Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
CCM C imejirusha huko baada ya ushindi wao wa kiti 1.
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Mkoa wa Mbeya na Wananchi wa mtaa wa Soko kata ya Ruanda jijini Mbeya wamefanya sherehe ya kumpongeza mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma Brian Mwakalukwa akiwa ni mshindi pekee wa nafasi hiyo kati ya mitaa 181 jijini Mbeya.
Kupata taarifa na matukio kuhusu uchaguzi serikali za mitaa ingia hapa: LGE2024 - Dar es Salaam: Matukio yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
Akizungumza baada ya sherehe hiyo Mwenyekiti wa mtaa wa Soko, Mwakalukwa amesema kwake ni furaha kupata ushindi kupitia chama ambacho watu wengi hawakudhani kama kingepata ushindi huku akiwaomba wananchi kushirikiana ili kuleta maendeleo katika mtaa huo na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wao wanachama wa vyama vingine wamesema ni wakati wa kuunga mkono juhudi za mwenyekiti huyo kwani wanafahamu uchapakazi wa kiongozi huyo.
PIA SOMA
- LGE2024 - CHAUMA yapata ushindi wa kiti 1 kati ya viti 181 Mbeya na kuwa chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi mkoani humo