Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Wakazi wa Mbagala Mzinga Wamefunga barabara ya kutoka Dar kwenda Mikoa ya kusini kwa madai ya kuchoshwa na ajali kwenye eneo lao, jambo hilo limesababisha foleni kubwa ya Magari.
Jambo hilo limemtoa Mkuu wa Mkoa wa DSM ofisini na kumfikisha eneo la Tukio ili kuwaomba wananchi hao waruhusu barabara iendelee kutumika .
Hata hivyo Bwana Chalamila amepokelewa na wimbo mpya uliotungwa eneo la tukio unaoitwa "bao 1 milioni 10 lakini barabara mbovu" ambao haufahamiki maana yake
=======
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewasili eneo la Mbagala Mzinga baada ya wananchi kufunga Barabara ya Kilwa inayounganisha Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya kusini, kwa madai ya kuchoshwa na ajali zinazotokea kila siku.
Chalamila amewasili eneo hilo asubuhi ya leo Mei 17, 2024 na kupokelewa na wananchi hao wakiimba ...goli moja milioni 10 halafu barabara mbovu.
Wananchi hao wamefunga barabara hiyo kutokana na ajali iliyotokea usiku wa jana Alhamisi Mei 16,2024 na kusababisha vifo vya watu wanne.
Kutokana na kufungwa kwa barabara hiyo kuanzia asubuhi ya leo kumesababisha foleni kubwa ya vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara hiyo.