Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji ( NWF) imekamilisha kwa asilimia 100 mradi wa maji wa Ruduga Mawindi uliopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa gharama ya shilingi bilioni 5.2.
Kwa sasa mradi huo unahudumia vijiji sita ambavyo awali wananchi wake walikuwa wanatumia maji ya mto Ruaha ambayo yaliwaweka hatarini kiafya.
Pia soma: Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Wakazi hao wamesema hawakuwa na tumaini la kupata huduma ya maji safi na salama tangu mwaka 1994 walipochanga fedha kwa ajili ya kupata mradi wa maji safi na baadae fedha hizo kutojulikana zilipo.
Wameipongeza Serikali kwa kuwapelekea huduma hiyo ya maji safi na salama ambayo kwa sasa wanaipata saa 24, na imeondoa karaha nyingi za utafutaji maji kwenye mito na makorongo.
"huko mahospitalini kila atakaeenda kutoka katika kijiji hiki cha Matemela lazima apimwe ana typhoid mpaka madaktari walilalamika huko kwenu kuna nini, tukasema tatizo maji tunayokunywa sio salama".
amesema Felechina Mganda, mkazi wa Matemela, Mbarali
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mbarali Mhandisi Samweli Hechei amesema kukamilika kwa mradi wa maji wa Ruduga Mawindi kumeongeza maradufu upatikanaji wa maji safi na salama.