Mbaroni kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa darasa la saba

Mbaroni kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa darasa la saba

Ni muendelezo wa umaskini mkubwa nchini, huyu binti chanzo kikubwa cha kupoteza maisha yake ni umaskini wa familia yao - inasemekana ALIBAKWA ambapo haijulikani aliyembaka ni nani na ni nini kilisababisha hadi abakwe.

Watoto wengi wa kike ambao bibi zao ama mama zao wanafanya biashara ya Pombe za kienyeji ni tatizo kubwa,
Yaan mkuu unauliza kilichosababisha yeye abakwe aisee unataka kutuaminisha hapa Kuwa wanaobakwa huwa Kuna kitu wanafanya na kupeleka kubakwa
 
Kwa nini ni tatizo mkuu ?
 
Yaan mkuu unauliza kilichosababisha yeye abakwe aisee unataka kutuaminisha hapa Kuwa wanaobakwa huwa Kuna kitu wanafanya na kupeleka kubakwa
hujajua hoja yangu? je binti alikuwa protected baada ya kubakwa? jibu hapana - kwa nini ?
 
Dodoma sip mkoa Salama kabisa..narudia Dodoma sio mkoa Salama licha ya kujazwa vyombo vya usalama.

Ndugu yangu alifika Dodoma akaingia Lodge hakuamka Tena!! Wahuni wakamzamisha silaha za kutosha!!! So sad!
 
Pole mkuu ni majambazi walimuuwa?
 
Apumzike wa amani 🙏
Hizi roho za kikatili zimeshika hatamu
 
hujajua hoja yangu? je binti alikuwa protected baada ya kubakwa? jibu hapana - kwa nini ?

Kama ni kulipiza kisasi kwa nini watoto wengine wabakie salama na binti pekee ndiye auawe ?
Binti yule darasa la Saba mkuu anawajua karibu watu wote mtaani kwake unategemea umbake umuache na anakufahamu SI atasema tu kina Fulani wamenifanyia hivi aisee so usiulize why kauliwa waliofanya hivyo wanajua atawataja simple tu mkuu hapo
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Halafu kuna mashoga sijui wanaharakati wafirwa watu kama hao wakikamatwa wakashughulikiwa ipasavyo ,wanaanza kuchongoa midomo kama chuchunge.
 
Ni Jumatatu Tarehe 3/10/2022 Farida anajiandaa na kwenda zake Shule akiwa ni Binti wa Darasa la Saba.

Farida anaenda Shule huku akiwa amejiandaa vyema kwa Mtihani wake wa Kumaliza Elimu ya Msingi.

Farida ana wadogo zake wawili ambao wanamuona Dada yao kama mfano kwao.

Alasiri Farida anarudi Nyumbani, anakutana na wadogo zake na Mama yake.

Jioni Mama Farida anaondoka kwenda kwenye Mihangaiko na kuwaacha Watoto wake Nyumbani huku akiamini atawakuta salama salimini.

Lahaula.... Majira ya Giza linapoanza kumea Wahuni wanaingia Ndani kwa Mama Farida, Wanawakuta watoto wake Watatu (Farida na Wadogo zake 2) huku Mama akiwa kaenda kuwatafutia Mkate wanawe.

Wahuni wanamkamata Farida, WANAMBAKA na baada ya hapo wanamuangushia kipigo, wanamtoa nje wanamuacha huku Damu zikiwa zinavuja.

Masikini... wadogo zake Farida, wanashuhudia unyama anaofanyiwa Dada yao lakini hawana cha Kufanya.

Mama anarudi kutoka kwenye kutafuta Mkate wa watoto wake, anakutana na Watoto wake wawili wakiwa katika hofu kubwa na Damu ikiwa imemwagika Nyumbani kwake.

Mama anauliza Dada yenu yupo wapi watoto kwa hofu wanamuangalia Mama Yao huku Machozi yakiwatoka anafuatilia Damu anakutana na Binti yake akiwa anahema kwa mba...li Sana.

Kilio kinamtoka, Majirani wanakuja na kumsaidia kumpeleka Farida hospitali.

Njiani Farida anakata Roho na Mauti yanamfika.

FARIDA MAKUYA

Ni nani?
Ni Binti aliyekuwa akisoma Darasa la Saba (2022) na alitarajiwa Kufanya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi Tarehe 5-6/10/2022.

Anaishi wapi?
Mtumba

Anasoma wapi?
Mtumba Shule ya Msingi.

Mkoa Gani?
Dodoma

Ninashindwa kuendelea kuandika, Roho inauma Sana. Unyama aliotendewa unaumiza Sana.

Pumzika kwa Amani FARIDA MAKUYA.
Poleni sana wafiwa. !!
 
Naendelea kusema na sitichoka, tunapaswa kuanza kutekeleza adhabu ya kùnyonga watu mpaka kufa mara baada ya hukumu ya Mahakama.

Rais ashauriwe vizuri na aanze kuridhia hukumu hizi zitekelezwe, wahukumiwa wa mauaji WANYONGWE!

Hakuna sababu yoyote yenye mashiko ya kutokutekeleza adhabu hii.

Watu wameshajichokea,wanajua wakiua wataenda gerezani na watakula na kulala bure, adhabu ya kufungwa maisha haiwasumbui tena.

Roho za ajabu watu wa aina hii kupiga sindano za kifo tuu habari za haki za binadamu siyo wakati wake huu tena, watu wamekua hatari zaidi ya wanyama wa porini.
 
Poleni sana.. hapo hata sijaona motive ya wao kumpiga. Labda aliwatambua.
 
Back
Top Bottom