Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Hivi wewe kwenu ni wapi ulinganishe na Mwanza? watu wameshakwambia Mbeya ilikuwaje ikawa jiji hauwelewi. Mwanza imepimwa CBD yote, Nyegezi yote, Buswelu yote, Nyamongolo yote, Igoma yote, Ghana yote, Nyamanoro yote Nyakato yote! hivi haunaga aibu kulinganisha Mwanza na vimiji vyako hivyo?.Mwanza ile inayojengwa daraja refu nchini km 3.2,daraja la juu la sgr (Viaduct)km 1.4,soko kubwa pale City Center, stend 2 za maana, meli kubwa kuliko yoyote nchi hii.Tuwe wakweli tu Mbeya bado sana kwa Mwanza tuache chuki za kijinga hazitusaidii nchi hii ni yetu sote hata Mwanza ni kwetu wote wa Tanzania. All in all Mwanza is most developed City by everything after Dar es Salaam.

Sent from my D6503 using JamiiForums mobile app
Uzuri wa Mwanza serikali haipo huko hivyo majengo mengi makubwa yanajengwa na watu au taasisi binafsi.
Kuna sehemu wameanza shindana na Dar kisa tu Serikali inajenga kule Wizara zaidi ya 26 na Taasisi 400 zinajenga.
 
Ukitaka kijua kuwa swala la mipangilio siyo moja ya utaratibu na tamaduni zetu , wewe nenda hata kaangalie sehemu au maeneo tunayowazika wapendwa wetu waliotutangulia ??.. jibu utakaro lipata kule basi ndiyo linalotoa picha halisi ya jinsi tulivyo..
Kuna makaburi pale Redcross Posta yamepangiliwa vizuri sana kama Marekani.

Sisi hadi makaburi tumeshindwa yapangilia vizrluri
 
Ni kweli, inareflect . Nadhani pia tuna watu wasio sahihi kwenye sehemu za kufanya maamuzi. Watu sahihi na wenye mawazo mazuri wapo na hata wakipata nafasi ya kuwa viongozi wanaishia kupigwa vita kama sio kupotezwa kabisa . Mfumo wetu unaruhusu machizi wengi kuwa viongozi. Ndio maana unaona sekta binafsi wanatoboa mambo yao, mipango yao kwa unahisi sababu nafasi kubwa huko zinatolewa based on Merit,
Mtu kama hana uwezo hawezi kuwa mkurugenzi wa Vodacom au CRDB, hawezi toboa.
Ila inawezekana kabisa mtu akawa tu na kadi ya chama ikawa ni kigezo ukaqualify kuteuliwa kuwa mkurugenzi hata wa Air Tanzania au TTCL au Bank ya Posta . Such awkward system.
Tatizo la mipango miji inaanza kwa Serikali za Mitaa kuchagua watu wasio na uwezo hapo ndo tatizo linaanzia.

Wale ndo walipaswa wazuie ujenzi holela au kuuziana viwanja kiholela.
 
Nani wa kulaumiwa?. Mi nimezaliwa na kukulia mbeya. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 maeneo mengi yalikua wazi na nchi ina wataalamu wa mipango miji lakini walizubaa tuu mpaka watu wakajenga hovyo na sasa maeneo ya wazi ni machache hata kujenga shule inashindikana.

Eneo lilipokua Soko la uhindini NHC walikua wameandaa fungu kabisa kupafanya pa kisasa ila madiwani na wafanyabiashara waliokuwepo mwanzo wakafanya fitna mpaka leo pako vilevile tuu. City park pamedorora mpaka wamempa mtu ajenge frame.

Mipango mibaya ya Mbeya serikali inahusika kwa asilimia kubwa, huwezi kuwaachia watu wajenge wanavyojiskia.
Tatizo ni siasa, serikali uwezo inao ila wakifanya hivyo inakuwa mtaji wa kisiasa
 
Ulipoitaja Mbalizi kuwa ipo Mbeya jiji nikajua wewe mgeni Mbeya. Kusoma Mbeya haimaanishi unaijua Mbeya.
Ni kweli Mbeya vumbi lipo lkn hainuki kama Dar, ni kweli Mbeya Kuna nyumba za tope lkn hakuna ujenzi wa kujenga chini ya mawe na kuhatarisha maisha ya wakazi kama Mwanza.
Hiyo Dar inayonuka ni Dar ipi?

Mi najua Mbeya yanuka Nguruwe
 
Kumbe Mbeya pa hovyo. Bora nibaki Butiama. Asante kwa kutusanua, kumbe mheshimiwa spika anaishi kijijini.

Karibuni Butiama. New Jersey ya Tanzania.
 
Japo mbeya ni nyumbani ila nalaumu sana uongozi kwa kukosa maono. Mbeya ni jiji lenye border 2, ji jiji lenye kila aina ya fursa...

Jiji hawana mpango mkakati na master plan nzuri. Mbeya kwa ujumla watu wengi wana kipato kizuri kuliko hata dodoma, wanaweza kujenga nyumba za kisasa ila tu mji ndio haujapimwa.

Hakuna sehemu za kupumzika, barabara za lami ni mbovu na chache sana.

Wanapaswa kupima maeneo mengi sana ili tuendako tusirudie makosa...
 
Mbeya sio jiji, haina hadhi hata ya manispaa ukiacha eneo kubwaa na idadi ya watu
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla in typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.


Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)


Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

Umeongea points tupu bila kuacha kitu! Mbeya haitakiwi kuitwa jiji hata siku moja, bora hata Iringa mara kumi! Mbeya ni mji wa hovyo bila kuonea aibu!
 
Back
Top Bottom