Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Jibu swali,Ili iwe Jiji inatakiwa iwaje? Bado sana ndio nini labda? Ndio Jiji Sasa unatakaje?
labda jiji liwe kwajili ya kilimo kutupia magorofa yakina lutimo mwashala (mkulu) ndio kuendelea mbeya kunauhaba wa barabara ukitaka kufika uyole,mbalizi ilakulazimu kupita barabara kuu
 
labda jiji liwe kwajili ya kilimo kutupia magorofa yakina lutimo mwashala (mkulu) ndio kuendelea mbeya kunauhaba wa barabara ukitaka kufika uyole,mbalizi ilakulazimu kupita barabara kuu
Ndio pattern ya Jiji na upekee wa Mbeya,unataka Mbeya iwe Dar au Dom?

By the way Barabara za Mitaa zinazidi kujengwa ambazo Kwa namna Fulani zitapita kando ya Tanzam.

On top of that kuna Uyole-Mbalizi Bypass Iko kwenye pipeline,Iwambi By pass ziko kwenye pipeline na mwisho Tanzam inajengwa.

Wewe unataka maendeleo gani? Huko Mwanza na Arusha Kuna Barabara wapi za maana Hadi upaparike na Vimji uchwara?

Wa kuicheka Mbeya ni Dom na Dar pekee.

Mwisho wewe ulitaka tuweke gorofa za nani? Wewe imejenga Yako tuiweke? πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyo ni hater ambae anasikia sana Raha kukana kwao 😬😬

Kama mnataka Mbeya ifanane na Dom waambieni watu wa Serikali wawekeze Mbeya kama wanavyojenga Mikoa Mingine.
Tunaipenda sana mbeya,ndio mana tunatamani kuiona mbeya ambayo itatuweka kifua mbele na sio utopolo huu uliopo Sasa hivi..Juzi wametia saini mkataba wa ujenzi wa stendi na soko lakini ukiangalia hizo picha za stendi na soko ni za kawaida sana ,why hatupendi kufanya vitu Kwa ukubwa..vitu ambavyo vitakuwa hot Kwa miaka mingi mbele??.Leo hii Mwanza wana stendi mbili zote Kali hata hii ya mbeya inayoenda kujengwa haiwezi kuingia stendi yoyote kati ya hizo mbili,tunakwama wapi?. Na bado tunajiita mkoa Giant..Kuna vimikioa vinakuja nyuma yetu naviona kabisa vitatuacha mbali sana
 
huwa najiuliza aliyesema hili liwe jiji sijui nan
 
Mtaishia kutamani hivyo hivyo ila watu wa Mbeya wanazidi kufanya Yao πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/p/C5Vz205NAGX/?igsh=OHlpMHljNnZ0c3o5
 
πŸ˜‚πŸ˜‚ nipo mbeya ndugu mbeya mji ujapangiliwa tunacho taka mbeya iwe mbeya kweli sio maneno tu,
tunavyanzo vya maji vingi lakini mbeya maji yanasumbua sanaa mfano tu sae itezi nsalaga igawilo,
iyo stand inayojengwa ivi ni stand yakujivunia kama jiji eneo dogo sanaa
 
Mji gani uliopangiliwa Nje ya Dom?

Una ruka ruka mada mbalimbali mara maji mara Barabara,wapi maji hayasumbui? 🀣🀣🀣

Uko Mbeya harafu hujui kinachoendelea ndio maana unaongea pumba πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://youtu.be/wJhMIIHtUjo?si=DHNqNFEptSpkyjHY
 
Ushauri wa member Game over uzingatiwe , Jiji la mbeya na wenye nyumba zilizo karibu na Bara bara kuu njia 4 wa jiandae kuanza kujenga maghorofa toka uyole Hadi mbalizi asiye na uwezo auze plot yake atatute maeneo ya pembezoni ya jiji. Hakuna namna Mbeya nyumba za udongo ziondoke barabarani kama ilivyo kuwa kariakoo miaka ya 70/80. Mashamba ya chuo cha kilimo Uyole yalindwe sana yabakie kwa matumizi ya chuo tu. Hata London kwa Malkia Elizabeth pana mashamba.
 
Mkuu, Mwanzo bajaj hazikuruhusiwa main road na mambo yalikua poa lakini sasa zimeruhusiwa ni vurugu tuu. Kuna routes nyingi sana ambazo hazihusishi main road. Tanzam road ziachiwe daladala pekee. Uwepo wa bajaj hizi πŸ‘‡ route hauna afya
1- kabwe -iyunga
2- kabwe- mjini
3-kabwe- Uyole
Mbeya ni mojawapo ya miji yenye public transport nzuri sana, tusiharibu kwa kuachia vibajaj kila sehemu. Bajaj wataenda ilemi, isanga, veta, airport, isyesye, ituha, mkoani, forest, must, shewa n.k

Ni kweli Kabwe/mwanjelwa/soweto ndio mjini yetu kwa sasa lakini bado halmashauri inatoa vibali ujenzi wa nyumba za kawaida tuu zisizo ghorofa, hii sio nzuri kwa maendeleo. Mafiati nimeona projects kama 2 hivi ya vijumba vya kawaida tuu visivyo na hadhi ya mjini.
 
Bajaji haijawahi kuwa tatizo Wacha ushamba.
 
Jibu swali,Ili iwe Jiji inatakiwa iwaje? Bado sana ndio nini labda? Ndio Jiji Sasa unatakaje?
Hao wengine utoto mwingi sana, hawajui hata Dar ni ndogo sana endapo ukiiringanisha na majiji ya nchi fulani!

Sasa sijui wanataka Mbeya tuiwekeje kwa lazima zao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…