Mbeya Jiji rekebisheni barabara yenu Kabwe-Mwanjelwa kupitia Airport

Mbeya Jiji rekebisheni barabara yenu Kabwe-Mwanjelwa kupitia Airport

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Habari wanajukwaa,

Nilifika Mbeya jana jioni hivyo nikatafuta Lodge karibu na stand ya nanenane nikalala. Asubuhi nikapanda daladala kuelekea mjini kufata kitu kilichonileta.

Nilichoshangaa baada ya kufika Kabwe daladala ikaingia kushoto kupita njia ya Airport kwenda kutokea Mwanjelwa, huko barabara ni vumbi tena lile vumbi zito, gari likiwa mbele yako huoni mbele au ukikutana na gari lingine vumbi linaingia ndani.

Nimefika mjini nguo yangu imejaa vumbi, nywele vumbi kama nina mvi.
Kwa kweli wameniudhi maana nilikuwa naenda kwenye ofisi ya heshima nikaingia na vumbi langu kama nimesafiri sehemu isiyokuwa na lami, mpaka wakanishangaa vumbi lilivyojaa mpaka kwenye kope.

Kama Jiji wameamua kupitisha ruti za daladala huko kwa nini wasitengeneze barabara kwanza?

Mbeya mnaudhi sana.
 
Back
Top Bottom