Uchaguzi 2020 Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi wakati akichukua fomu ya Uteuzi

Uchaguzi 2020 Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi wakati akichukua fomu ya Uteuzi

😂😂😂😂 Hivi uchumI wa kati pia unapelekea siasa za kati ?
 
Asante sana. Nashukuru ndugu yangu.

Maisha yetu ni mafupi sana Duniani, na hakuna mwanadamu aliye na miliki nayo ya kudumu. Tenda kila jema uwezalo, jitahidi kuukwepa uovu maana adhabu ya mwovu daima ipo.

Ni wapumbavu tu ndio hufikiria kumkomoa mwanadamu mwenzake. Mwenye hekima kila siku huongeza marafiki lakini mjinga huongeza maadui bila kujua kuwa kuongeza maadui ni kuimarisha milki ya maadui, na miliki ya maadui iliyojengeka ndiyo adhabu yake mwenyewe.

Kim Jong Il alitawala kwa upanga wa moto huko Korea ya Kaskazini. Lakini kwa muda mrefu aliteseka na ugonjwa ambao ulimwondoa katika umri wa mapema. Wapinzani wake waliteseka kwa kukosa uhuru lakini yeye aliteseka kwa magonjwa. Wabaya wake aliwaondoa kwa risasi, naye aliondolewa kwa tatizo la kiafya. Ukweli ni kuwa yeye na wahanga wake, wote waliteseka na wote walikufa.

Sasa hivi ni Kiduku, bado kijana kabisa. Ametesa na ameua lakini naye anateseka.

Kanuni ni moja, huwezi kutesa bila kuteseka, huwezi kuua halafu ukaishi maisha marefu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Raia mzalendo ni yule atafutaye uthibitisho wa ukweli juu ya kila kauli ya mtawala badala ya kuwa kasuku wa kuimba vibwagizo vya mtawala
 
The law demands getting police consent before you decide to gather in public area, not long ago the message was emphasised by IGP on national television and reiterated by media the next day.

So wether you believe the whole thing is ridiculous by merit still there is a law which must be respected.

Sugu has only himself to blame for the most part.
Very selective law it fits like OJ Simpson's gloves. Let it be....
 
Hizi mbinu ovu zilitabiliwa, zinaanza kuonekana kama zilivyotabiliwa.

Na bado tutasikia na kuona mengi. Muda utaongea
Wanapima upepo wa kulazimisha Tulia atulie kwny kiti Cha Jimbo october
 
Lissu atawaponza wengi huu uhamasishaji wake wakutaka watu wasindikizwe ni kucheza bahati nasibu na polisi.

Pamoja na makosa ya Sugu, lugha aliyotumia polisi kwa kweli ni very provocative, iliyokosa staha na si lugha ya kiaskari. Ata mabosi wake wakitetea lugha wananchi tutashangaa.

The whole arrest procedure is wrong, lakini huyu Lissu atawaletea watu matatizo.

Na huyo ni polisi mkubwa, jiulize hawa watu wanjifunzaga nini CCP? Si sawa ila nasema tu hawa jamaa wanaaibishaga heshima ya majeshi, hawajifunzi wenzao wakitoka TMA. sijui wakoje wanatafutia watu kesi tu!
 
Na Picha iko wazi. Sugu alikuwa tayari ameshakabidhi fomu zake kwa msaidizi ili kutii agizo la polisi. Mbona hao polisi hawatumii busara hata ndogo. Hapo Sugu kila dalili iko wazi ni mtiifu wa sheria, tatizo hizo lugha za Polisi.

Kama kuna maelekezo vile, hata angepigiwa simu angeenda Polisi. Uvumilivu una mwisho.

Polisi nyinyi ni sehemu ya jamii, msijisahau ndio kwanza mkoko unaalika maua.

Mkuu kwa uzoefu wako hawa jamaa wanatumia busara? Hata akili hiyo jiulize wanayo? Angalia yule mwingine na elimu, umri na cheo alivyokua akiropoka ITV! Wanasoma nini hawa watu?
 
M
Mkuu Wangu Una Maneno Makali na MATUSI loooh Shusha Pumzi Mkuu Wangu Mana unaweza UKAMMEZA MTU...

Amani Amani Amani Amani Amani.

Jioni Njema Mkuu Wangu
Sana sana naweza kumeza jiwe sio mtu.... 😀😀

Unanionea bure mkuu.... Kulala juu ya mawe km mjusi ndio matusi.... Hahaaa😂😂
 
Inawezekana mimi na wewe tukawa tunajipotosha kwa kutegemea majibu huko google

Hapa unapaswa kutupa mwanga huko tukaongezee tu
kwani tulia amewaenda pekee yake kwenye function zote za harakati zake kutengeneza mazingira ya kushawishi wapiga kura kwanini dabo standard
 
Mkuu mtu yeyote aliewahi fanya kazi ya security ata kwenye mall huko ulipo anajua how to approach a scene and appropriate amount of force to use uitaji Sirro akwambie hilo.

Ata mtu anaetaka kujua haki zake mbele ya polisi anajua ni yepi wanaruhusiwa na zipi sio behaviour sahihi.

..Polisi walivyowa-approach Mh.Sugu na watu wake ni kana kwamba walikuwa wanatafuta sababu ya kuwapiga.

..Hali hiihii ya kulazimisha kupiga hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo ndiyo ilisababisha mauaji ya Daudi Mwangosi.

..Wananchi wanaonekana wana FURAHA zao halafu polisi wanawaingilia na kujaribu kuvuruga amani.

..Hiyo siyo sahihi hata kidogo.
 
Mimi polisi hata awe ndugu yangu wa damu sitakaa
1.Nimchangie harusi
2.Sitakaa niende msiba wa polisi
3.Sitakaa nimzike
4.Sitakaa nimkope hata kama nahakika anakufa mama yake
5.Sitakaa nimpangishe
ANGALIZO: Sitakaa nivunje sheria kwenye kuwadeal ikiwemo kutowatukana ,kutowaua ,japo siwezi kuahidi sitowaombea mabaya
Ha ha ha... wamekukinai vilivyo mkuu. Ila kumbuka wanatumwa hao. Watumaji wapo kimyaaa. Juzi kule kwa PM watia nia wa upinzani walitekwa kimya kimya usiku wa manane
 
Rais wakati anaenda kuchukua fomu yale maandamano yake yalifuata sheria gani?
Zamani nilikuwa nikisikia watu wanajitoa muhanga nashangaa Sana. Kwa ccm wapo bize wanatengeneza mazingira hayo Tz
 
Huyo askari mbona ni kituko, badala ya kufanya kazi yake anaanza kufanya personal attacks; kwamba "nisije nikakuvunjia heshima ambayo kwanza huna".
Dah, Inaumiza Sana. Unajua mchawi unaloga linageuka simbili.
 
Ha ha ha... wamekukinai vilivyo mkuu. Ila kumbuka wanatumwa hao. Watumaji wapo kimyaaa. Juzi kule kwa PM watia nia wa upinzani walitekwa kimya kimya usiku wa manane
Walikuwepo akina Iddy Amini dada, Abacha, Albashiri, Bokasa, Gadafi, Sadam Hussein, mabutu, chiluba na wenzao leo hii wapo wapi? Hakuna mabaya yasiyo na mwisho
 
Haya una akili sana wewe, nina uhakika Lissu awezi kurudia tena kusema hakuna inayozuia mikusanyiko.
Kilatha, sijui kwa nini unashinda humu ukitetea mambo ya kijinga. Tukishaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu, kanuni reja reja zilizowekwa katika mazingira tofauti kuwekwa kando.

Nikisema kanuni rejareka ni zile sheria ndogo ndogo za kitaasisi ambazo au moja kwa moja zinapingana na Katiba ya nchi au hazizingatii wala kuheshimu matakwa ya sheria mama, Katiba.

Nakuapia kuwa mgombea wa CCM hawezi kufanyiwa uhuni kama huo aliofanyiwa Mh. Sugu. Wakati unafika wa hekima na busara kutumika ili angalau wagombea wote waonekana wamepewa fursa sawa.

Huyo OCS mhuni (ndio namwita mhuni kwani kaonesha kitendo cha kishenzi) kama mgombea angekuwa wa CCM si ajabu angeishia kupiga saluti. Huo ndio ukweli ambao nakupa uhuru wa kuupinga.
 
Back
Top Bottom