KERO Mbeya: Baadhi ya Mitaa ya Jiji la Mbeya ni michafu, tunakaribisha Milipuko ya Magonjwa

KERO Mbeya: Baadhi ya Mitaa ya Jiji la Mbeya ni michafu, tunakaribisha Milipuko ya Magonjwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Leo katika pitapita zangu kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya nimejionea namna ambavyo Jiji hili lilivyo chafu.

Viroba vya takataka vimerundikwa kila mahali katika mitaa ya Jiji hili.

Wenye mamlaka ya kukusanya taka nao ni kama hawaoni namna ambavyo Jiji limetapakaa uchafu.

Pichani ni mfano tu wa hali ilivyo, hapa ni Mitaa ya Kabwe ambapo ni katikati ya Jiji. Hii sio sawa hata kidogo.

Pia soma: DOKEZO - Mbeya: Wafanyakazi wa Dampo la Nsalaga wageuka wafanyabiashara wa bidhaa zinazotupwa hapo

Tunaelekea kipindi cha masika chondechonde ndugu zangu wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya oneni hili la sivyo tutapata magonjwa ya mlipuko.

Mtumie Tulia mwambie ni mojawapo ya majukumu yake kuhakikisha jimbo lake linakuwa safi
 
Sio jiji Tu hata watu wa mbeya kiasili ni wachafu, kujenga wamejenga hovyohovyo bila mpangilio, Kilimanjaro hadi mabibi vijijini husafisha mazingira kuzunguka nyumba kila asubuhi na kupanda Maua na bustani nzuri mbeya Hilo halipo , wako rafu hata mitaa yao haijapangika kwa barabara kama hata makambako, mbinga, babati, kahama, ifakara , mbeya wanajua kujirundika kama viroba vya takataka sehemu moja , msiba unatokea inabidi aombe kwa jirani,
Kipindupindu tayari
 
Back
Top Bottom