulia mwenyewe mfalme.

Ile barua aliyonituma ilikuwa imeandikwa kwa herufi za kibuluu Juu ya ngozi ya kimanjano yenye thamani, na maneno yaliyoandikwa yalikuwa haya:’Mfalme wa Bara Hindi, anayetanguliwa mbele kwa tembo elfu wanaokaa ndani ya jumba la kifalme, ambalo paa lake huwaka kama moto kwa vito vyekundu vya Johari elfu mia, na nyumba zake za hazina zina mataji elfu ishirini ya almasi: Nakuletea salamu Khalifa Harun-al-Rashid. Hata japokuwa zawadi nikuleteazo sikitu kikubwa twakuomba uzipokee kuwa ndiyo dalili ya heshima na urafiki wetu kwako, na hivi twafurahi kukuletea dalili hiyo, nasi pia twataka kwako heshima kama hiyo, kama ukiona twastahili. Kwaheri, ndugu.’

Ile zawadi niliyotumwa kupeleka ilikuwa ni gudulia moja la Johari lililonakshiwa, na urefu wake ulipata kama nusu futi, na maki yake kama kidole changu, nalo lilijazwa lulu kubwa kubwa za Kuchagua zilizo nzuri kabisa; na ngozi moja ya joka kuu lililokua na magamba kama reale, ambayo huwahifadhi na maradhi wale wanaoilalia. Kisha pia nikapewa na udi mwingi, na karafuu maiti na lozi. Mwisho nikapewa na mavazi ya kumeremeta ya nyuzi za zari na hariri.

Baada ya safari yetu ya siku kadha wa kadha mwisho tukafika Basra nami nikafanya haraka kwenda Baghdadi kupeleka ile barua ya mfalme, nikaenda mpaka nikafika kwenye lango la jumba la mfalme pamoja na jamaa zangu wengi waliochukua zile zawadi. Basi nilipokwisha kuwatolea habari zangu wale askari wa mlangoni mara wakanichukua kunipeleka mbele ya Khalifa, baada ya kumwinamia kumshika miguu, nikampa ile barua na zawadi. Hata alipokwisha isoma na kuangalia zile zawadi, akaniuliza kama mfalme wa kisiwa cha Serendib alikuwa tajiri kweli, na mwenye nguvu kama hivo anavyojigamba.

Nikainama tena kwa unyenyekevu mbele yake, nikajibu, 'Ewe Jemadari wa Uaminifu, naweza kukuhakikishia kuwa utajiri wake ni mkuu na enzi yake imetukuka mno, wala hapana kitu kilichozidi uzuri wa jumba lake tukufu. Anapokwenda safari, kiti chake cha enzi huwekwa juu ya mgongo wa tembo, na karibu yake hukaa mawaziri wake, na wapenzi wake, na watu wake wa baraza. Juu ya shingo ya tembo hukaa akida wake mwenye mkuki wa dhahabu mkononi mwake, na nyuma husimama akida mwingine achukuaye fimbo ya dhahabu, na juu ya fimbo hiyo pana zumaridi ndefu kama mkono wangu. Na watu elfu waliovalia nguo za dhahabu wamepanda juu ya tembo elfu waliopambwa kitajiri hutangulia mbele yake. Basi maandamano hayo ya mwendo wa taratibu yakiendelea mbele, yule akida aongozaye tembo wake hupiga mbiu, na kunena: "Mwangalieni mfalme mwenye enzi, aliye shujaa na mwenye nguvu, Sultani wa Bara Hindi, jumba lake limeezekwa kwa vito vyekundu vya johari elfu mia, tena ana mataji elfu ishirini ya almasi. Mwangalieni mfalme mkuu aliye kuliko Suleman na Maharaja, pamoja na utukufu wao wote!”

Kisha yule mmoja asimamaye nyuma yake hujibu hivi: "Mfalme huyu mwenye enzi na nguvu, lazima afe, lazima afe, lazima afe!”

‘Tena yule wa kwanza husema hivi: “Wote na tumsifu huyo aishiye milele.”

‘Zaidi ya haya, Seyid yangu, huko Serendib hakuna kadhi, kwani mfalme mwenyewe ndiye ahukumuye watu wake.’

Basi Khalifa akatosheka sana na habari hizi, akasema, 'Kwa barua hii inayotoka kwa mfalme naona mtu mwenye akili, tena naona anastahili kuwaongoza watu wake, na watu wake wanastahili kuongozwa nay eye.’

Alipokwisha kusema hivi akanipa zawadi za mali, ndipo nami. nikarudi nyumbani kwangu kwa amani. Basi Sindbad alipokwisha kusema, Hindbad akapewa mfuko wa reale mia za dhahabu, halafu yake wageni wote wakaondoka. Lakini waliambiwa kurudi tena siku ya pili waje wasikilize habari za safari ya saba. Basi Sindbad akaanza hivi:
 
SAFARI YA SABA, YA MWISHO​



BAADA ya safari yangu ya sita nikaapa kuwa sitasafiri tena, maana kwa ule umri wangu sasa ilifaa kukaa nistarehe, kwani mashaka yaliyonipata yalinitosha si haba. Basi nikapenda kukaa ili nimalize siku zangu kwa amani. Lakini siku moja nilipokuwa nikiwakirimu rafiki zangu, nikaambiwa kwamba akida wa Khalifa yuko nje mlangoni amekuja kutaka kuonana nami, hata alipokaribishwa kupita ndani akasema kuwa ametumwa kuniambia kwamba nifuatane naye mpaka mbele ya Harun-al-Rashid, ananiita, nami nikaondoka nikaenda. Baada ya kumwamkia, Khalifa akaniambia, ‘Sindbad! Nimekwita, sababu nina utumwa unifanyie. Nimekuchagua wewe uwe mpelekaji wa barua na zawadi hizi kwa mfalme wa Serendib, iwe ndio majibu ya barua yake na zawadi alizoniletea.’

Ama kwa amri hiyo ya Khalifa, nikawa kama niliyepigwa na radi. Nikasema, ‘Ewe, Jemadari wa Uaminifu, mimi ni tayari kutanya yote unayoamuru, lakini nakuomba ukumbuke kuwa nina huzuni kabisa, maana katika safari zangu zote nimekutwa na mateso mengi ambayo hayana hesabu. Nami kwa hakika nimeapa kuwa sitaondoka tena Baghdadi.’

Khalifa akasema, ‘Nakubali kuwa ulipatwa na mambo ya hatari Sana katika safari zako zote, lakini sioni sababu ya kukuzuia hata usinifanyie hili nitakalo. Nataka uende moja kwa moja mpaka kwa mtalme wa Serendib ukampelekee barua yangu, baada ya hivyo una ruhusa kufanya utakavyo. Lakini lazima uende, maana Cheo changu na utukufu wangu ndivyo utakavyo.’ Basi kuona sina njia ya kutolea udhuru wo wote, nikakubali kwenda, na Khalifa akafurahi sana kupata alivyotaka hata akanipa reale elfu za dhahabu kwa gharama za safari yangu, kisha akaniombea na Mungu nipate safari ya heri. Basi mara ile ile nikawa tayari kusafiri, nikachukua barua na zawadi nikaenda Basra kujipakia jahazini. Na muda ule ule jahazi yetu ikang'oa nanga, nikasafiri salama mpaka Serendib Nikashuka nikaenda kwenye lango la jumba la mfalme; nilipokwisha kutoa ujumbe wangu nikapelekwa mbele ya mfalme naye akanipokea kwa furaha kuu.

Akasema, 'Karibu, Sindbad, karibu! Mara kwa mara nilikuwsa nikikufikiri, na leo nimefurahi mno kukuona tena. Basi baada ya kumshukuru kwa heshima aliyonifanyia, nikamwonyesha zawadi za Khalifa alizomletea. Kwanza ilikuwa kitanda kamili chenye chandarua na nguo za zari thamani yake reale eltu za dhahabu, na kingine kama kile cha rangi ya zambarau. Na majoho hamsini yenye kutarizwa nyuzi za dhahabu, na nguo mia za kitani nyeupe zilizotoka Kairo, na Suez, na Kufa, na Skandaria, Na shanga nyingi za kila aina, na gudulia moja a jiwe la marmar lililochongwa umbo la mtu anayemlenga simba mshale, na meza moja ya thamani zamani ilikuwa ya mfalme Suleman. Mfalme wa Serendib akapokea zawadi hizo kwa kuridhika sana na kuhakikisha urafiki wa Khalifa alionao juu yake. Sasa kazi yangu ikawa imekwisha, nikatamani kurudi kwetu; lakini ilichukua kitambo kabla yule mfalme kuniruhusu kuondoka. Walakini, mwisho wake akanipa ruhusa pamoja na zawadi nyingi, nami sikukawia kwenda kujipakia jahazini ambayo saa ile ile iling’oa nanga na kusafiri. Basi kwa muda wa siku nne safari yetu ikawa njema, hata siku ya tano tukapata hasara kwa kutokewa na wezi walioikamata jahazi yetu, wakawaua wote waliojitetea, na wale waliosalimu amri wakafungwa mara moja, na mimi nilikuwa mmoja wao. Walipokwisha kutunyang'anya vyote tulivyokuwa navyo, wakatulazimisha kuvaa matambara na wakatuchukua kutupeleka kisiwa cha mbali, wakatuuza utumwani. Mimi nikanunuliwa na mfanyi biashara tajiri na kunichukua nyumbani kwake, akanivisha na kunilisha vema na baada ya siku siku kidogo akaniita kuniuliza kazi ninayo ijua.

Nikajibu kuwa mimi nilikuwa mfanyi biashara tajiri niliye kamatwa na wevi, lakini sikujua kazi ingine yoyote.

Akasema,'Niambie kweli, je, waweza kupiga mshale?’ Nikamjibu kuwa huo ndio uliokuwa mchezo wangu zama za ujana wangu, na hivyo sina shaka, kama nikijizoeza tena ustadi wangu utanirudia.

Basi kwa maneno haya akanipa upinde wa mshale kisha nikapanda pamoja naye juu ya tembo wake. Tukashika njia mpaka ndani ya mwitu mkubwa mno uliokua mbali na mji. Tulipofika katikati yake tukasimama, na bwana wangu akaniambia, ‘Mwitu huu umejaa makundi ya tembo, basi Jifiche juu ya huu mti mkubwa, wafume wote wanaokupitia karitu: na hapo utakapofaulu kumwua mmoja rudi nyumbani uje uniambie.’

Alipokwisha kusema hivi akanipa chakula naye mwenyewe akarudi mjini, nami nikapanda juu kileleni nikakaa kuangalia chini. Usiku ule nisione kitu, lakini asubuhi yake baada ya jua kutoka tu, nikaona kundi kubwa la tembo linakuja kwa vishindo na kuvunjavunja miti. Mara nikaiachilia mishale yangu na mwisho wake mmoja wao alianguka chini akafa, na wengine wakakimbia. Nikashuka chini ya mti niliojificha na kukimbilia mjini kwenda kumwambia bwana habari za kufanikiwa kwangu, na kwa hivyo nilisifiwa sana na kuandaliwa vitu vizuri vizuri.

Halafu tukatoka tukaenda pamoja na bwana wangu mpaka kule mwituni, tukachimba shimo kubwa ambamo tulimzika yule tembo niliyemwuwa, ili kusudi atakapooza bwana wangu arudi kuchukua pembe zake. Basi mradi nikawa mwinda muda wa miezi miwili, wala hapana siku iliyopita bure bila kuua tembo. Lakini fahamuni kwamba siku zote hizo nilikuwa sikai mahali pamoja, mara leo niko mti huu na kesho mti mwingine. Hata asubuhi moja nilipokuwa nikiangalia tembo wanaokuja, nikastaajabu kuona kuwa badala ya tembo kupitia chini ya mti niliopanda, kama vile ilivyokuwa desturi yao, siku ile walisimama kidogo na kuuzungukazunguka ule mti huku wakipiga baragumu zao za kutisha hata nchi ikatikisika kwa vishindo vya miguu yao. Na nilipoona wamenikazia macho kunitazama nikaogopa sana, hata ile mishale yangu ikanitoka mkononi kwa kutetemeka, ikaanguka chini. Kwa hakika wacha niwe na hofu, maana yule tembo mkubwa aliushika ule mti niliopanda juu kwa mkonga wake akaung’oa mara moja, nami nikaanguka chini na kuzingwazingwa na matawi yake nikaona kuwa sasa saa yangu ya mwisho imewadia; lakini yule tembo mkubwa aliniokota kwa upole na kuniweka mgongoni mwake kunichukua, na kundi zima likafuata kwa vishindo na kelele moja kwa moja ndani ya mwitu, nami nikawa nimeng’ang’ana kama mfu kwa woga. Hata nilipoteremshwa chini kusimama, nikajiona kama ninayeota ninaangalia kundi la tembo wanapita wakivunjavunja miti kwendea upande mwingine, na kupotea ndani ya mwitu wasionekane tena. Hata nilipopata fahamu na Kutazama huku na huku nikajiona nimesimama upande wa kilima kikubwa kulikotawanyika mifupa na pembe za tembo. Nikasema moyoni mwangu, ‘Hapa hapakosi kuwa ndipo mahali pao wanapozikana, tena labda wamenileta hapa kusudi ili niache kuwawinda wameona kuwa sina kitu nitakachho 1la pembe zao, na hapa zipo nyingi zaidi kuliko ninazoweza kuzichukua umri wangu wote.’
 
New Doc 2022-01-01 180932_page-0023.jpg
 
Haya basi! Nikafanya safari ya kurudi mjni upesi, wala humo njiani sikukutana na tembo hata mmoja, na hivyo ilinisadikisha kuwa wamekwenda mbali sana kusudi ile njia ya kwendea Kilima cha Pembe iwe wazi; ama sijui vipi nizisifu akili zao. Basi baada ya mwendo wa kutwa na kucha nikafika nyumbani kwa bwana wangu, naye aliponiona alinipokea kwa furaha na mastaajabu.

Akasema kwa sauti kuu, 'A, masikini Sindbad! Nilikuwa nikifikiri jambo gani lililokupata. Maana nilipokwenda kule mwituni niliona ule mti uliopanda juu umeng’olewa na mishale yako imeanguka kando yake, na tangu wakati huo nikawa na hofu kuwa sitakuona tena. Nakusihi uniambie jinsi ulivyoyaepuka mauti.’

Basi nikamweleza yote, na siku ya pili yake tukatoka tukaenda pamoja mpaka kule kwenye Kilima cha Pembe, naye akafurahi sana kuona yote niliyomwambia ni kweli. Tulipokwisha kumpakia tembo wetu pembe nyingi kwa kadiri alivyoweza kuchukua tukawa tunarudi mjini, humo njiani akasema, Ndugu yangu tangu leo siwezi kumfanya mtumwa mtu aliyenitajirisha namna hii chukua uhuru wako, na Mwenyezi Mungu akujalie baraka. Nami sitakuficha tena kukuambia kwamba tembo hawa wametutulia watumwa wetu wengi kila mwaka, ila wewe pekeo ndiye uliyenusurika na hila za nyama hawa, na hivi naona kuwa bila ya shaka una kinga ya Mungu ya namna ya peke yako. Na sasa mji mzima utatajirika kwa ajili yako bila hasara ya kuuawa mtu, na kwa sababu hiyo sitakupa uhuru tu, ila nitakupa na mali.’

Ndipo nami nikajibu, ‘Bwana wangu, nakushukuru sana, tena nakuombea Mungu akupe baraka nyingi. Ama mimi naomba uhuru na ruhusa ya kurudi kwetu tu basi.’

Akajibu, ‘Vema, msimu wa jahazi za kuchukua pembe karibu utakuja basi hapo ndipo nitakapokusafirisha na kitu cha kuweza kulipia nauli yako.’

Basi nikakaa naye mpaka wakati wa msimu, na kila siku tukawa tunakwenda kuchukua pembe kuongezea ghalani mwetu, mpaka ghala zake zote zikawa zinafurika kwa pembe. Wakati huo ikawa na wafanyi biashara wengine kuibaini siri ile, lakini kule bondeni ilikuwako pembe nyingi za kuwatosha wote. Hata jahazi za msimu zilipokuja bwana wangu akanichagulia moja aliyoipenda nisafirie, akanipakilia vyakula vingi, na pembe nyingi na tunu zote za thamani zinazopatikana katika nchi ile. Ama kwa hakika nilimshukuru sana, kisha tena tukaagana nikasafiri.

Hata nilipofika bandari ya kwanza nikateremka, nikawa nimefanya wasiwasi kuzidi kusafiri baharini kwa sababu ya yale yaliyonipata zamani. Basi nikauza pembe zangu kwa thamani kubwa, tena nikanunua na zawadi nyingi zilizo nzuri nzuri nikamtwesha ngamia wangu, nikaungana na msafara wa wafanyi biashara. Safari yetu ilikuwa ndefu tena ya kuchokesha, lakini nilivumilia hivyo hivyo, maana niljiona sina hofu tena juu ya upepo mkali wa baharini, wala ya wevi, au ya majoka, au hatari zingine zo zote zilizonitesa zamani, na mwisho wake tukafika Baghdadi. Jambo la kwanza nililofanya ni kujitokeza mbele ya Khalita, na kumpa habari ya kazi aliyonituma. Naye aliniambia kwamba kutorudi kwangu upesi kulimtia wasiwasi sana, walakini pamoja na hayo alitumai kuwa nitarudi salama. Basi nilipomweleza habari za mambo yaliyonipata ya tembo akastaajabu mno, akasema kama angalikuwa hayajui yaliyonipata kabla hangeweza kusadiki.

Basi kwa amri yake, hadithi hii na zile zinginezo nilizomwambia ziliandikwa na makarani wake kwa herufi za dhahabu, zikawekwa katika hazina yake. Halafu nikamwaga kwenda nyumbani kwangu, hali nimeridhika sana kwa heshima aliyonifanyia na kwa zawadi alizonipa; na tangu siku hiyo nikapumzika na kazi za kusafirisafiri, nikakaa mjini pamoja na jamaa zangu na rafiki zangu.



Hivi ndivyo Sindbad alivyoimaliza hadithi yake ya saba, ambayo ndiyo iliyokuwa safari yake ya mwisho. Kisha akamgeukia Hindbad, akamwambia, ‘Je, rafiki yangu, waonaje sasa? Ulipata kusikia mtu ye yote aliyeteseka zaidi, au aliyenusurika na mauti mara nyingi zaidi kuliko mimi? Si haki kwamba sasa nifurahi na kuishi kwa raha mustarehe!’

Hindbad alipoambiwa hivi, akasogea karibu yake na kumbusu mikono kwa heshima, akajibu, ‘Bwana wangu, kwa hakika ulipambana na hatari zinazotisha, maisha yangu hayawezi kufanana na maisha yako, na zaidi ya hayo, kwa ukarimu wako unastahili kuwa tajiri, Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu ya furaha na vicheko.’ hlafu Sindbad akatoa reale mia za dhahabu akampa, na tangu siku hiyo akawa katika rafiki zake wakubwa na akamfanya aache kazi yake ya uchukuzi, na kila siku aende akale chakula kwake ili katika ya maisha vake yote amkumbuke Sindbad, Baharia.
 
KISA CHA MBILIKIMO MWENYE KINUNDU​



KATIKA milki ya Kashga, ambayo kila mtu aijua, paliondokea mtu na mkewe waliokuwa wakipendana sana, na huyo mume kazi yake ilikuwa kushona. Hata siku moja alipokuwa kashughulika na kazi akatokea mbilikimo mwenye kibiongo akakaa kwenye mlango wa duka akaanza kuimba na kupiga kigoma chake. Mshoni akafurahika sana na kuchezacheza kwake, hata akafikiri kumchukua kwake ili akamfurahishe mkewe. Basi mbilikimo alipokubali kufuatana naye, mara yule mshoni akafunga duka lake wakatoka kwenda zao. Walipofika nyumbani wakakuta meza imeandaliwa tayari kwa chakula cha jioni, na baada ya dakika chache wote watatu wakakaa kula samaki aliyekaangwa vizuri na mke wa mshoni. Lakini ah! masikini, yule mbilikimo alikwamwa na mwiba mkubwa kooni, na kabla ya yule mshoni na mkewe kuwahi kumsaidia autoe, mara akafa.
 
Na juu ya kumsikitikia kwao sana, walijiogopea sana nafsi zao maana kama askari wakisikia, mtu na mkewe huenda wakafungwa gerezani kwa hatia ya kuua.

Basi kwa kutaka kuficha jambo hili la kutisha mno, wote wawili wakakaa kutunga mpango ambao utaleta shaka juu ya mtu mwngine, na nwisho wake wakaona hawana hila ila wamsingizie yule mganga wa Kiyahudi aliyekuwa akikaa karibu, kuwa ndiye aliyefanya uhalifu huo. Ndipo yule mshoni akamshika mbilikimo kichwani na mkewe miguuni wakamwinua, na kumchukua mpaka nyumbani kwa mganga. Wakabisha mlango na mara mtumishi aliyekuwa juu ghorofani, yeye na bwana wake, akashuka chini kuwauliza habari.

Mshoni akasema, ‘Mwambie bwana wako kuwa tumekuja na mtu mgonjwa ili amwague,’ kisha akasema na huku akimshikisha fedha mkononi, ‘Mpe hizi kifungua mkoba wake asione kuwa atapoteza bure wakati wake.’ Mtumishi akapanda tena ngazi kwenda kumpasha habari bwana mganga

Na kiasi ya yule mtumishi kutoweka machoni pa mshoni na mkewe, huku nyuma wakamchukua upesi yule maiti wakaenda kumwegemeza na kiguzo cha ngazi ya darini, nao wakarudi mbio kwao. Mganga alipendezewa sana kupata habari za mgonjwa maana alikuwa ni kijana, tena hakuwa na wagonjwa wengi, na hivyo alijaa furaha. Akamwambia mtumishi wake, ‘Chukua taa unifuate upesi,’ naye mwenyewe akatoka chumbani mwake kwa haraka kukimbilia kwenye giza, nusura auwangukie mwili wa kibiongo. Na bila kujua ni kitu gani akaupiga teke na mwili huo! Ukabingiria mpaka chini. Tena ilikuwa nusura umbingirishe na yeye mwenyewe pia

Mganga akaita, 'Lete taa! lete taa! Hata taa ilipoletwa na kuona jambo alilofanya akawa na hofu kuu. Akasema, Toba! Musa Nabi, kwa nini sikungojea taa? Nimekwishamwua mtu waliyeniletea nimwague, na kama nisipopata msaada, basi nimekwishapotea, kwani haitachukua kitambo tena kabla sijakamatwa kupelekwa gerezani kuwa ni mwuaji.

Na ingawa alifadhaika sana kwa sababu hiyo, lakini hakusahau kufunga mlango wake, ili kwamba wale watu wapitao wasije wakaona. Mradi akamchukua yule maiti akampeleka katika chumba cha mkewe; na hivyo ilikuwa nusura mkewe aingie kichaa kwa hofu.

Mkewe akalia kwa huzuni akinena, ‘Balaa imetushukia! Ikiwa hatutapata njia ya kumtolea maiti huyu nyumbani mwetu, hapo Jua litakapotoka hatutaweza kumficha tena. Lakini ilikuwa namna gani hata ukafanya makosa kama haya?’ Mganga akasema, ‘Hayo yaachilie mbali, ila iliyopo sasa ni kutafuta njia ya kumtolea. Basi kwa muda wa saa mbili tatu ikawa yule mganga na mkewe kugeuzageuza mashauri kwa kutafuta njia ya kujinusuru, lakini wapi! Hawakupata hata moja la kuwafaa. Mwisho wake mganga akawachilia mbali ikawa ni kujizatiti kwa lo lote litakalokuwa. Lakini yule mkewe ambaye alikuwa na akili kumshinda yeye mara ghafla akanena, 'Nimefikiri neno moja. Twende tumchukue huyu maiti mpaka juu ya paa, kisha tumteremshie ndani ya bomba la moshi la yule jirani yetu Mwislamu. Na wakati ule yule Mwislamu alikuwa akipaka mafuta meza ya sultani, na sehemu ya nyumba yake ilikuwa na chumba kikubwa cha vyakula, ambamo panya na vipanya walikuwa wakifanya karamu zao.

Basi yule mganga panmoja na yule mkewe, wakamwinua kibiongo na kumpitisha kamba makwapani mwake wakamteremsha ndani ya chumba anacholala mtoaji chakula wa sultani. Hata walipojua kuwa amegusa chini wakazivuta juu kamba polepole na kumwacha mumo humo wakarudi kwao; na kibiongo alionyesha kama aliyeegemea ukuta kweli.

Wale kule kufika kwao tu, mara mtoaji chakula wa sultani akaingia chumbani mwake. Kwani wakati huo alikuwa akitoka harusini usiku, naye alikuwa na taa yake mkononi. Basi kwa ile nuru ya taa akastaajabu sana kuona mtu amesimama katika bomba la moshi, na vile alivyo shujaa akashika fimbo na kumwendea yule mtu aliyemdhania ni mwivi. Akasema, “A, kumbe ni wewe unayeniibia siagi yangu, wala si panya na vipanya! basi leo utani tambua, wala hutatamani tena kurudi hapa.”

Kusema hivi akamwingilia kumpiga mpaka yule mbilikimo akaanguka chini, lakini vile vile akaendelea kumpiga, hata mwisho akastaajabu kuona yule mwivi amelala kimya hatikisiki, wala hajitetei. Basi katika kule kumwona amekufa, mara hofu ikamwi ngia, akasema, “Mama we! Balaa imenishukia, nimekwisha ua mtu, Toba! Kisasi changu kimepita mpaka, na pasipo msaada wa Mungu nimeangamia!” Mradi akajiona kuwa kamba za shingo zimekwisha mzunguka.

Lakini ile hofu ya kwanza ilipomtoka, akaanza kufikiri njia ya kuepukana na matata, ndipo akamkamata mikono mbilikimo na kumkokota nje barabarani akamwegemeza na ukuta wa duka moja, naye mwenyewe akarudi nyumbani kwake, bila kutazama nyuma hata mara moja. Baada ya dakika chache kabla ya jua halijatoka mfanyibiashara Mkristo tajiri, anayekopesha katika jumba la sultani kila namna ya vitu vinavyohitajiwa, akatoka nyumbani kwake, baada ya karamu

ya usiku, kwenda pwani kuoga. Ingawa alikuwa amelewa sana lakini alikuwa na fahamu ya kujua kwamba kupambazuka ku karibu, na hivyo Waislamu wote karibu watakwenda kusall. Mradi akazihimiza hatua zake ili asije akakutwa na mmoja anaye kwenda msikitini, ambaye akimwona hali yake aliyo mara atamkamata ampeleke mahakamani kuwa ni mlevi.

Basi katika ile haraka yake aliyokuwa nayo akampiga kumbo mbilikimo naye akamwangukia, kuona vile akafikiri kuwa anataka kupigwa na mwivi, ndipo akafanya haraka kumpiga ngumi akambwaga, kisha akapiga kelele kuita watu, huku anazidi kumpiga tu.

Mku wa askari anayeangalia nyumba akaja mbio, akamwuliza kwa hasira, “Wafanya nini?”

Mfanyi biashara akajibu, “Alijaribu kunibia, tena alikuwa karibu kunikaba roho.”

Askari akamshika mkono akimwambia, “Basi mwache, umekwisha lipiza kisası chako. Haya! na wewe nenda zako.”

Alipokwisha kusema hivi akanyosha mkono wake kumsaidia mbilikimo lakini mbilikimo hakuinuka. Hata yule askari alıpoinama kumtazama kwa karibu, akanena: “Oho! Kumbe ndiyo hivi ulivyofanya!” pale pale akamkamata mfanyi biashara na kumpeleka kwa msimamizi wa askari, ambaye alimtia gerezani mpaka hakimu aamke usingizini na kuwa tayari wa kusikiliza hukumu yake.

mfanyi biashara ulevi wake wote aliokuwa nao ulimtoka, lakini kila akifikiri sana hakuweza kufahamu Jinsi yule mbilikimo alivyokufa kwa kupigwa ngumi tu. Hata hapo mfanyi biashara alipoitwa mbele ya mkuu wa askari kuulizwa makosa yake ambayo hakuweza kukana, alikuwa bado angali akifikiri jambo hilo.

Kwa kuwa yule mbilikimo alikuwa ni mmoja wa watu wanaomchekesha sultani, mkuu wa askari akakusudia kukawilisha hukumu mpaka amshauri sultani mwenyewe, na hivyo akaenda nyumbani kwa sultani na kuomba ruhusa ya kuonana naye ili apate kumhadithia habari zake, na sultani akajibu: “Hakuna kusamehewa kwa mwuaji. Nenda ukafanye kazi yako.”
 
Basi mkuu wa askari akaamrisha mahali pa kunyongea pajengwe, Kisha akatoa na wapigaji mbiu waende kila barabara ya mjini watangaze kuwa siku ile kutanyongwa mwuaji.

Hata yote yalipokuwa tayari mfanyi biashara akatolewa gerezani kwenda kunyongwa. Huyo mnyongaji alitwaa kamba na kuipiga fundo barabara kisha akaizungusha shingoni mwa mtu yule asiye na bahati, tena alikuwa karibu kumning’iniza hewani, mara yule mtoaji chakula wa sultani akaja mbio akitweta sana huku akipasua kundi la watu, akamwambia mnyongaji, "Ngoja, ngoja, usifanye haraka. Kwani huyo siye aliyeua, ila ni mimi.”

Yule mkuu wa askari ambaye naye alikuwako pale pale akiangalia kila kitu kifanyike sawa, akamwuliza mtoaji chakula wa sultani maswali mengi, naye akamhadithia habari zote za kifo cha mbiikimo na jinsi alivyomchukua maiti mpaka pale alipokutwa na yule Mkristo mfanyi biashara.

Akaendelea kumwambia mkuu wa askari, “Mwamwua bure mtu asiye na hatia, kwani haiyumkini kuwa yeye aweza kuua mtu aliyekwisha kufa. Tena ni vibaya sana kwangu: ya mimi kuua kisha nimwachie mtu asiye na hatia ateswe kwa ajili ya kosa langu.”

Maneno haya aliyasema kwa sauti kuu yule mtoaji chakula wa sultani, na kila mtu aliyekuwapo aliyasikia, na kama sivyo yule mfanyi biashara hangefunguliwa.

Mkuu wa askari akamgeukia mnyongaji akamwambia, 'Fungua hizo kamba shingoni mwa Mkristo ukamfunge nazo huyu mahali pake, kwani naona kwa kuungama kwake mwenyewe, huyu ndiye mwuaji.

Mnyongaji akafanya kama alivyoambiwa, lakini wakati alipokuwa akikaza kamba, mara akasımamishwa na sauti ya mganga wa Kiyahudi akimsihi sana asubiri maana alikuwa na maneno ya lazima sana kutaka kusema. Hata alipoingia ndani kupita lile kundi la watu waliozunguka kutazama akamwendea mkuu wa askari. Akanena, "Ewe bwana mtukufu, Mwislamu huyu utakaye kumnyonga hastahili kufa, maana mimi ndiye mhalifu. Usiku uliopita mtu na mkewe ambao nilikuwa siwajui walikuja kunibishia mlango wangu, wakiniletea mgonjwa nipate kumwagua. Mtumishi wangu akaondoka kwenda kufungua mlango, lakini kwa vile hakuwa na taa mkononi hakuweza kuwatambua sura zao, ingawa walikubali niamshwe na wakatoa fungu la ujira wa kazi yangu wakampa. Basi wakati mtumishi wangu alipokuwa akinieleza habari hiyo wale watu wakamchukua mgonjwa wao mpaka kwenye ngazi ya juu ghorofani na kumwacha hapo. Hata nilipokwisha kuelezwa habari hiyo nikafanya haraka kutoka bila kungojea taa na kwa ajili ya ile giza nikakikwaa kitu ambacho kilibingiria ngazıni hakikusimama mpaka kilipofika chini. Niliposhuka kwenda kutazama nikaona mtu, nilipomwangalia sana nikamwona amekufa, na huyo maiti alikuwa ni mbilikimo. Ama mimi na mke wangu tuliogopa sana, mradi tukamchukua maiti mpaka juu ya paa la nyumba yetu tukaenda kumteremshia ndani ya bomba la moshi katika nyumba ya jirani yetu, mtoaji chakula wa sultani. Na yeye kule kumwona mtu chumbani mwake akamdhania ni mwivi mradi akamwingilia kumpiga mpaka akaanguka chini hana fahamu. Katika kuinama kwake kumtazama, akamwona amekufa fo! Sasa yule mtoaji chakula wa sultani akadhani kuwa kufa kwake kumetokana na kule kupigwa; lakini kwa hakika ilikuwa sivyo, yaani kama hivi unavyoona katika kueleza kwangu, lakini mimi ndiye mwuaji. Na ingawa sipendi kufanya maasi yo yote lakini sasa imebidi niteseke kwa maasi hayo, na hivi ni bora, kuliko kuwa na jukumu la kunyongwa watu wawili juu yangu. Kwa sababu hii, nakusihi umwondoe mtu huyu, na mimi niwe badili yake, kwani mimi ndiye mhalifu.”

Kule kusikia maneno ya mganga wa Kiyahudi, mkuu wa askari akaamuru achukuliwe akanyongwe, na yule mtoaji chakula wa sultani aachiliwe huru. Sasa kamba ikafungwa shingoni mwa mganga wa Kiyahudi, hata miguu yake ilipoanza kunyanyuka kutoka chini, mara watu wakasikia sauti ya mshoni ikimsihi sana mnyongaji asubiri kwa dakika moja, ili apate kusikiliza aliyonayo kusema.

Ndipo akamgeukia mkuu wa askari, akanena, “Ah! bwana wangu, ulikuwa karibu kutaka kuwaua watu watatu wasio na hatia, lakini kama utakuwa na subira kusikiliza kisa changu, utajua ni nani aliye mhalifu kweli. Anayehusika kuteswa hasa ni mimi! Kwani jana magharibi ilipokuwa ikiingia nilikuwa dukani pangu nikifanya kazi kwa bidii, mara akatokea mbilikimo mwenye kinundu ambaye alikuwa kama aliyelewa, akaja akakaa mlangoni. Akaniimbia nyimbo kadha wa kadha na mwisho wake nikamwalika kufika nyumbani kwangu, naye akakubali, ndipo tukaondoka kwenda nyumbani sote pamoja. Tulipokuwa tukila chakula nikampa kipande cha samaki, lakini mara mwiba ukamkwama kooni na Japokuwa tulifanya yote tuwezayo kumsaidia, lakini muda wa dakika chache akafa. Tukasikitika sana kwa kufa kwake, na kwa ajili ya kule kuogopa tusije tukakamatwa kuwa sisi ndio tuliomwua, tukamchukua maiti mpaka nyumbani kwa mganga wa Kiyahudl. Nikabisha, tena nikamtaka na mtumishi wake amsihi bwana wake Ushuka upesi aje kumwangalia mtu mgonjwa tuliyempelekea kumwagua, na katika kule kumhimiza kwangu ili ashuke upesi nikatoa fedha nikampa mtumishi, ili ziwe fungu la mganga. Yule mtumishi alipoondoka kwenda kumpasha habari bwana wake huku nyuma mimi na mke wangu tukamchukua yule maiti mpaka Juu ya ngazi ya ghorofani, tukamwacha hapo, kisha mimi na mke wangu tukafanya haraka kurudi kwetu. Katika kule kushuka ngazi kwake yule mganga, kwa ajali akamkwaa yule mtu, na kwa kumwona amekufa yeye mwenyewe akaamini kuwa ndiye aliyemwua. Lakini maadam sasa umejua kweli nakusihi umfungue, na mimi nife badili yake.”

Mkuu wa askari na ile kundi la watu watazamaji wakastaajabu mno kwa mambo haya ya ajabu yaliyotokea juu ya kifo cha mbilikimo mwenye kinundu.

Mkuu wa askari akamwambia mnyongaji, Mfungue mganga wa Kiyahudi, ukamfunge mshonı badili yake, kwa kuungama alikoungama mwenyewe juu ya uhalifu wake. Ama kwa hakika hiki ni kisa cha ajabu sana kinachostahili kuandikwa kwa herufi za dhahabu. Basi yule mnyongaji akafanya haraka kufungua mafundo yaliyomfunga mganga wa Kiyahudi, na kuzipitisha zile kamba shingoni mwa mshoni. Ikawa sasa yule sultani aliyepotelewa na mchekeshaji wake, kuwauliza majemadari wake mambo yaliyompata mchekeshaji wake. Wakajibu, “Seyid yetu, huyo mwenye kinundu alilewa sana kupita kiasi, kisha alitoka humu na kuonekana akizungukazunguka mjini, hata leo asubuhi ameonekana amekufa. Na huyo mtu aliyemwua alikamatwa na kufungwa gerezani mpaka mahali pa kunyongea palipokwisha kujengwa. Hata katika dakika hiyo ya kuuwa mhalifu alipofika, mara akatokea mtu mmoja, na mwingine tena na kila mmoja akidai kuwa yeye ndiye mwuaji, na hivyo iliendelea kwa kitambo, na hivi sasa mkuu wa askari yumo katika kumhoji mtu aliyejinadi kuwa yeye pekee ndiye mwuaji wa kweli. “

Sultani wa Kashga aliposikia maneno haya mara akamwamuru mtumishi wake kwenda kwa mkuu wa askari akawalete watu wote waliohusika na kifo cha mwenye kinundu pamoja na maiti mwenyewe. Mtumishi akaenda haraka kwa ujumbe huu, naye alifika kwa wakati hasa, kwani yule mshoni alikuwa kishaanza kuning’inia hewani, mara sauti yake ikasikilizana katika kundi la watu liilokuwa limenyamaza kimya, ikimwamuru mnyongaji kukata kamba. Yule mnyongaji alimtambua yule mtumishi aliye tumwa kuwa ni mmoja wa wajumbe wa sultani na mara akaikata kamba, basi yule mjumbe kuona kuwa yule mtu angali hai, akamtafuta mkuu wa askari kumpa ujumbe wa sultani. Na pale pale mkuu wa askari akatoka kwenda kwenye jumba la sultani pamoja na yule mshoni na mganga wa Kiyahudi, na mtoaji chakula wa sultani, na mfanyi biashara ambao walimchukua mwenye kinundu aliyekufa mabegani mwao.

Hata walipofika kwenye jumba la sultani, mkuu wa askari akajitupa chini kifudifudi miguuni pa sultani naye akamhadithia yote aliyoyajua. Sultani akastaajabu sana kwa habari hizi hata akamwamuru mwandikaji wake wa visa na hadithi aandike sawa sawa habari zile zilizopita, ili kwamba katika miaka hiyo ijayo kule kuokoka kwa ajabu kwa wale watu wanne waliojidhania kuwa wauaji, kusisahauliwe. Kisha sultani akamwuliza kila mmoja aliyehusika na kisa hiki cha mwenye kinundu, amweleze habari zake.
 
KISA CHA NDUGUYE KINYOZI WA TANO​



MIMI ni Kinyozi na nina ndugu sita. Hiki ni kisa cha ndugu yangu wa tano, Alnacha. Katika siku alizokuwa hai baba yetu, Alnacha alikuwa mvivu sana, hata kule kufanya kazi ya kujipatia chakula chake mwenyewe kulimshinda ikawa kila jioni kuomba, na vile alivyokuwa akipewa alikuwa akiviweka ili ale siku ya pili yake. Hata baba yetu alipokufa kwa uzee, aliacha reale mia saba, tukagawana, na kila mtoto alıpata mia mia. Alnacha, ambaye katika maisha yake yote hakupata kuwa na fedha nyingi kama zile, akawa anahangaika nazo asijue la kuzifanya. Mwishowe akaona ni afadhali anunue vioo, na chupa, na vitu vinginevyo vya namna kama hiyo.

Alipokwisha kununua vitu vyake akatoka kwenda kutafuta duka dogo lililo zuri, akakaa kitako mbele ya mlango wa duka lake ila vyombo vyake ameviweka ndani ya kapu wazi mbele yake akingojea wanunuzi wanaopita njia.

Basi akakaa katika hali hiyo huku amelikodolea macho lile kapu, lakini mawazo yake yalikuwa mbali kabisa. Na bila ya kufahamu mwenyewe akaanza kusema kwa sauti kuu, hata yule mshoni aliyekuwa na duka mlango wa pili wa duka lake, alimsikia waziwazi aliyokuwa akisema. Alinacha alisema hivi: Kapu hili limenigharimu reale 100, na hizo ndizo zote nilizokuwa nazo. Na maadam sasa nauza rejareja hivi vilivyomo kapuni huenda nikapata reale 200, na katika hizi mia mbili nitanunua tena vioo ambavyo vitanizalia reale 400, na kwa njia hii muda wa siku chache nitakuwa na reale 4000 ambazo zitajiongeza zenyewe mara mbili kwa urahisi. Hata hapo nitakapopata reale 10,000 (elfu Kumi), nitaacha biashara ya vioo niwe mwuzaji wa jonari, na wakati wangu wote utakuwa katika biashara za lulu na almasi na mawe mengineyo ya thamani. Mwisho, kama nikishatosheka na utajiri wangu, nitanunua nyumba nzuri sana ya shamba, kisha ninunue na farasi wengi halafu nitaishi Maisha ya raha na kuwakaribisha rafiki zangu katika karamu zangu zote nitawaita wapigaji vinanda na pia wachezaji kutoka miji ya karibu, ili waje kuwafurahisha Rafiki zangu. Walakini sitaitupa kazi ya biashara mpaka nipate mali nyingi kama reale laki moja za fedha, na hapo niwapo mtu wa kuheshimiwa sana nitamposa binti ya waziri mkuu nitamwambia babaake kuwa nimesikia habari zinazopendeza juu ya sifa za uzuri na akili ya binti yake. Na kwa hivyo siku ya harusi yetu nitakuwa tayari kulipa reale elfu za dhahabu na kama waziri akiyakataa haya ninayokusudia (lakini naona haitakua vigumu) nitamshika ndevu zake nimvute mpaka nyumbani kwangu.

Lakini hapo nitakapooa, nitamwekea binti yake matoashi kumi walio mahodari kumtumikia. Halafu nitavaa joho langu zuri lenye katarizwa uzi wa zari nyekundu, nipande farasi wangu mwenye tandiko la dhahabu safi na kanda za hatamu yake ziking’aa kwa lulu na almasi huku nikifuatwa na kikosi cha watumishi. Nitakwenda mwenyewe kwenye jumba la waziri mkuu, na wakati nikipita watu wanainamisha macho tena wanisujudie. Hata nikifika kwenye ngazi ya jumba la waziri mkuu nitashuka juu ya farasi, na watumishi wangu watashuka kwa safu upande wa kulia na wa kushoto, nami nitapanda ngazi za jumba lake na mwisho wake nitamkuta waziri mkuu ananingojea kunipokea. Hapo atanikumbatia kwa kuwa ni mkwewe, tena atanipa na kiti chake na yeye mwenyewe atajiweka chini yangu. Haya yakishafanyika watumishi wangu wawili wataingia ndani, hata kila mmoja amechukua kifuko cha reale eflu za dhahabu. Kimoja nitampa yeye nimwambie ‘Hizi hapa reale elfu za mahari ya binti yako, na hizi,’hali naendelea katika kusema na huku nimeshika kifuko cha pili.’Reale elfu zingine za kukuonyesha kuwa mimi ni mtu mwenye utu.’ Baada ya yeye kuuona ukarimu kama ule, hata hiyo dunia haitanena neno jingine.
 
Baadae nitarudi kwangu kwa fahari ile ile niliyokwenda nayo, na mke wangu atamleta jemedari wa kunisindikiza kwa vile nilivyo kwenda kumtembelea baba ake, na huyo jemedari nitamvika heshima kwa kumpa vao la mali na zawadi nzuri. Lakini kama yeye akiniletea zawadi, hata moja, nitaikataa nimfukuze aliyeileta.

Tena sitamwachilia mke wangu kutoka chumbani mwake kwa udhuru wowote bila ya ruhusa yangu.

Hakuna neno litakalokuwa thabiti kama langu na siku zote nitatahadhari katika kuvaa mavazi: kwa kadiri inavyostahili cheo changu. Usiku tunapoingia vyumbani mwetu nitakaa mahali pa heshima, na sura zangu zitakuwa za haiba, tena nitakuwa nikitazama mbele yangu sawasawa, na mke wangu aliye mzuri kama mwezi arobataashara, anaposimama kwa unyenyekevu mbele ya kiti changu nitajifanya kama simwoni. Halafu watumishi wake wataniambia: ‘Ewe, Bwana wa mabwana, mkeo aliye mjakazi wako amesimama mbele yako kungojea umwangalie. Kweli twajua kwamba amekutia uchungu sana hata hutaki kumwangalia, lakini mhurumie kwani amechoka kwa kusimama sana. Na hivi twakusihi, umwambie akae.’ Ama kwa kweli sitaonyesha hata dalili ya kusikiliza maneno yao, na kwa hivyo wataona haya sana. Basi kisha watajitupa chini ya miguu yangu kwa vilio na mwisho wake nitainua kichwa changu nimtupie jicho la kejeli halafu nirudie hali yangu ile ile ya kwanza. Watumishi wake watadhani kuwa labda sikupendezewa na nguo za mke wangu na kwa hivyo watamwondoa kwenda kumvisha nguo nzuri zaidi, na mimi kwa upande wangu nitaondoka kwenda kubadili zile nilizovaa nivae zingine zilizo nzuri zaidi. Basi wakiisha kumvisha nguo zake watarudi tena, lakini safari hii itachukua kitambo sana kabla hawajaweza kunifanya nimwangalie mke wangu.

Lakini mambo haya yote ni heri yaanze siku ile ile ya harusi yangu, maana nakusudia kuendelea na mengi zaidi katika hizo siku za mbele za maisha yetu.

Siku ya pili yake atamshtakia mamake kwa haya aliyotendewa na mashtaka hayo yatafanya moyo wangu kujaa furaha. Mamaake atakuja kunitafuta, na akiniona, ataniamkia kwa kunibusu mikono yangu kwa heshima tupu, aseme: ‘Bwana wangu (maana hatothubutu kujitia katika hatari ya kuniudhi kwa kuniita mkwe’ Kama tunajuana sana) nakusihi usikatae kumwangalia au kumkaribia binti yangu, kwani haja yake ni kukupendeza tu na anakupenda kwa moyo wake wote.’

Lakini sitayasikiliza maneno ya mkwe wangu kama vile nilivyoyasikiliza maneno ya wale watumishi. Atanisihi tena nimsikilize maombi yake, na wakati huo atajitupa chini ya miguu yangu lakini yote ni bure. Halafu atatwaa bilauri aitie mvinyo ampe binti yake akimwambia: ‘Twaa umpelekee mwenyewe mmeo hawezi kuwa mkatili hivyo hata akatae kupokea kila anachopewa.’ Basi mke wangu ataipokea bilauri anipe kwa kutetemeka na machozi yakimchiririka machoni; lakini mimi sitamwangalia kamwe, ila nitageuka niangalie kando upande mwingine. Hivi itamfanya alie zaidi na hali ile bilauri kaishika mkononi mwake, aseme: ‘Mume wangu nikupendae sana, sitaacha kukusihi mpaka unifanyie jamala upokee unywe.’ Lakini maneno hayo yatanigadhibisha. Ndipo hapo nitakapompiga jicho la hasira nimvurumishie ngumi ya shavu na teke la nguvu, hata apepesuke kutoka chumbani akaangukie kitanda kidogo cha ukumbini.’

Ama kwa hakika, ndugu yangu alishughulika sana kwa mawazo yake, hata akatupa teke kweli na kupiga lile kapu lake la vioo.
 
Yule jirani yake mshoni, aliyekuwa akimsikiliza maneno yake alipoona vile, akaangua kicheko akacheka sana.



Akamwambia, 'E, baa wee! Hata haya huna unamtenda hivyo mkeo naye hakukosa kitu? Bila ya shaka wewe mtu mbaya kwani hata machozi yake na maombi yake hayakukutia huruma. Na laiti kama mimi ningekuwa waziri mkuu, ningeamrisha upigwe mijeledi mia, kisha utembezwe mjini huku mpigaji mbiu, akikunadishia uovu wako.’

Sasa ile hasara ya uchumi wake wote, ikamtia akili ndugu yangu akaona kuwa hasara ile yote imetokea kwa ajili ya majisifu yake yasiyo maana, ikawa kurarua nguo zake na kung’oa nywele zake huku akilia kwa uchungu mno, hata wale watu wapitao njia walisimama kumsikiliza. Kwani siku hiyo ilikuwa Ijumaa, na watu wanaopita njia walikuwa wengi mno zaidi ya siku zote. Wengine walimsikitikia Alnacha, lakini wengine walimcheka tu, na yale majivuno yake yote aliyokuwa nayo yalimtoka pamoja na kapu lake la vioo, akawa analia kwa upumbavu wake. Hata akatokea bibi mmoja alayepanda nyumbu, ambaye kwa dalili alionyesha maarufu akasimama kuuliza sababu ya yule mtu kulia. Watu wakamwambia kuwa ni mtu masikini aliyetoa mali yake yote aliyokuwa nayo na kununua hili kapu la vioo, ambavyo sasa vimevunjika. Yule alipokwisha kuelezwa sababu ya kilio kile, akamgeukia mtumishi wake akamwambia: ‘Mpe cho chote ulicho nacho.’ Mara mtumishi akatoa kifuko cha reale mia tano za dhahabu, akampa ndugu yangu. Alnacha alizipokea kwa furaha kubwa, na kumshukuru yule bibi mara elfu, kisha akafunga duka lake ambalo hakuwa na haja nalo tena akarudi kwake. Lakini juu ya hivyo nafsi yake hata sasa ilikuwa na wasiwasi na haikutulia. Basi alipokuwa katika hali hiyo mara akasikia mtu akibisha mlangoni kwake, hata alipokwenda kufungua kutazama akamwona mwanamke mzee amesimama nje.

Yule mwanamke akamwita Alnacha akisema, ‘Mwanangu, nataka unifanyie hisani, kwani sasa ni wakati wa kusali nami bado sijatawadha. Basi tafadhali nakuomba unikaribishe nyumbani mwako, unipatie na maji nitawadhe.’ Yule ndugu yangu asikatae kumfanyia alivyotaka bikikongwe ijapokuwa alikuwa mgeni naye. Akatwaa birika la maji akampa halafu yeye akarudia kikao chake, kwa mawazo yake yale yale, ya kufikiri hali yake mbaya. Ndipo alipotwaa zile reale zake za dhahabu akazitia ndani ya mshipi mrefu mwembamba wa kitambaa na kuufunga kiunoni mwake. Wakati huu wote yule bi-kikongwe alikuwa akishughulika kwa sala zake, hata alipokwisha kusali akaenda mbele ya ndugu yangu akajitupa kifudifudi mara mbili, kisha akainuka na kumshika kichwa chake akimwombea dua za baraka zisizo kiasi. Lakini ndugu yangu alipomwona amevaa matambara akaona kuwa zile dua zake alizomwombea zilikuwa za maneno matupu, basi akaona afadhali ampe fedha kidogo ili aende akajinunulie nguo mpya, ndipo akatoa reale mbili za dhahabu akampa. Yule bi-kikongwe kastuka kwa mastaajabu, akaona kama aliyetukanwa, akanena, ‘Lo! Hivi ndiyo nini? Hivyo kumbe wewe bwana wangu, wanifananisha mimi na wale masikini wanaokwenda majumbani kuomba sadaka? Chukua fedha zako, nami nakuambia ahsante kwani sina haja nazo: maana mimi ni mtumishi wa bibi mzuri aliye tajiri sana, naye hunipa kila kitu nitakacho.’

Ndugu yangu hakuwa mwerevu sana wa kutambua: kuwa yule bi-kikongwe alikataa zile reale mbili alizompa kusudi apate zaidi, lakini yeye akawa ni kumwulizauliza kama ataweza kumfanyia hisani apate kumwona bibi huyo. Bi-kikongwe akajibu, ‘Tayari, na hasa yeye atafurahi umwoe, na uwe bwana wa mali yake yote. Haya basi chukua fedha zako unifuate.’

Furaha ikamjaa moyoni kwa kupata bahati mbili kwa mara moja, ya mali na ya mke mzuri, basi ndugu yangu hakuuliza tena ila akajifunga ule mshipi wake kiunoni, wenye reale mia tano za dhahabu alizopewa na yule bibi. Akatoka kwa furaha na kufuatana na yule bi-kikongwe.

Wakaenda kwa kitambo kidogo mpaka yule bi-kikongwe akafika na kusimama mbele ya mlango wa nyumba kubwa, na kubisha. Akatokea mtumishi wa Kiyunani kuja kufungua mlango, na yule bi-kikongwe akampitisha ndugu yangu katika uwanja ulio sakafiwa vema, mpaka ndani ya ukumbi uliopambwa vizuri. Sasa yule bi-kikongwe akamwacha hapo na yeye akaenda chumbani, kumwambia bibi yake kuwa ukumbini kuna mgeni, na kwa kuwa mchana ule ulikuwa na joto sana ndugu yangu akajipweteka kwenye kiti chenye mito, na kuvua kilemba chake kizito. Punde kidogo huyo bibi akatokea, na ndugu yangu katika kumtupia jicho kwa mara ya kwanza akamwona ni mzuri mno, tena amevalia mavazi ya kitajiri na kupendeza zaidi ya hivyo alivyotarajia kumwona. Basi akainuka katika kiti chake kumsalimu lakini yule bibi alimfanyia ishara akae astarehe, na yeye mwenyewe akakaa kando karibu yake. Baada ya ada ya kuulizana habari ilipokwisha, bibi akamwambia, ‘Twende chumba kingine, maana hapa hatukustarehe,’ basi wakaondoka kwenda chumba kidogo, ikawa yule bibi kuzungumza naye kwa kitambo. Halafu kwa ghafa yule bibi akaondoka na kumwambia, 'Ningojee hapa usiondoke, nitarudi sasa hivi.’

Basi akangoja kama alivyoambiwa, lakini badala ya kurudi yule bibi likaingia baba moja kubwa mno, lenye upanga wazi mkononi. Likamkaribia ndugu yangu kwa uso wa ghadhabu na kumwuliza, ‘Shughuli gani uliyo nayo hapa?’ Ama sauti yake na mambo yake yalikuwa ya kutisha mno hata ndugu yangu Alnacha hakuwa na nguvu za kujibu ila alijiachia tu akanyang’anywa dhahabu zake, na kutiwa majeraha kwa upanga bila kujitetea. Hata alipoachiliwa kwenda zake akawa hana nguvu za kuondoka akaanguka chini, na ingawa alikuwa na fahamu zake lakini alijiona amekufa. Lile baba kubwa likamwagiza mtumishi wa Kiyunani kwenda kuleta chumvi; ikawa wanamsugulia nayo katika majeraha yake na kwa hivyo aliona uchungu na maumivu sana, na ingawa alikuwa mzima akipumua, lakini hakuonekana na dalili ya kupona. Bası halafu wale watu walipotoka na kumwacha, akaja bi-kikongwe mmoja akamkokota mpaka kwenye mlango wa handaki, akamtupa ndani ya hilo handaki lililojaa watu waliouawa.

Bası kwa kule kuanguka kwake vibaya akazimia, lakini kwa bahati ile chumvi aliyosuguliwa nayo katika majeraha ndiyo ilikuwa heri yake kwa kumponesha maisha yake, sasa akawa anaanza kidogo kidogo kupata nguvu zake tena. Hata siku moja usiku, baada ya kupita siku mbili, akaweza kuinua ule mlango wa handaki akatoka; akaenda kujificha uani mpaka kulipopambazuka, ndipo alipomwona yule bi-kikongwe akitoka mle ndani ya nyumba kwenda kutafuta mawindo yake. Kwa bahati yule bi-kikongwe hakumwona ndugu yangu, na alipokuwa amekwenda zake wala haonekani tena Alnacha akatoka katika jumba hilo la wachinjaji akakimbilia nyumbani kwangu.

Nikamfunga dawa majeraha yake na kumwuguza vizuri baada ya mwezi kupita akawa mzima kama zamani. Wazo alilokuwa nalo ni kutafuta njia ya kufanya ili apate kujilipiza kisasi chake kwa kile kikongwe kiovu, na kwa nia hiyo alitwaa mfuko unaotosha kuingia reale mia tano za dhahabu, akaujaza vigae vya chupa. Akaupachika kwapani na kujitunga mshipi wake, kisha akajigeuza kama mwanamke mkongwe, na akatwaa jambia lake akalifunika nguoni.

Hata siku moja asubuhi alipokuwa akienda kwa kuinamainama na kuchechemea njiani, mara akamkuta yule adui yake wa zamani yumo katika kuzungukazunguka kuangalia kama anaweza kumpata mtu ye yote wa kumhadaa. Akamwendea, na akaiga sauti ya kike, na kumwuliza, ‘Je, huko kwako unazo mizani mbili unazoweza kuniazima? Nimefika sasa kutoka Ajemi, nami nimechukua reale mia tano za dhahabu ambazo nataka kuzipima, ili nione kama dhahabu yake ina uzani kamili.’

Kizee kile kibalaa kikajibu, ‘Ewe, mwanamke mwema! Umejua hasa mtu wa kumwuliza. Mwanangu ni mbadilishaji wa fedha, na kama utaniandama nitamwambia akupimie. Lakini imetupasa twende upesi maana kama tukikawia ataondoka aende dukani kwake.’ Kuisha kusema hivyo akaongoza njia mpaka nyumba ile ile ya zamani, na kitumishi kile kile cha Kiyunani kikatokea kufungua mlango.

Basi ndugu yangu akaachwa tena pale pale ukumbini, na mara huyo mtoto mbadilishaji wa fedlha akatokea kwa umbo la baba kubwa linalotisha. Hata alipomkaribia ndugu yangu, akamwambia, 'Ee kizee masikini, nyanyuka unifuate,’ na yeye mwenyewe akageuka kuongoza njia ya kwendea mahali pa kuuwa. Alnacha akaondoka kumfuata, lakini katika kule kumfuata kwake akachomoa jambia lake kiunoni akalipiga lile baba dharuba moja ya shingo akamdengua kichwa. Sasa ikawa yule ndugu yangu kuokota kile kichwa kwa mkono mmoja, na ule wa pili ukashika ule mwili kuukokotea kule kwenye handaki akautumbukiza pamoja na kile kichwa. Kile kitumishi cha Kiyunani kikawa kinakuja na bakuli lake la chumvi kikidhania kuwa yote yamefanyika kama desturi, lakini kilipomwona Alnacha ameshika jambia wazi mkononi kikatupa bakuli kukimbia. Lakini ndugu yangu alikuwa mwepesi na mara kile kichwa chake yule mtumshi kikakatwa nacho. Basi huo ukelele uliopigwa na kile kitumishi ulimfanya yule bi-kikongwe kuja upesi kuangalia lililokuwa, na kabla hajapata nafasi kukimbia, Alnacha akamkamata. Akamwambia, ‘Ewe, baa! Wanijua mimi?’

Akajibu kwa kutetemeka mwili mzima, 'Seyid yangu, wewe ni nani? Maana mimi sikupata kukuona.’

Akamjibu, 'Mimi ndiye yule uliyesali nyumbani kwake sala zako za hila. Sasa umesahau?’ Kusikia hivi yule bibi akajitupa chini kumshika miguu na kumsihi amhurumie, lakini wapi! Alnacha alimpiga dharuba moja ya upanga akamkata vipande vinne.

Sasa mle ndani ya nyumba kukawa kumebakia yule bibi mmoja, ambaye alikuwa hajui kabisa yanayopita mle ndani wakati ule. Ikawa ndugu yangu kumtafuta nyumba nzima na mwisho wake akamwona; naye alikuwa karibu kuzimia kwa hofu kwa kumwona ndugu yangu. Na huyu vile vile akasihi sana asiuawe, na kwa huruma zake Alnacha hakumwua, ila alimtaka amwambie jinsi alivyopata kuingia katika ushirika pamoja na watu wale wabaya aliowaua saa zile.

Akajibu, 'Zamani, nilikuwa mke wa mfanyaji biashara mwaminifu, na yule bi-kikongwe, ambaye uovu wake sikuujua, alizoea kuja kunitembelea. Hata siku moja akaniambia, ‘Bibi, leo nyumbani kwetu kuna harusi kubwa. Na kama utatufanyia heshima ya kuja, nina yakini kuwa utafurahi nafsi yako.’ Basi hapo ndipo nilipo ghilibiwa, nikavalia nguo zangu za mali na kuchukua kifuko cha reale mia za dhahabu, nikatoka nikaenda. Mara kule kuingia tu lile baba linalotisha likanitia mikononi.’

Ndugu yangu akasema, ‘Basi yule ayari bila shaka amepata mali nyingi.’

Yule bibi akajibu, 'Oh, nyingi kabisa! Na kama ukiweza kuzichukua zote zitakutia utajiri wa milele. Hebu njoo tuziangalie.’

Basi akamchukua Alnacha na kumpeleka ndani ya chumba Kimoja kilichojaa makasha yaliyojazwa dhahabu ambayo alitazama kwa mastaajabu. Bibi akamwambia, ‘Nenda ukalete watu waje wayachukue.’

Ndugu yangu alipoambiwa hivyo hakungoja tena, alikwenda barabarani kutafuta watu, na mara akapata watu kumi akaenda hao kule kwenye nyumba. Lakini alipofika akastaajabu sana kuona mlango wazi na kile chumba kilichokuwa na makasha ya dhahabu kitupu. Yule bibi alikuwa mwerevu zaidi kuliko yeye, na kwa nafasi ile ndogo aliyoipata akafanya chap-chapu kama alivyoweza, kuyahamisha makasha ya dhahabu. Lakini, na ndugu yangu naye alijaribu kujifariji kwa kuchukua vyombo vyote vilivyo vizuri, ambavyo kwa hakika havikuzidi thamani ya zile reale zake mia tano alizonyang'anywa.

Ah! Masikini Alnacha, alipotoka mle ndani ya nyumba alisahau kufunga mlango, na wale majirani kuona ile nyumba i wazi kisha ni tupu, wakawaambia askari, na siku ya pili yake walimkamata Alnacha kuwa ni mwivi. Ndugu yangu akajaribu kuwapa rushwa ili wamwachilie, lakini badala ya kumwachilia wakamfunga mikono nyuma, na kumlazimisha kwenda nao mpaka kwa kadhi. Kadhi alipokwisha kuelezwa sababu ya mashtaka yake, akamwuliza Alnacha wapi alikopata vyombo vile vyote alivyovipeleka nyumbani kwake jana. Alnacha akajibu, ‘Seyid yangu, mimi ni tayari kukuambia habari zote, ila nakuomba unipe ahadi kuwa sitaadhibiwa.’

Kadhi akasema, ‘Haya, nakuahidi.’

Basi ndugu yangu akaanza kueleza tangu mwanzo wa masaibu yake yote yaliyompata, na jinsi alivyojilipiza kisasi kwa wale waliomtesa. Na kwa habari ya vile vyombo, akamsihi kadhi amwachilie angalau sehemu, kusudi afidie zile reale zake mia tano alizonyang'anywa.

Lakini yule kadhi hakusema neno juu ya hayo, wala hakukawia kupeleka watu nyumbani kwa Alnacha, kwenda kuchukua vyombo vyote alivyovichukua kule kwenye ile nyumba. Basi kila kitu kilipokwisha chukuliwa na kuwekwa nyumbani kwa kadhi, ndipo kadhi akamwamuru ndugu yangu ahame mji, wala asirudi tena; maana aliogopa kuwa kama ndugu yangu atarudi, huenda pengine akaenda kwa Khalifa kushtaki. Mradi Alnacha akafuata hukumu, na alipokuwa njiani akiendea mji uliokaribiana na ule anaotoka, kwa ghafla akaangukiwa na kikosi cha wanyang’anyi wakamvua nguo zake na kumwacha utupu pale pale kando ya njia. Basi niliposikia hali alivyo, nikamkimbilia kwenda kumfariji.

Nilimpa kanzu yangu iliyo nzuri kuvaa. Hata usiku ulipoingia, nikamchukua na kurudi naye mpaka nyumbani kwangu, na tangu siku hiyo hata sasa yupo nyumbani kwangu, namtazama kama ndugu zangu wengine.
 
KISA CHA NDUGUYE KINYOZI WA SITA​



SASA imebaki kukuhadithia kisa cha ndugu yangu wa sita, jina lake Shakabak. Naye huyo alirithi kwa baba yetu vile vile kama sisi reale elfu za fedha ambazo aliziona nyingi mno, lakini kwa bahati mbaya zote zilimpotea na akawa masikini mwombaji. Lakini alivyokuwa na adabu na maneno matamu kazi yake hii mpya ilimfaa sana, hata akawa hana kazi ingine ila kufanya urafiki na watumishi wa nyumba kubwa kubwa kusudi apate kukaribiana na bwana zao.

Siku moja alipokuwa akipita njiani akaona jumba zuri mno lenye kundi la watumishi wanaozungukazunguka uani. Akawaza kuwa lile jumba pengine huenda likamzalia mavuno ya mali, mradi akaingia uani kuuliza ni jumba la nani.

Mtumishi mmoja akamjibu, 'Mwenzetu, watokea wapi? Wewe mwenyewe huoni kuwa jumba hili haliwezi kuwa la mtu mwingine ila Bamaside?’ hao Mabamaside walitukuka sana kwa wema wao na ukarimu wao. Ndugu yangu aliposikia hivi, akawauliza wale watumishi kama watampa sadaka. Watumishi hawakukataa, ila wakamwambia kwa heshima aingie ndani akaombe kwa bwana mwenyewe.

Ndugu yangu akawashukuru sana kwa heshima waliyomfanyia na kisha akaingia ndani ya jumba ambalo lilikuwa kubwa mno, hata lilimchukua kitambo kufika vyumbani kwa Bamaside. Mwisho katika chumba kilichotiwa rangi vizuri akamwona mzee mwenye ndevu ndefu nyeupe zilizomshuka mpaka kifuani, amekaa juu ya kitanda, naye alimkaribisha kwa wema hata ndugu yangu katoa hofu ya kusema haja yake. Akasema, ‘Bwana wangu, nisaidie mimi masikini ninayeponea sadaka ninazopewa na watu matajiri kama wewe.’

Kabla hajaendelea kusema zaidi Bamaside, akanena, ‘Hupatikanaje mtu kufa kwa njaa wakati huu nilio hapa Bagbdad? Ama hayo ndiyo mambo yanayofaa kukomeshwa kabisa! Isije ikasemwa kuwa mimi nimekutupa, nami nina yakini kuwa nawe kwa upande wako hutanitupa.’

Ndugu yangu akajibu, ‘Bwana wangu, nakuapia kutwa sijala kitu.’

Bamaside akastajabu, akanena, ‘Nini! Unakufa kwa njaa?’ mara akasema, ‘Mtumishi lete maji tunawe mikono kabla hatujakula nyama.’ Hapana mtumishi aliyetokea, lakini ndugu yangu akamwona Bamaside akisugua mikono yake tu kama mtu aliyekuwa akinyunyuziwa maji.

Kisha Bamaside akamwambia ndugu yangu, Mbona hunawi mikono yako na wewe?’ Yule Shakabak akadhani kuwa Bamaside anamfanyia mzaha (ingawa yeye hakuona kitu), mradi akajaongea kariba na kuiga vile vile alivyokuwa akifanya Bamaside.

Bamaside alipokwisha kunawa mikono yake, akainua sauti akinena,'Tuletee chakula upesi kwani tuna njaa sana!' Hapana chakula kilicholetwa, lakini Bamaside akajifanya kama anayemega chakula sahanini akitia mdomoni mwake, na huku akisema, 'Kula rafiki yangu, kula. Tafadhali kula usione haya, kula kama uliye nyumbani kwako. Maana najua kuwa mtu mwenye njaa hali sana.’

Shakabak akajibu, 'Niwie radhi bwana wangu, kisha naye akawa

anaiga vile vile kama kwanza.

Bamaside akamwuliza, ‘Wakionaje chakula hiki?’ Yule ndugu yangu ambaye hakuona nyama wala mikate, akajibu, Ah! bwana wangu, nakiona kizuri sana, wala sijapata kula chakula kitamu kama hiki.’

Bamaside akamwambia, ‘Basi kula sana kama upendavyo.’
 
Basi baada ya kuagizia kila namna ya vyakula (ambavyo havikutokea) kuwekwa mezani, na kusifu uzuri wa kila kimoja, yule Bamaside akasema kuwa amekula vizuri sana, na sasa wataendelea kunywa mvinyo wao. Ndugu yangu kwanza alikataa akasema kuwa iliharamishwa, lakini kwa vile Bamaside kumshikilia kunywa kwa kuwa haitapendeza kunywa pekee, akakubali kunywa kidogo. Ndipo yule Bamaside akajifanya kama anaejaza bilauri zao mara kwa mara, hata mwisho ndugu yangu akajifanya kama aliyelewa na kumpiga Bamaside ngumi ya utosini naye akaanguka chini. Naam, akainua tena mkono wake kutaka kumpiga mara ya pili ndipo Bamaside akampigia kelele akisema kuwa ana wazimu hivyo ndugu yangu akajituliza, na kumtaka radhi kwa aliyomtendea akisingizia ulevi aliokunywa. Basi kwa hivi Bamaside badala ya kukasirika sana, akaanza kucheka na kumkukumbatia kwa wema. Akasema, ‘Ama siku nyingi nilikuwa nikitafuta mtu wa namna yako wewe na leo nimempata, basi tangu sasa nyumba yangu ni yako, maana umenistahimilia na kuingia katika mchezo wangu na kujifanya kama ulaye na unywaye, hali hapana kitu. Basi sasa utatuzwa kwa chakula kizuri kweli. Halafu akapiga makofi na vyakula vyote walivyokuwa wakila kwa kuviwaza moyoni wakati ule wa karamu ya kwanza vikaletwa. Watumishi wakaja kuimba na kupiga vinanda vya kila namna. Na wakati huo wote Shakabak alikuwa akikirimiwa na Bamaside kama rafiki wa dhati na akavikwa mavazi mazuri mazuri.

Miaka ishirini ikapita, na ndugu yangu alikuwa vile vile akikaa na Bamaside kumtunzia nyumba yake, na kumsimamia mambo yake. Hata mwishowe mfadhili wake mkarimu akafa, na mali yake yote ikachukuliwa na sultani, hata vile vilivyokuwa haki ya ndugu yangu pia navyo vikachukuliwa. Na sasa akawa masikini kuliko hivyo alivyokuwa tangu kuzaliwa kwa hivyo akaazimia kubahatisha bahati yake pamoja na msafara wa wasafiri waliokuwa wakienda Makka. Lakini kwa bahati mbaya, ule msafara ulishambaliwa na kutekwa nyara na Mabedui, na wasafiri wakachukuliwa kifungoni. Ndugu yangu yeye akawa mtumwa wa mtu mmoja aliyekuwa akimpiga daima dawamu, akitumainia kuwa Shakabak atachoka na madhila na atataka kujikomboa, na hata japokuwa Shakabak alitaka hivyo, lakini ilikuwa kazi bure maana jamaa zake nao walikuwa masikini kama yeye mwenyewe. Mwisbo yule Bedui akachoka kusumbuliwa, ndipo akampandisha juu ya ngamia na kumpeleka katikati ya jangwa akamwacha kuko huko yeye na bahati yake. Msafara uliokuwa ukipita kwenda Baghdadi aliniaambia huko alikokuwa, nami nikafanya haraka kwenda kumuokoa na kumrudisha mjini, nikamkuta katika hali ya kusikitsha sana. Nikamchukua kukaa naye mimi.

MWISHO
 
Back
Top Bottom