ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
My Take
Kila siku hapa Tanzania Kuna ajari inatokea inayoua watu na chanzo mara zote ni uzembe wa madereva.
Swali,Je Serikali mumeshibdwa kuja na Sheria Kali za kuwadhibiti Hawa Madereva wanasababisha ajali Kwa uzembe?
---
Ni kwamba tarehe 03.09.2024 majira ya saa 1:10 jioni huko Kijiji cha Itamboleo, Kata na Tarafa ya Chimala, Wilaya ya Mbarali katika barabara kuu ya Mbeya - Njombe, Gari iliyokuwa ikiendeshwa na Mwidunda, mkazi wa ubaruku iliacha njia kisha kugonga gema, kuanguka na kusababisha vifo kwa watu tisa (09) kati yao wanaume 06 kati yao watoto 02, wanawake 03 ambao wote kwa sasa bado kutambulika.
Aidha, katika tukio hilo watu 18 walijeruhiwa kati yao wanaume 05, wanawake 13 na watoto 02 wa kiume na wa kike. chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi hilo kushindwa kulimudu gari hilo kwenye kona kali na kupelekea kuacha barabara, kutumbukia korongoni na kugonga gema. Dereva wa Basi hilo anaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Misheni Chimala akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya misheni Chimala na majeruhi wanapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine Hospitali ya Misheni Chimala.
Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Imetolewa na:
Benjamin E. Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Soma Pia: Polisi Mbeya wamshikilia Dereva wa Lori kwa kusababisha ajali
R.I.P ndugu 😭😭😭😭