Mbappe: ‘Jiwe Walilolikataa Cameroon’ Limekuwa Jiwe Kuu la Ufaransa

dottoz

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
1,510
Reaction score
870
NYOTA wa Kombe la Dunia ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG ya Ufaransa pia, Kylian Mbappe, aliwahi kukataliwa kuchezea timu ya Cameroon ambapo baba yake alitakiwa kutoa malipo ya fedha ambayo alishindwa kuipata. Lakini, Ufaransa, nchi ambayo alizaliwa, ilimchukua na kumwingiza katika ulimwengu mkubwa zaidi wa soka, bure!

Wilfried Mbappe, baba yake nyota huyo aliwahi kuviambia vyombo vya habari kwamba: “Nilitaka mwanangu achezee timu ya taifa ya Cameroon lakini shirikisho la soka likaniambia nitoe fedha kiasi fulani ambayo sikuwa nayo lakini Ufaransa haikunitaka nitoe wala senti moja.”

Mbappe (19) alizaliwa katika kitongoji cha Bondy, jijini Paris, Ufaransa katika familia ya wanamichezo ambapo baba yake alikuwa mcheza soka na kocha, mama yake aitwaye Fayza Lamari, alikuwa mcheza mpira wa mikono (handball). Vilevile, kaka yake wa kambo, Jires Kembo-Ekoko, ni mcheza soka wa kulipwa ambaye amecheza sehemu mbalimbali duniani, hivyo kumsaidia sana Kylian katika medani ya soka.

Mama yake Mbappe, Fayza Lamari, ni mwenye asili ya Algeria, na baba yake ni mwenye asili ya Cameroon, zote nchi za Afrika.

Nyota huyo ambaye aliing’arisha Ufaransa, ni mmoja wa wanasoka mahiri wapatao 15 wenye asili ya Afrika wanaoichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, na hivyo kuifanya iwe na mashabiki lukuki duniani wenye asili ya Afrika.
 
Mkuu wewe ni mshabiki wa yanga nini??

Naona jana mkapigwa 4 bila aiseeeee.
Sishabikii ligi ya bongo, huyo ngasa sijui hata anacheza timu gani zaidi ya kumsikia akizungumzwa huku mtaani
 
dah kipaji chake atoe pesa tena, daah huenda hata hapa lipo?
 
Serikali za kiafrika zinaua vipaji. Kikitokea kipaji wanachoa angalia kwanza kama watapata pesa kutokana na hiko kipaji kama hamna wanakipotezea.

Ndio maana vipaji vingi afrika vinafia njiani maana serikali wenyewe wanaviua.
Kesi kama ya mbappe kama baba ake asingempeleka ufaransa leo hii mbappe labda angekuwa dereva wa malori.

Mchawi wa waafrika ni waafrika wenyewe.
 
Sishabikii ligi ya bongo, huyo ngasa sijui hata anacheza timu gani zaidi ya kumsikia akizungumzwa huku mtaani
Sasa kiwango chake umekijuaje mpaka kumlinganisha na Mbape mzaliwa Afrika!!?
Waswahili bhana!!! Unaanzaje kumzungumzia mtu usiyemfahamu?
 
Angekwenda Cameroon sidhani kama angekuwa na kiwango alicho nacho sasa.
Angekuwa kama Ngasa tu
sio kweli wakina Etoo,Drogba,Kuffor,Yahya Toure na kaka yake, Samatta,Wanyama na kaka yake nk...bidii ya mtu na malengo..
 
NYOTA wa Kombe la Dunia ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya PSG ya Ufaransa pia, Kylian Mbappe, aliwahi kukataliwa kuchezea timu ya Cameroon ambapo baba yake alitakiwa kutoa malipo ya fedha ambayo alishindwa kuipata. Lakini, Ufaransa, nchi ambayo alizaliwa, ilimchukua na kumwingiza katika ulimwengu mkubwa zaidi wa soka, bure!

Wilfried Mbappe, baba yake nyota huyo aliwahi kuviambia vyombo vya habari kwamba: “Nilitaka mwanangu achezee timu ya taifa ya Cameroon lakini shirikisho la soka likaniambia nitoe fedha kiasi fulani ambayo sikuwa nayo lakini Ufaransa haikunitaka nitoe wala senti moja.”

Mbappe (19) alizaliwa katika kitongoji cha Bondy, jijini Paris, Ufaransa katika familia ya wanamichezo ambapo baba yake alikuwa mcheza soka na kocha, mama yake aitwaye Fayza Lamari, alikuwa mcheza mpira wa mikono (handball). Vilevile, kaka yake wa kambo, Jires Kembo-Ekoko, ni mcheza soka wa kulipwa ambaye amecheza sehemu mbalimbali duniani, hivyo kumsaidia sana Kylian katika medani ya soka.

Mama yake Mbappe, Fayza Lamari, ni mwenye asili ya Algeria, na baba yake ni mwenye asili ya Cameroon, zote nchi za Afrika.

Nyota huyo ambaye aliing’arisha Ufaransa, ni mmoja wa wanasoka mahiri wapatao 15 wenye asili ya Afrika wanaoichezea timu ya taifa ya nchi hiyo, na hivyo kuifanya iwe na mashabiki lukuki duniani wenye asili ya Afrika.
Usisahau wa Nigeria walimkataa ANTHONY JOSHUA (AJ) a.k.a FEMI BOY.
 
Natamani sana kujua why Yusuf Bakheresa anapeleka wachezaji wake Spain, na sio France..... kwangu mimi naiona France kama shortcut
 
Afrika inapoteza mengi kwa kwa tamaa za wachache. tuvumilie tu maana hatuwezi kuhama
 
Back
Top Bottom