Mbeya: Abiria washushwa kwenye mabasi na kurudishiwa nauli zao kisa mabasi kubeba abiria kuzidi uwezo

Mbeya: Abiria washushwa kwenye mabasi na kurudishiwa nauli zao kisa mabasi kubeba abiria kuzidi uwezo

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Zaidi ya abiria 20 wameshushwa na kisha kurudishiwa nauli zao kutoka kwenye mabasi mawili tofauti yanayofanya safari ya masafa marefu kupitia mkoani Mbeya baada ya mabasi hayo kukaguliwa na kubainika yamezidisha abiria kinyume cha sheria.

Abiria hao wameshushwa baada ya kikosi cha usalama barabarani kikiongozwa na Mkuu wa Kikosi hicho CP Notker Kilewa, kwa kushirikiana na kamati ya usalama mkoa kufanya ukaguzi na kukuta mabasi yaliyotokea mkoani Rukwa kuelekea Dar es Salaam yakiwa yamezidisha abiria na kuagiza kushushwa na pia warejeshewe nauli zao.

 
Back
Top Bottom