KERO Mbeya Jiji: Nusu ya fedha za kujikimu kwa ajira za Walimu wa mwaka 2025 hatujalipwa

KERO Mbeya Jiji: Nusu ya fedha za kujikimu kwa ajira za Walimu wa mwaka 2025 hatujalipwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ni zaidi ya mwaka sasa tangu walimu tuliopata ajira mwaka 2025 turipoti kazini, lakini bado hatujalipwa fedha za kujikimu ambazo ni stahiki ya kila mtumishi wa umma. Kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma, fedha hizi zinapaswa kulipwa ndani ya siku saba baada ya mtumishi kuripoti katika kituo chake cha kazi.

Tumekuwa tukifuatilia suala hili mara kwa mara, lakini majibu tunayopata kutoka kwa wahusika hayaridhishi na hayatoi mwelekeo wa lini malipo hayo yatafanyika. Kinachotutia wasiwasi zaidi ni kwamba walimu wa ajira mpya katika baadhi ya wilaya nyingine tayari wamelipwa fedha zao za kujikimu kwa ukamilifu.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba mamlaka za juu na wizara husika zifuatilie kwa karibu suala hili ili kubaini sababu za ucheleweshaji huo. Pia tunaomba uchunguzi ufanyike kuhusu mwenendo wa fedha hizi katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, kwani kuchelewa huku kwa muda mrefu kumezua hofu miongoni mwa walimu kwamba huenda kulikuwa na ubadhirifu au matumizi yasiyo sahihi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya stahiki zetu.

Tunaomba sauti zetu zisikike na hatua stahiki zichukuliwe ili walimu wote wanaodaiwa fedha za kujikimu walipwe haki zao kwa wakati.
 
Back
Top Bottom