Pre GE2025 Mbagala: RC Chalamila apokelewa kwa Wimbo "Bao 1 milioni 10 lakini barabara mbovu"

Pre GE2025 Mbagala: RC Chalamila apokelewa kwa Wimbo "Bao 1 milioni 10 lakini barabara mbovu"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waacheni waendelee na kumpamba "mama" yao maana siku hizi hadi wanasema kapunguza vifo vya wanaozaa, mara hata madaktari wakifanikisha upasuaji mgumu wanasifia eti "madaktari wa mama" waokoa mgonjwa na sifa zote.
Sasa wananchi watamuondoa huyo anayeshindwa kutengeneza barabara, kuboresha maisha, mishahara na pension bora, ajira za vijana nk kisha huyo anayepunguza vifo watambakiza ila adhibitishe kuwa ni yeye kweli
😆😆😆😆
 
Ukiona Mbagala imeamka jua kumekucha
Hakik
Hatimaye nchi nzima itaamka maana kuna maeneo ya nchi hii hakuna barabara bali zimebakia njia. Pesa wanapewa wasanii, kulipia magoli, kuwalipa machawa, kusafirisha misiba ya watangazaji, kuwatibu wasanii wakati kundi kubwa la watanganyika linataabika kwa kuwa na huduma duni.
Masikini Watanganyika
 
Aise! Bila shaka habari zimeshafika Chamwino! Kwa kuwa Uchaguzi umekaribia Mama ni msikivu ataagiza taasi inayohusika ikalitazame jambo hilo.
 
Soon Dar nzima itaamka.
Ingekuwa na sie tunaonyesha muamko huko mtaani kama hao wamama tungekuwa mbali sana ila sisi kutwa tupo mitandaoni athari ya miamko yetu inaishia humu haionekani huko mtaani.
 
Ingekuwa na sie tunaonyesha muamko huko mtaani kama hao wamama tungekuwa mbali sana ila sisi kutwa tupo mitandaoni athari ya miamko yetu inaishia humu haionekani huko mtaani.
Labda hukuniona kwenye maandamano.
 
Back
Top Bottom