Mbeya: Ajifungia kwenye nyumba yeye na mkewe kisha kuchoma nyumba moto, kisa wivu wa mapenzi

Mbeya: Ajifungia kwenye nyumba yeye na mkewe kisha kuchoma nyumba moto, kisa wivu wa mapenzi

Eee mnaishi mitaa tofauti mnaonana mara moja ila msichokane
Inahitajika semina ya mahusiano ili kunusuru uhai,watu wakishindwana waachane tu
Tatizo sio ndoa, tatizo ni kwamba Africa bado hatupo updated. Leo hii wanaondoa wanaweza kuwa wamechokana, kufikia stage ambayo marriage can't work no more, ila Jamii italazimisha wasameheane.

Mkiwafosi sana, ndio yanaenda kuwa haya.
 
View attachment 2549166
Mtoto wa marehemu akiwa Hospitalini akiendelea na matibabu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya

View attachment 2549166
Mtoto wa marehemu akiwa Hospitalini akiendelea na matibabu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na operesheni, misako na doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Aidha tumeendelea kupata mafanikio kwa kukamata watuhumiwa wa makosa mbalimbali na kuwafikisha mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin E. Kuzaga amesema Mnamo tarehe 08.03.2023 majira ya saa 04:00 usiku huko maeneo ya Nyigamba, Mtaa wa Itezi, Jijini Mbeya, mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la HAMIS PIUS [41] Dereva, Mkazi wa Nyigamba alifariki dunia kwa kuungua moto baada ya kujifungia ndani ya chumba anacholala na mke wake aitwaye REBELIA MAKOSO [38] Mkazi wa Nyigamba kisha kumwaga mafuta ya Petroli na kuwasha moto.

Wakati wa tukio hilo, mke wa marehemu alipiga kelele kuomba msaada kwa mtoto wake aitwaye MKESHILISI HAMIS [21] ambaye alikuwa chumba kingine ambaye alikwenda kutoa msaada kwa kupiga teke mlango wa chumba na kisha kumuokoa mama yake lakini baba yake alikataa kutoka ndani na kupelekea kuungua hadi kupoteza maisha.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi. Majeruhi ambao ni mke na mtoto wa marehemu wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi kutokana na majeraha ya moto waliyoyapata mwilini.
View attachment 2549167
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin E. Kuzaga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi. Aidha tunatoa wito kwa jamii kutatua migogoro yao ya kifamilia na ndoa kwa kukaa meza moja ya usuluhishi badala ya kuchukua maamuzi magumu kama hayo.
Asijekuwa bujibuji maana huko ndo kwao. Huyo mwanaume anatuabisha si angetafuta mwanamke mwingine kimya kimya
 
Nyie wanaume mnaofanya ngono na wake za watu mnaona raha gani kuharibu maisha ya wengine. Ona SAsa jamaa kajiua utabeba laana yake
 
Back
Top Bottom