Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Mbeya haina hadhi ya jiji. Mbeya ni Kijiji Kikubwa

Jibu swali,Ili iwe Jiji inatakiwa iwaje? Bado sana ndio nini labda? Ndio Jiji Sasa unatakaje?
labda jiji liwe kwajili ya kilimo kutupia magorofa yakina lutimo mwashala (mkulu) ndio kuendelea mbeya kunauhaba wa barabara ukitaka kufika uyole,mbalizi ilakulazimu kupita barabara kuu
 
labda jiji liwe kwajili ya kilimo kutupia magorofa yakina lutimo mwashala (mkulu) ndio kuendelea mbeya kunauhaba wa barabara ukitaka kufika uyole,mbalizi ilakulazimu kupita barabara kuu
Ndio pattern ya Jiji na upekee wa Mbeya,unataka Mbeya iwe Dar au Dom?

By the way Barabara za Mitaa zinazidi kujengwa ambazo Kwa namna Fulani zitapita kando ya Tanzam.

On top of that kuna Uyole-Mbalizi Bypass Iko kwenye pipeline,Iwambi By pass ziko kwenye pipeline na mwisho Tanzam inajengwa.

Wewe unataka maendeleo gani? Huko Mwanza na Arusha Kuna Barabara wapi za maana Hadi upaparike na Vimji uchwara?

Wa kuicheka Mbeya ni Dom na Dar pekee.

Mwisho wewe ulitaka tuweke gorofa za nani? Wewe imejenga Yako tuiweke? 😂😂
 
Huyo ni hater ambae anasikia sana Raha kukana kwao 😬😬

Kama mnataka Mbeya ifanane na Dom waambieni watu wa Serikali wawekeze Mbeya kama wanavyojenga Mikoa Mingine.
Tunaipenda sana mbeya,ndio mana tunatamani kuiona mbeya ambayo itatuweka kifua mbele na sio utopolo huu uliopo Sasa hivi..Juzi wametia saini mkataba wa ujenzi wa stendi na soko lakini ukiangalia hizo picha za stendi na soko ni za kawaida sana ,why hatupendi kufanya vitu Kwa ukubwa..vitu ambavyo vitakuwa hot Kwa miaka mingi mbele??.Leo hii Mwanza wana stendi mbili zote Kali hata hii ya mbeya inayoenda kujengwa haiwezi kuingia stendi yoyote kati ya hizo mbili,tunakwama wapi?. Na bado tunajiita mkoa Giant..Kuna vimikioa vinakuja nyuma yetu naviona kabisa vitatuacha mbali sana
 
Moja kwa moja kwenye mada;

Wenyewe wanaita green city, hii sio kweli . Jina linatakiwa liwe Dusty City.
Hivi pamoja na Hali ya hewa nzuri kitu gani kinazuia halmashauri ya mji kuwa na mipango ya upandaji wa miti ?

Mji wa Mbeya ni kati ya miji mikubwa (Kwa eneo na idadi ya wakazi) Lakini maisha ya mbeya kwa ujumla ni typical kijijini. No order , hakuna ustaarabu, chaotic , vumbi, makelele , watu wanapita na magari ya matangazo ya kila aina Hadi ya misiba. Hawa NEMC badala ya kudeal na kidimbwi na kitambaa cheupe kwanini huku hamuoni?

Mbeya hakuna usafiri wa Taxi , Bajaji ni nyingi kuliko abiria na hazina route yaani kokote anaenda. Daladala routes ni mbili tu Mjini Mbalizi au Mjini Uyole. Ikifika saa tatu usiku basi wewe daka boda uende uendako.

Mbeya hakuna hadhi wala mwonekano wa jiji, tofauti kabisa na Arusha au Mwanza, Mji mzima hakuna hata sehemu ya kufanya matembezi ? Mbeya nyumba za tope zimetapakaa kuanzia uyole, sae, hadi soweto makunguru hadi nzovwe na iyunga.. huko mbalizi ni balaa lingine.

Inashangaza kuona 2023 katikati ya mji serikali inajenga fremu za kupangisha. That’s so annoying.
Why not some modern Structure like a shopping mall?

Hivi mna uhakika hawa viongozi wa halmashauri ya mji wa Mbeya walienda shule kweli? Miaka kadhaa ya nyuma kulikuwa na Fursa ya kujenga Soko la kisasa au shopping mall pale mwanjelwa jamaa wa huko halmashauri ya mji wakaja na lidude la kizamani (structure nzee ya miaka ya 1700s huko) tena kwa mabilioni ya pesa, baada ya pale SIDO kuungua tukajua watakuja na kitu cha tofauti, wapi. Yaleyale.

Picha: Mwonekano wa juu wa mji wa mbeya.

Fremu za Biashara zinazojengwa na Halmashauri ya jiji la mbeya katikati ya mji (CBD)

Jengo la soko la mwanjelwa lililojengwa kwa gharama kubwa (bilioni 60+) pesa za walipakodi

Eneo la kabwe, hapa jioni hugeuka gulio.. hapa unahitaji tu kuwa na bidhaa..nenda kabwe then mwaga chini uza. Vurugumechi.

Miundombinu ni duni sana, duni mno . Barabara ni moja tu ya TAZAM Highway inayopita mjini ambayo ni chakavu sana na ni moja (Sio Dualed). Mbeya si rafiki wa watembea kwa miguu sababu utagongwa muda wowote kama sio na bajaji basi bodaboda. Hakuna jogging Mbeya.

Kwa upande wa huduma za Afya mbeya pako [emoji817]. Mengine ni hovyo kabisa..

Ushauri:
1. Mradi mpya wa barabara ya njia nne toka uyole hadi Uwanja wa ndege ufanyike njia sita maeneo ya Mjini kupunguza foleni, na pia kuwe na provisions za watembea kwa miguu, pale mafiati kuwe na interchange kurahisisha traffic na angalau tusifikirie kubomoa na kujenga tena kwa miaka 15 ijayo.

2. Zijengwe nyumba za kisasa za makazi sehemu kama airport ya zamani. Pia kile chuo cha kilimo kitoe yale mashamba kwa NHC na zijengwe affordable houses nk. Mashamba hayatakiwa mijini. Nchi ina mapori mengi sana

3. Upandaji wa miti iwe ni kipaumbele. Walau kupunguza lile vumbi mjini. Watoto wa shule za misingi na sekondari can easily do this bila hata gharama.

5. Think Big. Jiji linaweza kuanza kufikiria kuwa na reli nyepesi ya abiria toka uwanja wa ndege wa Songwe hadi Uyole, na kubranch pale Meta ikaenda hadi mjini na kuja kutokea mwanjelwa. Kwa Jografia ya mji wa mbeya reli hii itarahisisha usafiri kwa zaidi ya 80% ya mahitaji ya usafiri wa mjini.

6. Maeneo ya wazi yawepo. Hii in muhimu sana.
NB: Mimi sio mwandishi wa wa habari.

huwa najiuliza aliyesema hili liwe jiji sijui nan
 
Tunaipenda sana mbeya,ndio mana tunatamani kuiona mbeya ambayo itatuweka kifua mbele na sio utopolo huu uliopo Sasa hivi..Juzi wametia saini mkataba wa ujenzi wa stendi na soko lakini ukiangalia hizo picha za stendi na soko ni za kawaida sana ,why hatupendi kufanya vitu Kwa ukubwa..vitu ambavyo vitakuwa hot Kwa miaka mingi mbele??.Leo hii Mwanza wana stendi mbili zote Kali hata hii ya mbeya inayoenda kujengwa haiwezi kuingia stendi yoyote kati ya hizo mbili,tunakwama wapi?. Na bado tunajiita mkoa Giant..Kuna vimikioa vinakuja nyuma yetu naviona kabisa vitatuacha mbali sana
Mtaishia kutamani hivyo hivyo ila watu wa Mbeya wanazidi kufanya Yao 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C5Vz205NAGX/?igsh=OHlpMHljNnZ0c3o5
 
Ndio pattern ya Jiji na upekee wa Mbeya,unataka Mbeya iwe Dar au Dom?

By the way Barabara za Mitaa zinazidi kujengwa ambazo Kwa namna Fulani zitapita kando ya Tanzam.

On top of that kuna Uyole-Mbalizi Bypass Iko kwenye pipeline,Iwambi By pass ziko kwenye pipeline na mwisho Tanzam inajengwa.

Wewe unataka maendeleo gani? Huko Mwanza na Arusha Kuna Barabara wapi za maana Hadi upaparike na Vimji uchwara?

Wa kuicheka Mbeya ni Dom na Dar pekee.

Mwisho wewe ulitaka tuweke gorofa za nani? Wewe imejenga Yako tuiweke? 😂😂
😂😂 nipo mbeya ndugu mbeya mji ujapangiliwa tunacho taka mbeya iwe mbeya kweli sio maneno tu,
tunavyanzo vya maji vingi lakini mbeya maji yanasumbua sanaa mfano tu sae itezi nsalaga igawilo,
iyo stand inayojengwa ivi ni stand yakujivunia kama jiji eneo dogo sanaa
 
Mji gani uliopangiliwa Nje ya Dom?

Una ruka ruka mada mbalimbali mara maji mara Barabara,wapi maji hayasumbui? 🤣🤣🤣

Uko Mbeya harafu hujui kinachoendelea ndio maana unaongea pumba 👇👇

View: https://youtu.be/wJhMIIHtUjo?si=DHNqNFEptSpkyjHY
 
Ushauri wa member Game over uzingatiwe , Jiji la mbeya na wenye nyumba zilizo karibu na Bara bara kuu njia 4 wa jiandae kuanza kujenga maghorofa toka uyole Hadi mbalizi asiye na uwezo auze plot yake atatute maeneo ya pembezoni ya jiji. Hakuna namna Mbeya nyumba za udongo ziondoke barabarani kama ilivyo kuwa kariakoo miaka ya 70/80. Mashamba ya chuo cha kilimo Uyole yalindwe sana yabakie kwa matumizi ya chuo tu. Hata London kwa Malkia Elizabeth pana mashamba.
 
Tangu lini Bajaji zikawa tatizo Mjini? In fact napenda usafiri wa aina mbalimbali badala ya kurundikana kwenye madaladala ,Kila mtu achague anaoupenda.

Pili pattern ya Mbeya ni Linier inategemea Barabara kuu Moja ,so no way kuwa na njia za Nje ya Mji maana kwanza hazipo labda kama zinazojengwa Sasa zitakuwa tofauti.

Mwisho kule Uhindini Kwa Sasa hajufai biashara labda residential apartments,hostels na Ofisi za Umma, biashara zote zimehamia Tanzam Roads.

Mimi naipenda Mbeya
Mkuu, Mwanzo bajaj hazikuruhusiwa main road na mambo yalikua poa lakini sasa zimeruhusiwa ni vurugu tuu. Kuna routes nyingi sana ambazo hazihusishi main road. Tanzam road ziachiwe daladala pekee. Uwepo wa bajaj hizi 👇 route hauna afya
1- kabwe -iyunga
2- kabwe- mjini
3-kabwe- Uyole
Mbeya ni mojawapo ya miji yenye public transport nzuri sana, tusiharibu kwa kuachia vibajaj kila sehemu. Bajaj wataenda ilemi, isanga, veta, airport, isyesye, ituha, mkoani, forest, must, shewa n.k

Ni kweli Kabwe/mwanjelwa/soweto ndio mjini yetu kwa sasa lakini bado halmashauri inatoa vibali ujenzi wa nyumba za kawaida tuu zisizo ghorofa, hii sio nzuri kwa maendeleo. Mafiati nimeona projects kama 2 hivi ya vijumba vya kawaida tuu visivyo na hadhi ya mjini.
 
Bajaji haijawahi kuwa tatizo Wacha ushamba.
 
Back
Top Bottom