Mbaroni kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa darasa la saba

Mbaroni kwa tuhuma za kubaka na kumuua mwanafunzi wa darasa la saba


Naendelea kusema na sitichoka, tunapaswa kuanza kutekeleza adhabu ya kùnyonga watu mpaka kufa mara baada ya hukumu ya Mahakama.

Rais ashauriwe vizuri na aanze kuridhia hukumu hizi zitekelezwe, wahukumiwa wa mauaji WANYONGWE!

Hakuna sababu yoyote yenye mashiko ya kutokutekeleza adhabu hii.

Watu wameshajichokea,wanajua wakiua wataenda gerezani na watakula na kulala bure, adhabu ya kufungwa maisha haiwasumbui tena.

Ni kweli watu hawana hofu kabisa.
 
Mkoa huu wa dodoma ni makao makuu ya nchi lkn una matukio ya ajabu na mabaya sana..
 
Wanyongwe mara moja kabla hawajashtakiwa wanaweza kushinda kesi
 
Dah.....hao wanyama wakidakwa sijui wapewe adhabu ipi
Wapigwe za kichwa ndio adhabu inayowafaa hakuna kucheka nao mhuni akifanya uhuni na wewe mfanyie uhuni kupitiliza hio ndio dawa ya mhuni

Piga shaba za kichwa wote wakajielezee huko kuzimu pumbafu

Imeuma sana hawatakiwi kuchekewa kabisa hao simbiilisi watoto wa Ibilisi
 
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji wa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16) aliyeuawa usiku akiwa nyumbani kwao Oktoba 4, 2022.

View attachment 2378787
Marehemu enzi za uhai wake

Binti alitakiwa kuwa miongoni kwa watahiniwa wa mitihani wa darasa la saba inayotamatika leo nchi nzima. Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati wa tukio hilo la mauaji.

Huzuni ilitawala wakati wa maziko yake hapo jana.

” Tukio la kifo chake ni baya kuelezeka,” amesema Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Martin Otieno.

“Kwa sasa tumewakamata watu wawili kwa mahojiano na ikithibitika watafikishwa mahakamani,” amesema.

Inasemekana binti huyo alishambuliwa wakati mama yake alipoondoka nyumbani kwenda kuuza pombe za kienyeji na aliporudi akiwa amelewa alikutana na michirizi ya damu kuanzia mlangoni baada ya kuwasha tochi ya simu yake.

Baada ya shambulio hilo, binti huyo alipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu kabla ya kufikwa na umauti.

----
😥😥 R I p pc kar
 
Wamebaka wameua ...waliwe ndogo na wauwawe.
Wake za nyapala hao
Afande bila kusahau kumpa Nyapala Mkuyati .
#Unyama Mwingi sana
 
Dodoma sip mkoa Salama kabisa..narudia Dodoma sio mkoa Salama licha ya kujazwa vyombo vya usalama.

Ndugu yangu alifika Dodoma akaingia Lodge hakuamka Tena!! Wahuni wakamzamisha silaha za kutosha!!! So sad!
Ilikuaje??
 
Wapigwe za kichwa ndio adhabu inayowafaa hakuna kucheka nao mhuni akifanya uhuni na wewe mfanyie uhuni kupitiliza hio ndio dawa ya mhuni

Piga shaba za kichwa wote wakajielezee huko kuzimu pumbafu

Imeuma sana hawatakiwi kuchekewa kabisa hao simbiilisi watoto wa Ibilisi
Subhanallah. Wanaweza wakakamatwa na kuadhibiwa wasio wahusika, na wahusika wakaendelea kudunda na kufanya uhalifu
 
Subhanallah. Wanaweza wakakamatwa na kuadhibiwa wasio wahusika, na wahusika wakaendelea kudunda na kufanya uhalifu
Imeandikwa 'usimnyime mtoto kiboko' sasa hao kiboko chao ni kuwatembezea moto na kitu cha moto
 
Kuna movie inaitwa tears of the sun, Bruce William, akiwa Kama luten,wa jeshi la Mmarekani,ametumwa Nigeria for rescue mission anakuta wamisionari wanakaribia kuvamiwa, Lakini padre wa kikatoliki anagoma kuondoka anamuaga Bruce" Go with God, Bruce anamjibu God has already left Africa" haya Mambo yanathibitisha kauli hii [emoji24][emoji24]
 
Waliotekeleza hili tukio wakikamatwa adhabu ni kunyongwa mpaka kifo. Mambo mengine nashindwa kuelewa kwanini mtu anafanya tena kwa mtoto mdogo kama huyo. Inasikitisha.
Hapa ndio wanawake wanapaswa kuona umuhimu wa baba na kuwa na mtoto wa kiume tena atakayelelewa na baba.
 
Back
Top Bottom