Mbasha afurahia wanawake wanavyompenda

Mbasha afurahia wanawake wanavyompenda

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598

Msanii wa muziki wa Injili, Emanuel Mbasha ambaye wengi humsifia kwa utanashati wake, amesema anamshukuru Mungu kwa kuonyeshwa kupendwa, baada ya mabinti wengi kumtamani kimapenzi.

Akiongea na eNewz ya East Africa Television, Emmanuel Mbasha amesema ingawa wanawake wengi wanafunguka hisia za mapenzi juu yake, lakini anamuomba Mungu ampe mtu sahihi zaidi ili yasije yakajirudia yaliyomkuta awali.

"Wadada wengi wananipenda wa kila aina na hiyo iko wazi, ukiangalia DM yangu kila siku inajaa meseji, kuna kila aina, na ninamshukuru Mungu kwa kipaji hicho, maana yake kupendwa nako ni kibali na ni baraka za Mungu, sasa nikikurupuka tu kuchukua nitaingia majanga, natamani nipate mtu sahihi, nifanye naye maisha tupate watoto tuendelee mbele, maana yake sitawaza kukaa hivi milele ila kwa sasa sina sababu ya kukurupuka", amesema Emmanuel Mbasha.

Mbasaha ambaye amesema amechoshwa na upweke, ameendelea kusema kwamba..."mimi nimetokea kwenye changamoto kubwa sana ya mahusiano, angekuwa mwengine angedata angeanza kunywa pombe, kuvuta bangi na kufanya mabaya, lakini nilisimama na Mungu, hivyo nimetulia nikisubiria Mungu aniletee mtu sahihi".

Emmanuel Mbasha ameachana na aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mwanamuziki wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha, huku akimshtaki kwa kosa la kumbaka mdogo yake, kesi ambayo Emmanuel aliachwa huru kutokana na kukutwa hana hatia.

Muungwana
 
awe muwazi tu[emoji20]
 
Kumbe kupendwa kipaji , basi na mie ninacho
 
kwa alichofanyiwa na dada yule naona bado ana moyo wa chuma big up mbasha[emoji119]
 
hatari sana ina maana hana mtu anayemsaidia kwa sasa toka aachane na mkewake
 
Mimi sijawahi kupenda dress code manguo ya kuwaka kila mda casual kwakwe mwiko kila SAA ni kama anaenda kufunga ndoa....kwa mwanaume rijali haipendez mwanaume avae rangi za kiume kama idriss sultan au king kiba....huyu mbasha na themed PhD lao moja.
 
Kiukweli Mungu amuongoze katika njia iliyosahihi maana alichopitia ni ngumu sana kukibeba kwa hali ya kawaida mke wako wa ndoa kukutengenezea kesi ya ubakaji mvua 30 tena bila aibu hakuweza kuificha dhamira yake mbele za watu nilitokea kumchukia sana huyo mwanamke ila Mungu amsamehe ila ulimpiga muhuri ambao hautamtoka milele Name Mbasha sikumbuki tena nyimbo yake hata moja ambayo alishawahi kuimba
 
Back
Top Bottom