Mbeya: Basi la Kampuni ya Shari lapata ajali Mbarali, Watu 9 wapoteza maisha, Polisi wamshikilia Dereva

Mbeya: Basi la Kampuni ya Shari lapata ajali Mbarali, Watu 9 wapoteza maisha, Polisi wamshikilia Dereva

Barabara ya mbarali to Mbeya town ni mbaya mno hata ukiwa unaendesha gari binafsi inakuhamisha
 

My Take
Kila siku hapa Tanzania Kuna ajari inatokea inayoua watu na chanzo mara zote ni uzembe wa madereva.

Swali,Je Serikali mumeshibdwa kuja na Sheria Kali za kuwadhibiti Hawa Madereva wanasababisha ajali Kwa uzembe?
---
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva Alfredy Baharia maarufu kama Mwidunda (50) mkazi wa Ubaruku wilayani Mbarali aliyekuwa akiendesha Gari namba T.896 DHK aina ya Yutong basi la abiria mali ya kampuni ya Shari line lililokuwa likitokea Sumbawanga kuelekea Ubaruku Wilaya ya Mbarali.

Ni kwamba tarehe 03.09.2024 majira ya saa 1:10 jioni huko Kijiji cha Itamboleo, Kata na Tarafa ya Chimala, Wilaya ya Mbarali katika barabara kuu ya Mbeya - Njombe, Gari iliyokuwa ikiendeshwa na Mwidunda, mkazi wa ubaruku iliacha njia kisha kugonga gema, kuanguka na kusababisha vifo kwa watu tisa (09) kati yao wanaume 06 kati yao watoto 02, wanawake 03 ambao wote kwa sasa bado kutambulika.

Aidha, katika tukio hilo watu 18 walijeruhiwa kati yao wanaume 05, wanawake 13 na watoto 02 wa kiume na wa kike. chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa basi hilo kushindwa kulimudu gari hilo kwenye kona kali na kupelekea kuacha barabara, kutumbukia korongoni na kugonga gema. Dereva wa Basi hilo anaendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Misheni Chimala akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya misheni Chimala na majeruhi wanapatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wengine Hospitali ya Misheni Chimala.

Jeshi la Polisi linaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa makini na kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.

Imetolewa na:
Benjamin E. Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Soma Pia: Polisi Mbeya wamshikilia Dereva wa Lori kwa kusababisha ajali
Nashauri serikali iweke sheria ya kwamba kuwe na vigezo maalumu vya kila dereva wa mabasi makubwa, ikiwemo uzoefu na historia ya kutosababisha ajali. Trafiki wa barabarani asikague tu leseni pekee, pamona na hali ya gari bali pia wasifu (CV) ya kila dereva wa basi kubwa. Tunaeza anza na madereva wa kampuni za mabasi na maarufu kisha tukashuka mpaka ngazi za chini. Hii inaeza saidia kupunguza uzembe na ajali.
 
Ajali ni Moja ya vyanzo vya vifo Tanzania sawa TU na malaria
 
Back
Top Bottom