Mbali ya SETTINGS nini kingine husababisha CCTV CAMERA ioneahe wrong date/time?

Mbali ya SETTINGS nini kingine husababisha CCTV CAMERA ioneahe wrong date/time?

prida

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
1,297
Reaction score
2,596
Fundi wetu wa uhakika yuko china saaa tumekuwa hoves.Wamekuja fundi wawili tukiwaambia shida wanafanya settings lakini bado mfumo unaonesha mwaka,siku,tarehe na saa isio sahihi

Huyu wa pili anadai kuna battery ya kidude gani sijui inatakiwa kubadilishwa.

Kabla hatujampatia fedha ya hiyo battery tunaomba wataalamu wetu wa JF mtusaidie kujua MBALI YA SETTINGS KIPI HUSABABISHA CCTV CAMERA KUONESHA WRONG TIME/DATE?

Asanteni🙏🙏
By MAMA WAWILI
 
Kwanza ni cmos battery ni battery inayokuwa ndani ikitokea dvr au nvr imezima husaidia kutunza kumbukumbu kwa wakati huo na kama haitafanya kazi basi kumbukumbu zitarudi kama awali 'default settings'.

Pili kama dvr au nvr imeunganishwa na internet angalia current local time ipo +3 mara nyingi inasomeka nairobi au Kuwait, hii inasaidia kuweka mda kulingana na mahali ulipo ikiwa tofauti na masaa yatakuwa tofauti.
 
Angalizo la mwisho prida hakikisha kifaa chako kinakuwa na backup kuondoka usumbufu,

Unaweza kuinunulia UPS ili umeme ukikatika iendelee kuwa hewani maana umeme wa TANESCO kwa siku unakatika hata mara sita
 
Nadhani hicho ndo fundi alisema.
Asante mkuu🙏
 
Angalizo la mwisho prida hakikisha kifaa chako kinakuwa na backup kuondoka usumbufu,

Unaweza kuinunulia UPS ili umeme ukikatika iendelee kuwa hewani maana umeme wa TANESCO kwa siku unakatika hata mara sita
Hicho ni bei gani mkuu?
Ila sijui kipo coz hata umeme ukikatika matukio yanakua recorded
 
Hicho ni bei gani mkuu?
Ila sijui kipo coz hata umeme ukikatika matukio yanakua recorded
APC BACK UP – UPS 650VA Universal Outlet
APC-700-2.webp

Inakuwa namna hii, ila kama unasema ikikatika inaendelea kuwa on basi ipo kwenye backup tayari.
 
Ila kama inapoteza majira bila umeme kukatika huenda ikawa sio shida ya cmos battery.

Iangaliwe kwenye regions kama alivyoshauri jamaa hapo juu, time zone iwe +3.

Na ukiona Mama wawili ameuliza kitu ujue homework ya kutosha imeshafanyika.
 
Mkuu prida, hiyo battery ipo kweli — ndo hiyo CR2032, ndogo kama ya kwenye ubao wa kompyuta (motherboard), iko ndani ya NVR/DVR yenyewe.

Kitu cha kukupa picha: haihusiani kabisa na kurekodi. Kurekodi kunakwenda na umeme/UPS. Hiyo kibattery kazi yake ni kutunza SAA tu kifaa kikizimwa kabisa. Ndo maana ulichanganyikiwa — "umeme ukikatika bado inarekodi" ni kweli, ila saa ni stori nyingine kabisa.

Ikifa: kurekodi kuko sawa, lakini kila NVR ikizimwa na kuwashwa upya, tarehe/saa inarudi default. Hapo ndo unaona hiyo wrong date/time.

Bei yake chee tu (elfu 2-3 hivi), na kuibadilisha ni dakika, kama kubadili battery ya BIOS ya kompyuta. Ukitaka kujua kama ndo hiyo: weka saa sahihi, zima NVR kabisa kama dakika 10, iwashe — kama saa imerudi nyuma, ni hiyo battery.

Tip moja: kama NVR ipo kwenye mtandao, washa time sync (NTP) uweke timezone GMT+3 (Dar). Hapo hata kama battery ni teke, ikiwaka ikiwa online inajirekebisha saa yenyewe.

Usiipuuze ila — saa mbovu inaharibu ushahidi. Kukitokea wizi, footage yenye tarehe/saa isiyo sahihi ni ngumu kuitumia polisi au bima.

Ukihitaji msaada wa kupata hiyo battery au kuseti muda, niandikie. — Zhang YuWen, AtlasCommTech | WhatsApp +86 186 1168 3168
 
Ila kama inapoteza majira bila umeme kukatika huenda ikawa sio shida ya cmos battery.

Iangaliwe kwenye regions kama alivyoshauri jamaa hapo juu, time zone iwe +3.

Na ukiona Mama wawili ameuliza kitu ujue homework ya kutosha imeshafanyika.
FUndi kesharekebisha mkuu🙏
 
Back
Top Bottom