Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Habari waungwana,Kuna hawa Askari wa kikosi Cha usalama Barabarani mkoa wa Mbeya wamezidi kuchukua Rushwa.
Muda huu Niko safarini kutoka Mbeya kuelekea mkoa wa Songwe tumekutana na Askari maeneo ya Ifisi na Songwe viwandani wao kazi Yao ni kuchukua Rushwa tu.
Wanasimamisha Magari lakini hakuna ukaguzi wowote wanaoufanya badala yake wanazunguka nyuma ya gari kisha konda anawafuata na kuwapa pesa.
Hivi hii ndiyo kazi inayowafanya kukaa Barabarani kuchukua Rushwa au lengo ni kuimarisha usalama?
Gari zimezidisha abiria,lakini wao hilo hawalioni,wenyewe ni kukusanya pesa tu.
Na hii njia Leo ina Askari wakike tu .
Jeahi la Polisi waambieni Askari wenu kuwa wanatakiwa kuwa waadilifu na siyo kama hivi wanavyofanya.
Wanatakiwa kukagua magari na siyo kuchukua Rushwa tu.
Na ninyi madereva na makondakta ndiyo mnawaendekeza hawa Askari Kwa kuwapa pesa,haiwezekani umesimamishwa tu unakumbilia kutoa pesa wakati haujakaguliwa wala hauna kosa.
Ndiyo maana ajali zimekuwa nyingi sana hivi Sasa na hii nikutokana na baadhi ya watu wakiwemo Askari wa kikosi Cha usalama Barabarani kushindwa kufanya kazi zao Kwa waledi.