Mbeya: Emmanuel Patson Mwesa, akamatwa kwa kumuua bosi wake kwa panga

Mbeya: Emmanuel Patson Mwesa, akamatwa kwa kumuua bosi wake kwa panga

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Songwe lilifanya msako huko Kijiji cha Mwaka - Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, Machi 21, 2022 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa EMMANUEL PATSON MWESA [22] Mkazi wa Mwaka - Tunduma aliyekuwa akitafutwa kwa kosa la mauaji ya bosi wake.

Bosi huyo ambaye amefahamika kwa jina la ASUMWISYE LUFINGO @ MWAMBONIKE [37] Mkazi wa Isangawana tukio lililotokea mnamo tarehe 02.01.2022 wakiwa shambani.

“Ni kwamba mnamo 02.01.2022 majira ya saa 16:00 mchana huko Kijiji cha Isangawana, Kata ya Matwiga, Tarafa ya Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, ASUMWISYE LUFINGO @ MWAMBONIKE [37] akiwa shambani na wafanyakazi wake mtuhumiwa EMMANUEL PATSON MWESA [22] na mwenzake aliuawa kwa kukatwa panga kichwani. Chanzo cha tukio ni madai ya fedha ya ujira ya kulima shamba.

Aidha, katika tukio hilo, watuhumiwa waliondoka na pikipiki ya marehemu yenye namba za usajili MC.776 BES aina ya Fekon.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilianza msako na hatimaye kumkamata mtuhumiwa huko mkoani Songwe.

Aidha, Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa mwingine ambaye walishirikiana katika tukio hili. Mahojiano na mtuhumiwa yanaendelea ili kubaini ilipo pikipiki ya marehemu waliyoondoka nayo mara baada ya kufanya tukio hilo.
 
Back
Top Bottom