Mbaroni kwa kumpiga risasi ya paja mtu aliyetaka kumshambulia kwa shoka

Mlinzi wa Kampuni ya Kachipa aitwaye James Mtongori (28) Mkazi wa Katoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kumpiga risasi pajani, Kijana Kulwa Sylvester (26) Mkazi wa Katoro Tarafa ya Buseresele Mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema kabla ya kujeruhiwa Kulwa alitaka kumkata kwa shoka Mlinzi huyo ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi kwenye paja.

"Kabla ya kujeruhiwa alitaka kumdhuru Mtuhumiwa kwa kumkata na shoka ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi, Mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma”

Aidha Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa Wananchi pamoja na Walinzi wa Kampuni mbalimbali kutojichukulia sheria mkononi “Kulwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Katoro na anaendelea vizuri”
Huyo msemaji wa polisi chenga
 
Ndio sheria. Sometimes sheria inashangaza. Wakati ule adhabu ya kunyonga ilikuwa inatekelezwa. Yule mnyongaji baada ya kunyonga anapelekwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya kuua nakuachiwa na Tena akinyonga anapelekwa Tena hivyo hivyo mahakamani na kuachiwa. Sasa Unabaki kushangaa tu WTF?!
Hahaha mkuu nimecheka balaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Jamani james kapewa silaha kwa ajili ya ulinzi wa kampuni na si kwa ajili ya masuala yake binafsi, hiyo ina maana silaha itatakiwa kutumika pale endapo kuna jambo lolote la kuhatarisha kampuni au mali ya kampuni limetokea au kutaka kufanyika, tofauti na hapo risasi hiyo haina kibali cha kutumika kwa ulinzi binafsi wa james, tayari ni kinyume na sheria
Una akili timamu?

Baada ya kumuua kwa shoka kisha angepora hiyo silaha mini kingefuata?

Wewe ni Division Zero kama Kamanda Mwaibambe!
 
Nchi hii matatizo matupu,wakati fulani Mambosasa akiwa kamanda wa polisi kanda maalumu Dsm niliwahi kumsikia akiwalamikia na kuwalaumu baadhi ya watu wanaomiliki silaha kihalali lakini wanashindwa kujiami pale unapotokea uhalifu sasa huko mtu kaitumia kwa kujiami halafu tena yeye ndiye anakamatwa!
 
Mlinzi wa Kampuni ya Kachipa aitwaye James Mtongori (28) Mkazi wa Katoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa kumpiga risasi pajani, Kijana Kulwa Sylvester (26) Mkazi wa Katoro Tarafa ya Buseresele Mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema kabla ya kujeruhiwa Kulwa alitaka kumkata kwa shoka Mlinzi huyo ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi kwenye paja.

"Kabla ya kujeruhiwa alitaka kumdhuru Mtuhumiwa kwa kumkata na shoka ndipo Mtuhumiwa alijihami kwa kumfyatulia risasi na kumjeruhi, Mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano na upelelezi ukikamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma”

Aidha Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa Wananchi pamoja na Walinzi wa Kampuni mbalimbali kutojichukulia sheria mkononi “Kulwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Katoro na anaendelea vizuri”
Acheni upumbavu,kwa hiyo angekaa tuu apigwe shoka?
 
Una akili timamu?

Baada ya kumuua kwa shoka kisha angepora hiyo silaha mini kingefuata?

Wewe ni Division Zero kama Kamanda Mwaibambe!
Sawa division one,
Ingekuwa hivyo basi walinzi wote wangekuwa na haki ya kutumia silaha kwa raia yeyote atakaewasogelea,
 
James hana kosa na hata akipandishwa mahakamani anashinda hiyo case. Alichokifanya ni SELF DIFENCE hata kama angemtandika risasi ya kifua huyo aliyeshika shoka. Walichofanya polisi ni utaratibu wa kawaida tukio lihusisho siraha ya moto litokeapo..
 
Kosa la mlinzi James Mtongori (28) linalo sababisha kushikiliwa na Polisi ni kumpiga risasi pajani kijana Kulwa Sylvester (26) bila ushahidi. James alitakiwa asubiri kupigwa shoka na Kulwa ili ushahidi ukamilike.

Jeshi la Polisi tunawatakia kazi njema, ili HAKI ikapatikane MAHAKAMANI
Hahahahaaa apigwe shoka ushahidi upatikane hatari sana
 
Ukiua au ukijeruhi wakati unajilinda, yote ni shida; nini umuhimu wa kumiliki silaha?
 
Ndio sheria. Sometimes sheria inashangaza. Wakati ule adhabu ya kunyonga ilikuwa inatekelezwa. Yule mnyongaji baada ya kunyonga anapelekwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya kuua nakuachiwa na Tena akinyonga anapelekwa Tena hivyo hivyo mahakamani na kuachiwa. Sasa Unabaki kushangaa tu WTF?!
Chai hii [emoji1787]
 
Jamani james kapewa silaha kwa ajili ya ulinzi wa kampuni na si kwa ajili ya masuala yake binafsi, hiyo ina maana silaha itatakiwa kutumika pale endapo kuna jambo lolote la kuhatarisha kampuni au mali ya kampuni limetokea au kutaka kufanyika, tofauti na hapo risasi hiyo haina kibali cha kutumika kwa ulinzi binafsi wa james, tayari ni kinyume na sheria
Bush Lawyer
 
Back
Top Bottom