Mbabe Gattuso apewa mikoba AC MILAN

Mbabe Gattuso apewa mikoba AC MILAN

Tangu jamaa aichukue AC milan sasa hivi inagonga mpira si mchezo.....

Nahisi safari hii wakikutana na juventus lazma wakae....

Naiona AC milan kurudisha makali yake ya nyuma...
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Tangu jamaa aichukue AC milan sasa hivi inagonga mpira si mchezo.....

Nahisi safari hii wakikutana na juventus lazma wakae....

Naiona AC milan kurudisha makali yake ya nyuma...
Kama uliangalia mechi yao ya jpili nahisi ushagunndua Gattuso kaamua timu yake yote ni roho mbaya tu
 
Mimi pia nilishangaa why huyu mtukutu kakabidhiwa timu kubwa kama ile....

Mwanzo alikuwa akisusua sua sana ila michezo ya hivi karibuni alizinduka kutoka usingizini alikuwa anatoa dozi kwelikweli na juzi alivyomfunga As Roma nilishangaa sana.....
Yaani timu inayokutana nayo inakua na kazi mbili kwanza kudili na Gattuso pili kuwa makini na wale masela wake uwanjaniii
 
Kama uliangalia mechi yao ya jpili nahisi ushagunndua Gattuso kaamua timu yake yote ni roho mbaya tu
A.S Roma alikuwa anakula goli nne ile mechi sema umakini ulikosekana kwa baadhi ya nafasi walizotengeneza. Leo tena wanaingia uwanjani kupigania nafasi mojawapo ya kucheza champions league msimu ujao. Ni mechi ya nusu fainali ya copa italy dhidi ya Lazio ikiwa ni mchezo wa marudiano.
 
Kiukweli siku hizi sichoki kuwafatilia mechi zao
 
fikiria leo Ac milan akutane na madrid halafu ronaldo awe uwanjani sijui gattuso atawaza nini
 
Kiukweli siku hizi sichoki kuwafatilia mechi zao
ila ana ratiba ngumu sana kwanzia atoke kwa Roma, leo anacheza mechi muhimu sana dhidi ya lazio anahitaji droo ya magoli au ushindi. Wikiendi ana mechi ya ligi dhidi ya inter milan. Baada ya hapo ana mechi dhidi ya arsenal katika europa league
 
Wanaume Juve anasubiri mshindi wa leo wakutane final...
 
Final copa Italy: Juventus vs Ac milan.
Ac milan wameingia fainali kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka sare 0-0 hadi dakika 120. Kalinic ndiye mchezaji aliyeupeleka mchezo huo hadi kwenye penati kutokana na kukosa nafasi ya wazi kabisa ya kuifanya Milan imalize mchezo. Pongezi tena kwa Gatuso kwa kuendeleza ushindi
 
Nampongeza sana huyu kamanda, yuko vizuri. But kwa Allegri watakuwa na wakati mgumu. Tusubiri kiongozi..

Usiku Mwema!
 
Back
Top Bottom