Mbeya is Awesome. Hata kwenu pia ni kuzuri, kusifie huku ukisindikiza na picha za chombeza

Mbeya is Awesome. Hata kwenu pia ni kuzuri, kusifie huku ukisindikiza na picha za chombeza

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mbeya ni mkoa uliobarikiwa kwa baraka za mwilini na baraka za rohoni. Mbeya ni njema atakaye na aje.

Mbeya ndio mkoa ambao umekuwa ukiongoza kutoa timu nyingi zaidi zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Miongoni mwao ni Tukuyu Stars (Banyambala), Mecco, Tiger, Mbeya City, Mbeya Kwanza na Ihefu.
Tukuyu Stars Logo loves me.jpg

.

Mkoa wa Mbeya umekuwa mchangiaji mkubwa wa chakula nchini. Mchele, mahindi, ndizi, Makatapera (parachichi), viazi na vitu vingine vizuri mdomoni na mwilini hutoka Mbeya.
Organic Bujibuji .jpg



Mbeya ndio nyumbani kwa wasanii, kuanzia wanamuziki, waigizaji, magwiji wa mitindo, urembo, uchekeshaji na vipaji paji vingine vingi, Mbeya is the Best.

Kwa vivutio vya utalii ndio usiseme, Mbeya is the best place to be. Barabara iliyopita kwenye mwinuko wa juu kabisa barani Africa iko Mbeya.

Mbeya kuna uoyo mzuri wa asili, hebu angalia hii mandhari ya Mlima Mbeya (Mbeya Peak)
Screenshot_20221224-071554_WhatsAppBusiness.jpg
hakika ukifika, hutotamani kuondoka.

Mbeya ndiyo nyumbani kwa Mlima Rungwe. Mlima Rungwe ndio chanzo cha mito 12 inayopita Busokelo na Rungwe kwenda ziwa Nyasa. Uhai wa ziwa Nyasa hutegema sana ekolojia ya mlima Rungwe na safu za milima ya Livingston
images (18).jpeg


Mlima Rungwe kwenye background
images (19).jpeg
Uzunguni Josho Deep Mifugo Road.jpg
 
Daraja la kiteputepu tape bridge.jpg

Kyela: hii ni wilaya iliyo kusini mwa mkoa wa Mbeya. Hii wilaya inasifika sana kwa kilimo cha mpunga,kakao,nk ...hali ya hewa na nzuri kukiwa na joto la wastani pamoja na mvua za maana kuanzia mwezi wa pili mwishaon hadi mwezi wa nne. Asilimia kubwa ya wakaaji wa hii wilaya ni wakulima hasa mpunga pmj na kakao. Pia kuna ziwa Nyasa watu wanafanya uvuvi pamoja na utalii ktk ziwa hili kuna Matema beach, mwamunyange beach nk., pia biashara kwa sana ktk wilaya ya kyela ambapo wafanya biasha kutoka Malawi hufika wilaya ya kyela kununua badhaa,,,,wakaaji wa wilaya ya kyela ni wakarimu sana.
 
Mbeya ndiyo nyumbani kwa Mlima Rungwe. Mlima Rungwe ndio chanzo cha mito 12 inayopita Busokelo na Rungwe kwenda ziwa Nyasa. Uhai wa ziwa Nyasa hutegema sana ekolojia ya mlima Rungwe na safu za milima ya Livingston
Ongeza nyama nyama mkuu kuna vingi hujavieleza... Nimekaa hapa kwa Sokomatola nafuatilia huu uzi
 
Back
Top Bottom