Mbeya: Auawa kwa kupigwa Risasi kisa kudai ushuru wa maegesho wa shilingi 7,500

Duh.kama hayo in ya kweli wananchi walitakiwa wampe kipigo cha kutosha
 
👍
 
Parking system bado ina mapungufu sana,na watu wataendelea kulumbana hadi kuuwana, Kama machine ya parking inaweza peleka taarifa za deni la parking kwa office yao,at the same time inatakiwa na taarifa hizo na mteja zimfikie saa hiyo hiyo,ili na yeye awe na taarifa za deni lake analo daiwa!!
 
UNANIJUA MIMI NANI?........ hizi zimerudi awamu hii.

KWA SASA FEDHA INA ONGEA, JAMAA NATASHIKILIWA KWA MIEZI 3 HIVI.
WATU MTASAHAU,
MASHTAKA YATABADIRIKA,
MWISHO ANARUDI MTAANI KAMA KAWAIDA.
 
Hahahaaa hapo ww n wivu na wenye vicenti tu.ndio hoja kuu kwako.
Marehemu pumzika kwa amani.
Na roho yako mungu aiweke panapo stahili.
 
Jamaa namfahamu anaitwa John mikindo white hv
 


JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemkamata mchimbaji na mnunuzi wa madini, Ezekiel Luhwesha (31) akituhumiwa kumuua wakala wa maegesho ya magari jijini Mbeya, William Mgaya (58).

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga alisema Luhwesha ambaye ni mkazi wa wilayani Chunya mkoani Mbeya, anatuhumiwa kumuua Mgaya Novemba 26 saa 4:30 asubuhi katika eneo la Mafiati kata ya Ruanda kwenye ofisi za Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) jijini humo.

Kamanda Kuzaga alisema jana kuwa siku ya tukio, Mgaya na mwezake Almasi Shaban (32) wote wakala wa maegesho ya magari, wakiwa katika kazi yao ya kukusanya ushuru walimkamata Ezekiel baada ya kuscan namba ya gari lake T 772 DVY Toyota Hilux.

Ilidaiwa kuwa gari lilikuwa likidaiwa Sh 7,500 na mtuhumiwa alitakiwa kulipa deni hilo lakini alihitaji kuhakiki deni hilo hivyo waliongozana hadi ofisi za Tarura.

“Baada ya kuoneshwa taarifa katika mfumo, mtuhumiwa aliliridhika na kuahidi kulipa deni hilo, lakini wakala Willium Mgaya alimtaka kulipa deni hilo papo kwa hapo kwa sababu deni hilo ni la muda mrefu na ndipo yalitokea majibizano yasiyo rafiki kati yao na kupelekea mtuhumiwa kutoa pisto yake na kumfyatulia risasi kifuani Willium Mgaya na kupoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu,”alisema Kamanda Kuzaga.

Alisema mtuhumiwa yupo polisi na silaha yake aina ya bastola yenye namba T.0620-19J0037 ikiwa na risasi tisa ndani ya magazini inashikiliwa.
Kamanda Kuzaga alihimiza wamiliki wa silaha za moto wazingatie masharti ya umilikishwaji kama walivyoomba na wasizitumie tofauti na masharti yalivyoeleza ikiwa ni pamoja kujichukulia sheria mkononi.

Chanzo. millardayo
 
Sheria zilitungwa kwa watu wanyonge tu. Ndiyo maana viongozi wanawapenda sana watu wanyonge.
Huyu jamaa atatoka ndiyo maana hata alipompiga risasi mtu alikuwa ana uhakika 100% atatoka.
Money talks
Sasa Viongozi wakiamua kujinufaisha kwenye hili kosa,Sasa itakuwaje na familia ya Muhangaa!!??
 
Sasa Viongozi wakiamua kujinufaisha kwenye hili kosa,Sasa itakuwaje na familia ya Muhangaa!!??
Nina ushahidi wa hili. Jirani yetu aliua ila alitoa ng'ombe 70 akatoka.
Unamkumbuka yul mkuu wa mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri?
Wanaofungwa ni wale ambao hawana hela. Kuhusu familia ya marehemu huwa wanamsemo wao. "Watajijua wenyewe"
 
Baada ya miaka 2 utasikia yuko nje hana kosa
Mkuu unayosema yapo, ila cha kumuomba Mungu kila siku kukuepusha nacho ni aina hii ya makosa, mauaji.

Kuna rushwa sote tunajua, lakini kesi za mauaji Tz zinafuatiliwa kwa karibu sana na zinasumbua.

Ukipatwa na huu mkasa wa kesi ya namna hii,usipokuwa na utulivu waweza kufirisika mapema ukakosa hata pesa ya kuajiri wakilii kabla hata kesi haijaanza kutajwa, kwa sababu kila mtu atajifanya ni mhusika wa kukusaidia, ni wapigaji tu wakikuona una mtero!

Fanya vituko vyote lakini kuuwa mtu kwa bahati mbaya ama makusudi, usiombee.

Hii ni kwa namna utakavyohangaika nayo na saa zingine kupoteza uelekeo wa maisha yako forever!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…