Mbadala wa kufanyiza waalimu mtihani kabla ya kuajiriwa

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Binafasi napendekeza badala ya kuwapa waalimu mitihani kabla ya kuajiriwa, kuwe tu na kigezo cha pass stahiki cha masomo atakayofundisha.....
Sijui kwa nini umchague mwalimu wa Kiswahili & History (kwa mfano) mwenye ufaulu wa D kwa masomo husika wakati umeacha kuchukua mtu mwenye ufaulu wa B halafu uanze tena kupoteza gharama eti unajustify uwezo wake?
Utaratibu huu Kisaiyansi utakuwa hauko sawa sawa....
 
Alama unazopata kwenye mtihani mmoja wa mwisho kuhitimu kozi haziwezi ku determine uwezo wako wa kumudu somo hilo. Maksi hushuka na upanda kadri unavyofanya mitihani. Frequency kamwe haziwezi kuwa zilezile hata ufanye mitihani mia maksi zitakuwa zinapanda au kushuka. Kinachotakiwa ni uwezo wa kulimudu somo unalofundisha. Niliingia kufundisha masomo ambayo nilifeli lakini nafundisha wanafunzi vema na nazidi ku gain momentum. Sasa kama ningesema nilifeli sitaweza kufundisha somo hilo ningepata wapi ujuzi na umahiri wa kulifundisha somo lililonitesa na kufeli huko nyuma? Hawa walimu wapya wafanye tu mitihani ya masomo wanayoenda kufundisha, chuoni wanafundishwa mbinu tu za kufundisha na huko kazini wanaenda kufundisha yale waliyojifunza shuleni kuanzia msingi mpaka sekondari.
 
Wale wanaoenda kufundisha msingi watapewa mambo ya mtaala wao na wale wa sekondari watapewa ya huko. Shida hakuna kama ulikuwa unafanya vizuri hakuna ugumu hapo. Changamoto itakuwepo kwenye masomo ya math/physics, kuna hisabati hapo, labda na english nayo itakuwa kizingimkuti
 
Kwani wametangaza kuanza kutoa mitihani kwa walimu ajira mpya??
 
habari zipo leo mpaka magazetini. We jiandae vema kufanya mtihani wa masomo utakayoenda kufundisha. Kama ni hisabati kajiande kuanzia chekechea mpaka la saba. Kama ni wa sekondari kasome masomo yako kuanzia form one mpaka four/six
 
Watanzania tuache ujanja ujanja wa masuala muhimu kwa Taifa na suala la ajira ni muhimu sana na halihitaji ujuaji mwingi kama wa mleta mada.

Duniani kote suala la mitihani kabla ya ajira linaangaliwa sana na sio huo ufaulu wa Darasani. Muajiri ni lazima atoe mitihani kwa muajiriwa Ili ajue skills and competencies za muajiriwa ,huo ufaulu wa darasani ni kipimo kimojawapo.

Nashangaa mleta mada anapokuja na hoja za kupinga jambo hilo na kutaka mfumo wa kupeana ajira utumike badala ya mfumo wa kushindanisha waombaji.
 
Kuna walimu wa msingi ni waoga kufundisha hisabati kuanzia la tano hadi saba, wanang'ang'ana na darasa la tatu na nne tu halafu wanababaisha wanafunzi wakifika la tano hawajui walichofundishwa huko chini, inabidi uanze upya kufundisha ya chini ndio ueleweke unayoyafundisha. Sekondari nako unakuta mwalimu anang'ang'ana na form one tu juu hapandi, wakati mwalimu unatakiwa utawale mada zote kuanzia chini hadi juu
 
Binafasi napendekeza badala ya kuwapa waalimu mitihani kabla ya kuajiriwa, kuwe tu na kigezo cha pass stahiki cha masomo atakayofundisha.....
Sijui kwa nini umchague mwalimu wa Kiswahili & History (kwa mfano) mwenye ufaulu wa D kwa masomo husika wakati umeacha kuchukua mtu mwenye ufaulu wa B halafu uanze tena kupoteza gharama eti unajustify uwezo wake?
Utaratibu huu Kisaiyansi utakuwa hauko sawa sawa....
Kapige interview mzee baba mambo yanabadilika.
 
Walimu wengi hawakufaulu vizuri mitihani ya kidato cha nne shida ilianzia hapo!!
 
Walimu wa msingi wengi walifeli fom4 na wachache waliofaulu washajiendeleza
 
Watanzania tuache ujanja ujanja wa masuala muhimu kwa Taifa na suala la ajira ni muhimu sana na halihitaji ujuaji mwingi kama wa mleta mada.

Duniani kote suala la mitihani kabla ya ajira linaangaliwa sana na sio huo ufaulu wa Darasani. Muajiri ni lazima atoe mitihani kwa muajiriwa Ili ajue skills and competencies za muajiriwa ,huo ufaulu wa darasani ni kipimo kimojawapo.

Nashangaa mleta mada anapokuja na hoja za kupinga jambo hilo na kutaka mfumo wa kupeana ajira utumike badala ya mfumo wa kushindanisha waombaji.

Mimi sijapinga ila Kimsingi ufaulu wa darasani unabeba 85% na hako kamtihani kanabeba 15%
Labda nikupe mfano: Waalimu wanaofundisha shule za Msingi pengine 80% hawana pass ya Hesabu sasa huo mtihani unasaidia nini kwa mtu ambaye tayari hana pass ya somo husika?.
Kama umefuatilia matokea ya ufaulu wa somo la Hesabu shule za msingi za umma pengine 80% ya wanafunzi hupata alama sifuri kila mwaka kwa sababu ya kuchukua hoja nyepesi nyepesi......
Na hata wakiajiri waalimu wenye degree, kama hawatakua na ufaulu wa somo husika ni kazi bure!!! Tuache ushabiki; Kigezo cha ufaulu wa darasani ndio kila kitu kwa masuala serious kama Academic & Afya mengine ndio yafuate.....
Kuna kazi nyingine nyingi tu zinategemea jitihada za mtu mwenyewe ila sio academic & Afya!
 
Kufanya mtihani sio shida, shida inakuja mtu umemalza form 6 mwaka 2014 alaf uje upewe physics paper 1 leo 2024 umeshakaa mtaani bila ajira ukiendelea na harakati nyingine walau mkono uende kinywani miaka kumi unategemea utatoboa?

Hii ni janja janja tu ya serikali ya kukwepa kutoa ajira,
 
Alama unazopata kwenye mtihani mmoja wa mwisho kuhitimu kozi haziwezi ku determine uwezo wako wa kumudu somo hilo. Maksi hushuka na upanda kadri unavyofanya mitihani. Frequency kamwe haziwezi kuwa zilezile hata ufanye mitihani mia maksi zitakuwa zinapanda au kushuka. Kinachotakiwa ni uwezo wa kulimudu somo unalofundisha. Niliingia kufundisha masomo ambayo nilifeli lakini nafundisha wanafunzi vema na nazidi ku gain momentum. Sasa kama ningesema nilifeli sitaweza kufundisha somo hilo ningepata wapi ujuzi na umahiri wa kulifundisha somo lililonitesa na kufeli huko nyuma? Hawa walimu wapya wafanye tu mitihani ya masomo wanayoenda kufundisha, chuoni wanafundishwa mbinu tu za kufundisha na huko kazini wanaenda kufundisha yale waliyojifunza shuleni kuanzia msingi mpaka sekondari.
Fact
 
Back
Top Bottom