Mbagala, Dar es Salaam: Mahabusu wadaiwa kumpiga askari na kutokomea kusikojulikana

Mbagala, Dar es Salaam: Mahabusu wadaiwa kumpiga askari na kutokomea kusikojulikana

Hakuna kosa dogo wala kubwa Polisi wameshindwa kazi
 
Nchi ya kitu kidoogo... mahabusu mnachanga teni teni watu 20 inapatikana 200,000 mnamkata mitama askari mnatokomea kupoteza ushahidi kwan shi ngap bwana .. kila mtu ashike njia yake ..wote tutakufa tu..askari wenyewe hao wote wana njaa kali ajabu.

Bwahaha [emoji1787]
Hapo nakubaliana na wewe walahi
 
Kila nikijaribu kuelewa ilikuaje!
FB_IMG_16309210488163447.jpg
 
Safi sana.
Nimefurahi kusikia hii Habari.
 
Ila huu msalaa mkubwa wakikamatwa
Hehehe

Ova
 
Salaam wadau,nimeipata tetesi,mahabusu wa kituo Cha polisi maturubai wamevunja lock up na kumpiga Askari ,na hatimaye, wamekumbilia kusikojulikana.
Mwenye taarifa zaidi. Atujuze.
Tumsubiri IGP,NYAKORO, SIMON SIRO,atatueleza,au mwingine mwenye full information.
 
Makosa madogo madogo ni kama yapi? Mtuanapata ujasiri wa kympiga askari mwenye silaha na kuvunja mahabusu unasema makosa madogo madogo, sasa kwanini mliwakamata kama makosa ni madogo? Dawa yao Hamza
 
Mahabusu waliokuwa wanashikiliwa kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai, kilichopo Mbagala wilayani Temeke wametoroka baada ya kumpiga askari kisha kuvunja lango la chumba cha mahabusu na kutokomea kusikojulikana.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja usiku, jijini Dar es Salaam limethibitishwa na Jeshi la Polisi huku likisema wanaendelea na msako wa kuwabaini walipo mahabusu hao.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Murilo alipotafutwa na Mwananchi azungumzie tukio hilo, alisema yuko msibani Kibondo, atafutwe kaimu wake, Daniel Shila ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Kanda ya Maalum Dar es Salaam azungumzie hilo.

Kamanda Shila alipotafutwa na Mwananchi alikiri kuwapo kwa tukio hilo, lakini akasema “waliotoroka ni mahabusu wenye makosa madogo waliokamatwa kwenye doria iliyofanywa na jeshi hilo, si wale wenye kesi mbalimbali.”

MWANANCHI

Sirro yeye hana habari, yupo busy anayaruka Madebe tu
 
Kuvunja na kutoroka huo ni msala!

Kama kuna mwizi wa kesi ya kuku,bata,kupigana
Kama ana akili timamu sijui kama anaweza kutoroka, akitoroka basi kaumia

Ova
 
asante Hamza Mohamed unazidi kutuwakilisha MwenyeziMungu akupunguzie adhabu huko uliko
 
Watakuwa na undugu wa karibu na Shujaa Hamza.

Back
Top Bottom