Mbegu za mahindi DK ni mbegu bora

Jifunafu

Senior Member
Joined
May 25, 2020
Posts
182
Reaction score
693
Wakuu, Leo nimetembelea maonyesho ya wakulima hapa rock city na nikapita mabanda mbali mbali ya wauzaji na wazalishaji wa mbegu Bora za aina mbali mbali.

Kilicho nivutia ni Hawa kampuni ya mbegu za mahindi ya DIKALEB,jamaa wana mbegu Bora na za kiwango Cha juu.

Ninapenda kulima zao hili na nitapanda mbegu za Hawa jamaa na kuzingatia maelekezo yote walio nipa.

Wakuu Kama kunamtu mwingine anajua zaidi mbegu Bora za mahindi tupeane riport,natengemea kuingia field muda SI mrefu.

 
Panda mbegu kulingana na eneo na hali ya hewa husika. Jaribu kuuliza wenyeji ni mbegu gani inakubali kabla ya kupanda.
Sawa mkuu, kwa maelezo niliopewa na afisa kilimo wao ni kwamba Kila mbegu inafanya vizuri kulingana na eneo au ukanda husika.hilo Halima shaka mkuu.
 
Umepima udongo ukajua mahitaji ya aina ya Mbolea?

Harafu hapo ni kilimo cha umwagiliaji hakina magonjwa mengi sasa wew jichanganye masika uone moto.
Acha kumtisha kamanda! Kupanga ni kuchagua.. Dekalb(DK) ni miongoni mwa mbegu bora sana kwa sasa! Iwe kwa Kumwagilia au Mvua za Msimu! Mkuu kama ukanda uliopo mvua ni za kutosha basi panda DK 777 nzuri sanaa! Utani shukuru baadae.
 
Acha kumtisha kamanda! Kupanga ni kuchagua.. Dekalb(DK) ni miongoni mwa mbegu bora sana kwa sasa! Iwe kwa Kumwagilia au Mvua za Msimu! Mkuu kama ukanda uliopo mvua ni za kutosha basi panda DK 777 nzuri sanaa! Utani shukuru baadae
Changamoto ya hii mbegu mahindi yake Yana punje ndogondogo ukilinganisha na mbegu nyingine
 
ila mkuu hiyo mbegu mwaka wa pili huezi iludia ..
 
Sababu za kukosa ni mbegu walizotumia hao

Sababu za kukosa ni mbegu walizotumia hao wenzako ?
Wanajamvi Mimi kwa uzoefu wangu yangu nianze kulima mahindi mwaka 2018 mkoa wa manyara, nmekuwa nkilima dk89 hii hubeba watoto waeili had watatu, huhtaj mvua ya kutosha, kwa upande wa dk31 inabeba wawl au mmoja punje zake nyeupe na kubwa za kuvutia machon! Mbegu hii inaiva mapema ht km mvua haztosh unauhakka wa kuvuna! Nmefka mkoa wa ruvuma nmekuta mbegu zngne tofaut! Hitimisho mbegu znategemeana na kampun gan imewah kufka eneo huska na kuteka soko hvyo wakulima kujenga Iman kuhusu mbegu hzo! Karbun songea, mashamba meng na mvua Ni uhakka! 0785629498
 
Nipo Songea tangia ،2006
 
DEKALB ni miongoni mwa mbegu bora za mahindi.
Zinazaa vizuri, wakati mwingine zaidi ya hindi moja kwa shina.
Inavumilia kwa kiwango kikubwa upungufu wa mvua na mahindi yake matamu.
Utamu wa mahindi haya hufanya ndege kuyapenda pia yanapoanza kuzaa.

Aidha, ni vema kufuata ushauri ili kujua ni DK namba ngapi inafaa kulingana na ukanda unapotaka kuzalishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…