Pre GE2025 Mbagala: RC Chalamila apokelewa kwa Wimbo "Bao 1 milioni 10 lakini barabara mbovu"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
😂😂nimecheka na kuhudhunika sana..😞😞...Sasa Tunaanza kuelewana Cha kusikitisha ..n kwamba Hawa wananchi Hawa (wanafki wenye faida ) wanasubir liwakute wao ndio waonyweshe kuguswa .

Tupaze sauti na mambo mengne yote ya hovyo..mfano taarifa za C.A.G..kwan haya n Kwa maslahi yetu wote...

ila yote Kwa yote mmetisha hata kama Chalamila aliwapanga ,muhimu Ujumbe umefika Naomba 'NITABARUKU'
 
😂🤣🤣 "ambao wimbo huo haujulikani maana yake" aisee
 
Wakazi wa Mbagala Mzinga Wamefunga barabara ya kutoka Dar kwenda Mikoa ya kusini kwa madai ya kuchoshwa na ajali kwenye eneo lao, jambo hilo limesababisha foleni kubwa ya Magari.

Jambo hilo limemtoa Mkuu wa Mkoa wa DSM ofisini na kumfikisha eneo la Tukio ili kuwaomba wananchi hao waruhusu barabara iendelee kutumika .

Hata hivyo Bwana Chalamila amepokelewa na wimbo mpya uliotungwa eneo la tukio unaoitwa "bao 1 milioni 10 lakini barabara mbovu" ambao haufahamiki maana yake

=======
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewasili eneo la Mbagala Mzinga baada ya wananchi kufunga Barabara ya Kilwa inayounganisha Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya kusini, kwa madai ya kuchoshwa na ajali zinazotokea kila siku.

Chalamila amewasili eneo hilo asubuhi ya leo Mei 17, 2024 na kupokelewa na wananchi hao wakiimba ...goli moja milioni 10 halafu barabara mbovu.

Wananchi hao wamefunga barabara hiyo kutokana na ajali iliyotokea usiku wa jana Alhamisi Mei 16,2024 na kusababisha vifo vya watu wanne.

Kutokana na kufungwa kwa barabara hiyo kuanzia asubuhi ya leo kumesababisha foleni kubwa ya vyombo vya moto na watumiaji wengine wa barabara hiyo.

Huo wimbo unamtosha chala.
 
Duh sikuwahi kuiona hii. Hizi clip ndo za kusambazwa kipindi hiki cha kudai Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom