Mbeya City sasa wanaishi kwa matumaini

Mbeya City sasa wanaishi kwa matumaini

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319

KOCHA wa Mbeya City, Juma Mwambusi alimaliza mkataba wake wa kuifundisha timu hiyo lakini kumekuwepo na siri kubwa juu ya hatima yake ndani ya kikosi hicho ingawa viongozi wa timu hiyo wanadai kuwa bado ni mwajiriwa wao.

Leo Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe alishindwa kutoa ufafanuzi wa hatima ya Mwambusi huku akisistiza kuwa makubaliano ya mkataba mpya ni siri yao na kocha huyo ingawa taarifa za ndani kutoka City zimeeleza kuwa bado hawajafikia makubaliano ya mkataba mpya.

Mbali ya hilo, Kimbe alisema kuwa hawana presha na Ligi Kuu msimu ujao kwani wanaamini kikosi chao kipo vizuri na usajii wanaufanya unazingatia mahitaji ya timu na mapendekezo ya benchi la ufundi huku akisistiza kuwa kuondoka kwa nyota wao si tatizo ndani ya City.

"Mwambusi bado ni kocha wetu, atumie mkataba wa zamani au mpya hilo ni siri yetu baina ya pande mbili, mwajiri na mwajiriwa, kasi ndani ya timu haijapungua na tutawashangaza mashabiki wa soka msimu ujao, watarajie kuona majina ambayo ni mageni lakini kazi yao ni kubwa.

"Tangu msimu umalizike hatujaondokewa na wachezaji wengi, na haitupi shida kwani tunasajili wengine ambao pia ni bora na wanafaa kuichezea timu yetu, wapo pia wachezaji kutoka timu ya vijana tutawapandisha," alisema Kimbe.

Ingawa Kimbe anasema timu yao imeondokewa na wachezaji wachache lakini mpaka sasa BOIPLUS inafahamu kuwa wachezaji zaidi ya 10 wametimka ambao ni Deus Kaseke, Peter Mwalyanzi, Peter Mapunda, Paul Nonga, Saady Kipanga, Anthony Matogolo, Cosmas Fredy, Ramadhan Abdul, Idrisa Rashid, Deo Julius, David Burhan na Lambon Ashery.

Chanzo: BoiPlus Blog

10906246_612237655589282_1427524500915532943_n.jpg

Na wachezaji wengi walioondoka walikuwa kikosi cha kwanza
 
Na wachezaji wengi walioondoka walikuwa kikosi cha kwanza

Labda wana plan B, maana hata misim iliyopita waliibua watu kutoka kusikojulikana, akina Saad Kipanga na Hamadi Kibopile ambao walikuwa hawana nafasi kikosi cha Kwanza.
 
ngoja washuke daraja msimu ujao hao

Mimi sitamani washuke daraja, kwani kutatoa upenyo kwa timu za majeshi kuongezeka kwenye ligi wakati hazina mvuto.
 
Mimi sitamani washuke daraja, kwani kutatoa upenyo kwa timu za majeshi kuongezeka kwenye ligi wakati hazina mvuto.

umeongea point sana. ila wamejipanga vipi ili wasishuke daraja?
 
umeongea point sana. ila wamejipanga vipi ili wasishuke daraja?

Wanajipanga kusema ukweli, ila ndani ya timu hizi ndogo kuna hujuma nyingi sana mkuu.

Angalia jitihada za Mbeya City nje na ndani ya uwanja, ni timu ambayo licha ya kupatwa na misukosuko msimu uliopita, haijatimua kocha wala kupaniki. Chunguza wanavyoweka kambi ya timu kimkakati na sio kwa sifa, chunguza usajili na nidhamu ya timu kwa ujumla utagundua kitu cha ziada.

Nje ya uwanja ni timu ambayo inajimarisha kiuchumi kila mwaka, wametafuta mikataba na makampuni kadhaa na juzi kati Washabiki wameanzisha kampuni yao ambayo itapewa tenda fulani fulani za timu kama kuuza bidhaa na kadhalika.

Huoni kama wanajitahidi mkuu?
 
mbeya city wanajitahidi kweli sema mpira wa kibongo hujuma sana hasa kwa timu zinazoonesha ushindani sana.ila pia viongozi wa mbeya city naona wajipange sana wasirubuniwe kirahisi
 
mbeya city wanajitahidi kweli sema mpira wa kibongo hujuma sana hasa kwa timu zinazoonesha ushindani sana.ila pia viongozi wa mbeya city naona wajipange sana wasirubuniwe kirahisi

Hapo walipo wamevuka viunzi vingi sana vya hujuma.

Angalia TFF walitaka waingine timu tatu Kombe la Kagame, lakini chaguo lao likawa Simba badala ya City ili mashindano yanoge. Sasa kama taasisi inayosimamia soka inaweza kufanya upuuzi kama huu, huko chini chini inakuwaje?
 
tff ndo inaharibu mpira wetu. mbeya city ilichaguliwa ila wao walitaka kuforce simba ishiriki. soka la bongo mpaka liendelee inabidi tuweke siasa pembeni
 
Back
Top Bottom