Mbaroni kwa kumpiga risasi ya paja mtu aliyetaka kumshambulia kwa shoka

Mbaroni kwa kumpiga risasi ya paja mtu aliyetaka kumshambulia kwa shoka

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mlinzi wa Kampuni ya Kachipa aitwaye James Mtongori (28) Mkazi wa Katoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kumpiga risasi pajani, Kijana Kulwa Sylvester (26) Mkazi wa Katoro Tarafa ya Buseresele Mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema kabla ya kujeruhiwa Kulwa alitaka kumkata kwa shoka Mlinzi huyo ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi kwenye paja.

"Kabla ya kujeruhiwa alitaka kumdhuru Mtuhumiwa kwa kumkata na shoka ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi, Mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma”

Aidha Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa Wananchi pamoja na Walinzi wa Kampuni mbalimbali kutojichukulia sheria mkononi “Kulwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Katoro na anaendelea vizuri”
 
James ahamishiwe Dar ili awasaidie raia wanaoonewa na panya road. Huku Dar watu wana silaha lakini wanaogopa kuzitumia.

Kamanda Mwaibambe afikishwe kortini kueleza ni kwa namna gani James anatuhumiwa kwa kujichukulia sheria mkononi.
 
Tuna polisi ya kidwanzi sana, hawa ni wajinga sana.

Mtu una jihami halafu unawekwa rumande huo si usng nini maana ya kumiliki chopper sasa?

Huoni hapo unawakata matumaini watu wanaomiliki gun endapo watajaribu kujihami dhidi ya uvamizi wa panya road ambao umekuwa ukiwaweka watu katika hofu kubwa?
 
James ahamishiwe Dar ili awasaidie raia wanaoonewa na panya road. Huku Dar watu wana silaha lakini wanaogopa kuzitumia.

Kamanda Mwaibambe afikishwe kortini kueleza ni kwa namna gani James anatuhumiwa kwa kujichukulia sheria mkononi.
Mi nikiwa na chopper afu wametokea panya road, hayo maneno ya huyo polisi kwangu ni upuuzi tu
 
Mlinzi wa Kampuni ya Kachipa aitwaye James Mtongori (28) Mkazi wa Katoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kumpiga risasi pajani, Kijana Kulwa Sylvester (26) Mkazi wa Katoro Tarafa ya Buseresele Mkoani Geita.
Ndio sheria. Sometimes sheria inashangaza. Wakati ule adhabu ya kunyonga ilikuwa inatekelezwa. Yule mnyongaji baada ya kunyonga anapelekwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya kuua nakuachiwa na Tena akinyonga anapelekwa Tena hivyo hivyo mahakamani na kuachiwa. Sasa Unabaki kushangaa tu WTF?!
 
Jamani james kapewa silaha kwa ajili ya ulinzi wa kampuni na si kwa ajili ya masuala yake binafsi, hiyo ina maana silaha itatakiwa kutumika pale endapo kuna jambo lolote la kuhatarisha kampuni au mali ya kampuni limetokea au kutaka kufanyika, tofauti na hapo risasi hiyo haina kibali cha kutumika kwa ulinzi binafsi wa james, tayari ni kinyume na sheria
 
Kosa la James kufikishwa mahakamani ni nini?
Kosa la mlinzi James Mtongori (28) linalo sababisha kushikiliwa na Polisi ni kumpiga risasi pajani kijana Kulwa Sylvester (26) bila ushahidi. James alitakiwa asubiri kupigwa shoka na Kulwa ili ushahidi ukamilike.

Jeshi la Polisi tunawatakia kazi njema, ili HAKI ikapatikane MAHAKAMANI
 
Jamani james kapewa silaha kwa ajili ya ulinzi wa kampuni na si kwa ajili ya masuala yake binafsi, hiyo ina maana silaha itatakiwa kutumika pale endapo kuna jambo lolote la kuhatarisha kampuni au mali ya kampuni limetokea au kutaka kufanyika, tofauti na hapo risasi hiyo haina kibali cha kutumika kwa ulinzi binafsi wa james, tayari ni kinyume na sheria
Kwa hiyo James alitakiwa atulie tu ili shoka litue kichwani na kumuondoa duniani?
 
Jamani james kapewa silaha kwa ajili ya ulinzi wa kampuni na si kwa ajili ya masuala yake binafsi, hiyo ina maana silaha itatakiwa kutumika pale endapo kuna jambo lolote la kuhatarisha kampuni au mali ya kampuni limetokea au kutaka kufanyika, tofauti na hapo risasi hiyo haina kibali cha kutumika kwa ulinzi binafsi wa james, tayari ni kinyume na sheria
Kwaio ilitakiwa mguu uondolewe tu huku bunduki ikiwa kwapani kama pambo!!!

Andha kanoon!

Kusema kusudio ni kulinda mali ya kampuni, vipi ikiwa mshambuliaji alitaka amuue mlinzi ndio akafanye uhalifu?
 
Back
Top Bottom