Mbatia achachamaa, ahoji Deni la Taifa limefikaje Tsh 71 trilioni? Ataka Serikali iombe radhi

Mbatia achachamaa, ahoji Deni la Taifa limefikaje Tsh 71 trilioni? Ataka Serikali iombe radhi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
1623140203532.png

Mwenyekiti wa NCCR, Mageuzi Mh. Mbatia amehoji inakuwaje leo tunaambiwa deni la taifa limefika tsh 71 trilioni? Kwa miradi gani mbona hatuioni?

Mbatia amedai mbona serikali ilikuwa inatuambia haikopi ila inatumia fedha zetu za ndani?

Mbatia ameitaka serikali iombe radhi wananchi kwa kutubebesha mzigo wa deni bila kutujulisha mapema.

Source:
Clouds tv!
 
Wakati wa Jiwe jamaa alikuwa kimya akila dili butu la kuwa ati chama kikuu cha Upinzani Bungeni, sasa sijui kiko wapi. Wenzake wanazunguka mikoani ku-huisha uhai wa chama chao, yeye yupo ofisini anasubiri kipenge cha uchaguzi ashiriki - ili aitangazie Dunia kwamba uchaguzi ulikuwa huru na haki.

Huyu mzee bana.
 
Baada ya sponsor kwenda zake ndio anapata akili za kuhoji deni la taifa. Anyways, ile slogan za pesa zetu za ndani maana yake ilikuwa tutalipa wenyewe hayo madeni, si unajua tena hatuwezi kusema mabeberu wanatukopesha pesa za maendeleo na hela za wastaafu tumenunulia ndege.
 
Baada ya sponsor kwenda zake ndio anapata akili za kuhoji deni la taifa.
Anyways, ile slogan za pesa zetu za ndani maana yake ilikuwa tutalipa wenyewe hayo madeni, si unajua tena hatuwezi kusema mabeberu wanatukopesha pesa za maendeleo na hela za wastaafu tumenunulia ndege.
Huku ndiyo walipokuwa wanapigia pesa haswa kwenye miradi mikubwa
 
Back
Top Bottom