Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kama nilivyoeleza kwenye heading hapo, suala la ulipaji Kodi Kwa sisi Watanzania ni kipengele. Watanzania wengi wetu Kama sio wote hatupendi kulipa Kodi.
Hata wanaolipa Kodi ni kutokana na hawana jinsi mazingira yanawabana tu.
Ila Kama wangeambiwa kwa hiyari yao nakuhakikishia watu wasingelipa kodi.
Watumishi wa Umma kama sio kukatwa juu kwa juu kwenye mishahara Yao na waajiriwa wa sekta binafsi zile kubwa, wangekuwa wanalipwa mikononi mwao kisha wao wenyewe ndio wakalipe Kodi, na kuhakikishia kodi isingelipwa.
Siku ya jana nilikuwa naongea na Mbunge mmoja ambaye ni rafiki yangu sana, akanichekesha mno. Nilipomgusia suala la kukatwa Kodi kwenye mishahara yao, alionyesha kukasirishwa Sana na mpango huo. Hataki kabisa Mshahara wake uguswe, yaani alikuwa mkali Kama mbogo ungedhani Mimi ndiye ninayemkata😃😃😃.
Usishangae Rais halipi Kodi,
Usishangae Mawaziri na wabunge hawalipi Kodi,
Kodi kulipa Kwa Watanzania ni kipengele.
Hata hivyo nafahamu kuna indirect Tax ambazo watu hulipa Kodi, lakini hapa nazungumzia Direct Tax.
Maeneo niliyowahi kuishi, Wafanyabiashara wakisikia TRA au Manispaa wanakuja, utashindwa kushangaa, watu watafunga MADUKA, ofisi na kukaa pembeni wakijifanya sio wakazi wa eneo hilo😃😃😃
Haya ninayoyazungumza wote tunayajua, hakuna asiyejua kuwa Watanzania wengi ni mabingwa waliobobea Kwa kukimbia kulipa Kodi.
Wanaoomba joto ya jiwe ni Wafanyabiashara WA mjini, katikati ya Mji au jiji hawa mazingira hatawaruhusu kuwakimbia TRA Ila vinginevyo, wangekuwa nao wanakimbia tuu.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia nchi hii ingekuwa moja ya nchi zilizoendelea.
Kama Watanzania wengi tungekuwa tunapenda kulipa Kodi, nakuhakikishia Wafanyakazi WA TRA wangekuwa na maisha ya kawaida Sana, kwani mishahara yao sio mikubwa kihivyo lakini Rushwa ndio inawafanya watambe hapa mjini.
Ukitaka kuwabana Watanzania wengi yaani wengi walipe Kodi basi hakikisha unawabana kwenye Maeneo yanayotumiwa na wengi na walipe indirect way.
Kwa mfano, kwenye MIAMALA ya simu, vocha Kama serikali ilivyofanya,
Sema serikali iangalie kwenye Kodi zenyewe wazikatazo waweke walau nafuu sio haya makato nyonyaji,
Masuala ya Luku waongeze, Masuala ya Bill ya maji waongeze,
Lengo sio kuwakomoa Watanzania Bali kuwafanya walipe Kodi, maana Kwa njia ya kawaida serikali imethibitisha haiwezi kulipisha Watanzania Kodi.
Na Watanzania wengi tumethibitisha hatuwezi kulipa Kodi Kwa hiyari yetu pasipo nguvu.
Nawasilisha, mwenye hoja karibu, na wenye povu pia Ruksa
Taikon wa Fasihi
Ruaha, Iringa