dottoz
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 1,510
- 870
NYOTA wa Kombe la Dunia ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG ya Ufaransa pia, Kylian Mbappe, aliwahi kukataliwa kuchezea timu ya Cameroon ambapo baba yake alitakiwa kutoa malipo ya fedha ambayo alishindwa kuipata. Lakini, Ufaransa, nchi ambayo alizaliwa, ilimchukua na kumwingiza katika ulimwengu mkubwa zaidi wa soka, bure!
Wilfried Mbappe, baba yake nyota huyo aliwahi kuviambia vyombo vya habari kwamba: “Nilitaka mwanangu achezee timu ya taifa ya Cameroon lakini shirikisho la soka likaniambia nitoe fedha kiasi fulani ambayo sikuwa nayo lakini Ufaransa haikunitaka nitoe wala senti moja.”
Mbappe (19) alizaliwa katika kitongoji cha Bondy, jijini Paris, Ufaransa katika familia ya wanamichezo ambapo baba yake alikuwa mcheza soka na kocha, mama yake aitwaye Fayza Lamari, alikuwa mcheza mpira wa mikono (handball). Vilevile, kaka yake wa kambo, Jires Kembo-Ekoko, ni mcheza soka wa kulipwa ambaye amecheza sehemu mbalimbali duniani, hivyo kumsaidia sana Kylian katika medani ya soka.
Mama yake Mbappe, Fayza Lamari, ni mwenye asili ya Algeria, na baba yake ni mwenye asili ya Cameroon, zote nchi za Afrika.
Nyota huyo ambaye aliing’arisha Ufaransa, ni mmoja wa wanasoka mahiri wapatao 15 wenye asili ya Afrika wanaoichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, na hivyo kuifanya iwe na mashabiki lukuki duniani wenye asili ya Afrika.