Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Uzuri wa Mwanza serikali haipo huko hivyo majengo mengi makubwa yanajengwa na watu au taasisi binafsi.
Kuna sehemu wameanza shindana na Dar kisa tu Serikali inajenga kule Wizara zaidi ya 26 na Taasisi 400 zinajenga.
 
Ukitaka kijua kuwa swala la mipangilio siyo moja ya utaratibu na tamaduni zetu , wewe nenda hata kaangalie sehemu au maeneo tunayowazika wapendwa wetu waliotutangulia ??.. jibu utakaro lipata kule basi ndiyo linalotoa picha halisi ya jinsi tulivyo..
Kuna makaburi pale Redcross Posta yamepangiliwa vizuri sana kama Marekani.

Sisi hadi makaburi tumeshindwa yapangilia vizrluri
 
Tatizo la mipango miji inaanza kwa Serikali za Mitaa kuchagua watu wasio na uwezo hapo ndo tatizo linaanzia.

Wale ndo walipaswa wazuie ujenzi holela au kuuziana viwanja kiholela.
 
Tatizo ni siasa, serikali uwezo inao ila wakifanya hivyo inakuwa mtaji wa kisiasa
 
Hiyo Dar inayonuka ni Dar ipi?

Mi najua Mbeya yanuka Nguruwe
 
Kumbe Mbeya pa hovyo. Bora nibaki Butiama. Asante kwa kutusanua, kumbe mheshimiwa spika anaishi kijijini.

Karibuni Butiama. New Jersey ya Tanzania.
 
Japo mbeya ni nyumbani ila nalaumu sana uongozi kwa kukosa maono. Mbeya ni jiji lenye border 2, ji jiji lenye kila aina ya fursa...

Jiji hawana mpango mkakati na master plan nzuri. Mbeya kwa ujumla watu wengi wana kipato kizuri kuliko hata dodoma, wanaweza kujenga nyumba za kisasa ila tu mji ndio haujapimwa.

Hakuna sehemu za kupumzika, barabara za lami ni mbovu na chache sana.

Wanapaswa kupima maeneo mengi sana ili tuendako tusirudie makosa...
 
Mbeya sio jiji, haina hadhi hata ya manispaa ukiacha eneo kubwaa na idadi ya watu
 
Umeongea points tupu bila kuacha kitu! Mbeya haitakiwi kuitwa jiji hata siku moja, bora hata Iringa mara kumi! Mbeya ni mji wa hovyo bila kuonea aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…