Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mwanasiasa mkongwe, James Mbatia, amesisitiza kuwa kisheria yeye ndiye Mwenyekiti wa halali wa chama cha NCCR-Mageuzi kufuatia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akizungumza kwenye mahojiano, Mbatia ameeleza kuwa baada ya kuondolewa madarakani kinyume cha sheria, aliamua kufuata njia za busara na hekima kwa kwenda mahakamani kwa takriban miaka miwili, ambapo mahakama ilitangaza kuwa maamuzi yote yaliyofanywa dhidi yake yalikuwa batili na kurejesha uenyekiti pamoja na uwanachama wake.
Pia, Soma: Mbatia aibwaga NCCR Mageuzi mahakamani
Ikumbukwe kuwa, Machi 29, 2025 Khamis achaguliwa mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, amrithi Mbatia
Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi ulimchagua Haji Khamis kuwa mwenyekiti wa chama hicho akichukua nafasi ya James Mbatia aliyekuwa mwenyekiti.
Wajumbe wa mkutano huo walimchangua Khamis kwa kura 508 kati ya kura 511, huku kura moja ikimpinga na mbili ziliharibika.
Khamis alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar na muda mrefu amekuwa akikaimu nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho baada kuondolewa James Mbatia.