UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MBARALI, VYAMA VITANO VYAJITOKEZA
Vyama
vitano vyachukua fomu za uteuzi uchaguzi mdogo jimbo la Mbarali Tanzania. Hayo yabainishwa na
msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbarali Bw. Missana Kwanguru katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Kofia nyingine ya Bw. Missana Kwangaru yeye ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbalali Mkoa wa Mbeya.
KAMPENI ZAANZA KWA KISHINDO
09 Sept. 2023
DP chama cha Mtikila ktk kampeni jimbo la Mbarali, Mbeya uchaguzi mdogo wa mbunge, rudisheni kadi za CCM kama kule Mtwara
View: https://m.youtube.com/watch?v=Btsmwhomk6Y
Mgombea wa
DP Mzee Oswald Joseph Mndeva aanza kampeni kabambe huku akiwaomba wakaazi wote wa Mbarali waichague
DP ili waweze kuendelea na shughuli za maendeleo za kilimo, uvuvi na ufugaji ambazo ni shughuli kuu maeneo ya Usangu ambazo zinapata changamoto kutokana na sera mbovu
CCM katika sekta hizo tahwa zinaziajiri maelfu ya wakaazi wa Mbarali.
Wagombea wengine ni Halima Abdallah Magambo wa
AAFP, Bw. Zavery Laurent Seleleka wa
UDP, Bw. Exavery Town Mwataga wa
CCK, Bw.Bosco Daudi Mahenge wa
UPDP huku chama kikongwe cha
CCM Bi. Bahati Ndingo ndiyo anasimama.
Uchaguzi huo mdogo unatazamiwa kufanyika tarehe 19 September 2023 taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyotundikwa katika tovuti yake rasmi
www.nec.go.tz /news inasema.