Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

Mbeya: Hakimu wa Mahakama ya Wilaya auawa kwa kipigo kutoka kwa Wananchi wenye hasira kali

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, Dk. Vicent Anney amesema watu wawili wameuawa akiwemo hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Handeni, Joachim Mwakyoma baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Novemba 14, 2023, Dk. Anney amesema tukio hilo limetolea katika kijiji cha kibole halmashauri ya Busokelo.

Amesema hakimu huyo alikuwa ameambatana na wenzake wawili kwenda kwenye shamba lenye mgogoro na wanakijiji walishinda kesi katika Mahakamani Kuu Desemba mwaka 2022 baada ya kesi hiyo kusikilizwa mahakamani kwa miaka zaidi ya 10.

Dkt. Anney amesema taarifa za awali zinaeleza kuwa kitendo cha hakimu na wenzake kuingia katika shamba hilo kiliwashtua wananchi waliowafuata na kuwahoji na yakaibuka malumbano.

Amesema katika tukio hilo wananchi wawili walipigwa risasi na mmoja wa watu waliokuwa wameambata na hakimu na walikimbizwa katika hosptali ya Itete kwa matibabu zaidi na hali zao zinaendelea vizuri.

Dkt. Anney marehemu licha ya kuja kijiji hapo kwa ajili ya mapumziko, pia alikuwa kwenye taratibu za kukata rufaa mahakamani kupinga hukumu.

“Kwa sasa tumeliachia Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo kuwasaka watu waliohusika na mauaji. Wilaya hii imekithiri matukio ya mauaji yanayohusiana na migogoro ya ardhi,” amesema.

Akigusia tabia isiyofaa ya wananchi kujichukulia sheria mkononi Dk Anney amesema, "tunaendelea kushughulikia matukio hayo ikiwepo kushirikisha na viongozi wa dini, kamati za amani wilaya kuona wanakemea na kutoa elimu kwa jamii kuachana na tabia ya kuchukia sheria mkononi."

Diwani wa Busokelo ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri, Anyosisye Njobelo amesema, "ndio tukio hilo limetokea kwenye kijiji kilicho katika kata yangu ila kwa sasa mimi sio mzungumzaji tuviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake."

Mmoja wa wananchi wa kata ya Kiwila Wilaya ya Rungwe ambaye aliomba jina lake lisitajwe amesema changamoto kubwa ni mienendo ya kesi za migogoro ya ardhi zinavyoendeshwa kwenye vyombo vya maamuzi.

“Tukisema kwa Tanzania, Rungwe kuna migogoro mingi sana ya ardhi, mauaji lakini tushukuru Mungu ujio wa Mkuu huyu wa Wilaya, Dk. Vincent Anney ameweza kudhibiti kwa wananchi wanaohusika kukamatwa na kuchukuliwa hatua kidogo imesaidia,” amesema.
Hii ikiendelea uonevu wa kupitia kalamu utapungua.
 
dah, kuna watu wakiwa na bastola wanafikiri wamemaliza kila kitu, ona bastola imeshindwa kumsaidia kuokoa uhai wake.

Tuishi kwa busara na adabu nyingi ili tuwe salama kuliko kuamini silaha tulizo nazo.
Polisi wa Tz waione hii
 
JF AKSANTE KAMPUNI YAKE IMERUDI... UTAANZISHA LINI CHAMA, UTAANZISHA LINI BIASHARA, UTANUNUA LINI KIWANJA KILICHOPIMWA, UTAJENGA LINI FLY OVER, UTAJENGA LINI MWENDOKASI, UTAPELEKA LINI SGR KILIMANJARO VYOTE HIVYO UTAVILETA WEWE WELEWA
Duuuh! mkuu mbona hata sielewi unamaanisha nini au umeñiquote kimakosa au labda unanena kwa lugha?
 
Nimekutana na hili andiko kwenye mitandao yetu hii, naamini mamlaka zitatuambia ukweli wa hii kitu....

Anaandika Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh. Siriel Mchembe👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿👇🏿

Niimepokea taarifa kutoka kwa DC Rungwe Dkt. Vincent Anney kwamba alfajiri ya leo, Hakimu Joakim Mwakyolo wa Mahakama ya Wilaya hapa Handeni ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko Busokelo Tukuyu/Rungwe.

Marehemu alikuwa likizo maana huko Rungwe ndipo anapotokea.

Chanzo cha kuuawa ni Mgogoro wa Ardhi kati yake na wanakijiji hicho anachotoka.

Alishindwa kesi ya ardhi Mahakama Kuu dhidi ya kijiji, lakini baada ya muda akaonekana kwenye eneo la Mgogoro akiwa ameongozana na Watu wawili.

Inadaiwa kuwa yeye na watu hao wawili kuna vitu walikuwa wanavichimbia ardhini kwenye eneo hilo la mgogoro jambo ambalo lilitafsiriwa na wanakijiji kwamba ni ushirikina.

Wananchi walipowazonga watatu hao na kuwahoji kuhusu suala hilo, ugomvi ukatokea kati yao, jambo lililopelekea mmoja wa watu waliokuwa na Hakimu huyo kuwapiga risasi wanakijiji wawili miguuni.

Baada ya hapo wananchi wakapandwa hasira na kumshambulia kwa mawe na silaha mbalimbali Hakimu huyo pamoja mmoja wa watu aliokuwa nao, huku mwingine akitoweka kuelekea kusikojulikana.

Hivyo vifo vilivyoripotiwa ni viwili. Hakimu pamoja na mmoja wa watu alikwenda nao kwenye eneo la mgogoro.

Pole sana Mhimili wetu wa Mahakama, hasa Hakimu wa Wilaya Handeni Mhe.Sabuni kwa kuondokewa na mtumishi huyu. Poleni ndugu zangu wa Handeni.

Tuwaombee pumziko la amani - Amina.

===================

TAARIFA RASMI YA MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vincent Anney amesema “Ni tukio la kweli, Hakimu alikuwa na mgogoro na Wanakijiji, yeye si mwananchi wa Rungwe ila alinunua eneo Rungwe.

“Zamani baba yake alikuwa anaishi Rungwe akahamia Kyela, hata yeye Hakimu alizaliwa hukohuko Kyela. Hapo kati alianzisha mgogoro na wananchi akisema anataka eneo la babu yake lakini hiyo ni sehemu nyingine, si sehemu ambayo tukio limetokea.

“Eneo ambalo limesababisha auawe ni kubwa kuna karibia ekari 1000, ni msitu na ni hifadhi ambayo imekuwa ikisadia mvua, alinunua kinyemela, wananchi wakamshtaki Mahakamani.

“Akashindwa kesi, alikuwa katika harakati za kukata rufaa, kesi ikiwa imeisha akaenda shambani akiwa na watu wengine wawili akaanza kuchimbachimba, inasemakana alikuwa anachimba dawa.

“Yakatokea majibizano kati yake na Wananchi waliofika eneo hilo, akatoa bastola na kuwapiga risasi Wananchi wawili miguuni.

“Wananchi wakakasirika na kuanza kumpiga kisha kusababisha kifo chake pamoja na mmoja kati ya wale watu wawili alioongozana nao, mwingine mmoja alitokomea haijulikani alipokwenda.

“Tumeshawakamata watu kama saba hivi kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea.”
hii story mbona kama ya miaka kadhaa iliyopita.
 
Back
Top Bottom