Uchaguzi 2020 Mbeya: Joseph Mbilinyi(Sugu) akamatwa na Polisi wakati akichukua fomu ya Uteuzi

😂😂😂😂 Hivi uchumI wa kati pia unapelekea siasa za kati ?
 

Raia mzalendo ni yule atafutaye uthibitisho wa ukweli juu ya kila kauli ya mtawala badala ya kuwa kasuku wa kuimba vibwagizo vya mtawala
 
Very selective law it fits like OJ Simpson's gloves. Let it be....
 
Hizi mbinu ovu zilitabiliwa, zinaanza kuonekana kama zilivyotabiliwa.

Na bado tutasikia na kuona mengi. Muda utaongea
Wanapima upepo wa kulazimisha Tulia atulie kwny kiti Cha Jimbo october
 

Na huyo ni polisi mkubwa, jiulize hawa watu wanjifunzaga nini CCP? Si sawa ila nasema tu hawa jamaa wanaaibishaga heshima ya majeshi, hawajifunzi wenzao wakitoka TMA. sijui wakoje wanatafutia watu kesi tu!
 

Mkuu kwa uzoefu wako hawa jamaa wanatumia busara? Hata akili hiyo jiulize wanayo? Angalia yule mwingine na elimu, umri na cheo alivyokua akiropoka ITV! Wanasoma nini hawa watu?
 
M
Mkuu Wangu Una Maneno Makali na MATUSI loooh Shusha Pumzi Mkuu Wangu Mana unaweza UKAMMEZA MTU...

Amani Amani Amani Amani Amani.

Jioni Njema Mkuu Wangu
Sana sana naweza kumeza jiwe sio mtu.... 😀😀

Unanionea bure mkuu.... Kulala juu ya mawe km mjusi ndio matusi.... Hahaaa😂😂
 
Inawezekana mimi na wewe tukawa tunajipotosha kwa kutegemea majibu huko google

Hapa unapaswa kutupa mwanga huko tukaongezee tu
kwani tulia amewaenda pekee yake kwenye function zote za harakati zake kutengeneza mazingira ya kushawishi wapiga kura kwanini dabo standard
 

..Polisi walivyowa-approach Mh.Sugu na watu wake ni kana kwamba walikuwa wanatafuta sababu ya kuwapiga.

..Hali hiihii ya kulazimisha kupiga hata kama hamna sababu ya kufanya hivyo ndiyo ilisababisha mauaji ya Daudi Mwangosi.

..Wananchi wanaonekana wana FURAHA zao halafu polisi wanawaingilia na kujaribu kuvuruga amani.

..Hiyo siyo sahihi hata kidogo.
 
Ha ha ha... wamekukinai vilivyo mkuu. Ila kumbuka wanatumwa hao. Watumaji wapo kimyaaa. Juzi kule kwa PM watia nia wa upinzani walitekwa kimya kimya usiku wa manane
 
Rais wakati anaenda kuchukua fomu yale maandamano yake yalifuata sheria gani?
Zamani nilikuwa nikisikia watu wanajitoa muhanga nashangaa Sana. Kwa ccm wapo bize wanatengeneza mazingira hayo Tz
 
Huyo askari mbona ni kituko, badala ya kufanya kazi yake anaanza kufanya personal attacks; kwamba "nisije nikakuvunjia heshima ambayo kwanza huna".
Dah, Inaumiza Sana. Unajua mchawi unaloga linageuka simbili.
 
Ha ha ha... wamekukinai vilivyo mkuu. Ila kumbuka wanatumwa hao. Watumaji wapo kimyaaa. Juzi kule kwa PM watia nia wa upinzani walitekwa kimya kimya usiku wa manane
Walikuwepo akina Iddy Amini dada, Abacha, Albashiri, Bokasa, Gadafi, Sadam Hussein, mabutu, chiluba na wenzao leo hii wapo wapi? Hakuna mabaya yasiyo na mwisho
 
Haya una akili sana wewe, nina uhakika Lissu awezi kurudia tena kusema hakuna inayozuia mikusanyiko.
Kilatha, sijui kwa nini unashinda humu ukitetea mambo ya kijinga. Tukishaingia kwenye kipindi cha uchaguzi mkuu, kanuni reja reja zilizowekwa katika mazingira tofauti kuwekwa kando.

Nikisema kanuni rejareka ni zile sheria ndogo ndogo za kitaasisi ambazo au moja kwa moja zinapingana na Katiba ya nchi au hazizingatii wala kuheshimu matakwa ya sheria mama, Katiba.

Nakuapia kuwa mgombea wa CCM hawezi kufanyiwa uhuni kama huo aliofanyiwa Mh. Sugu. Wakati unafika wa hekima na busara kutumika ili angalau wagombea wote waonekana wamepewa fursa sawa.

Huyo OCS mhuni (ndio namwita mhuni kwani kaonesha kitendo cha kishenzi) kama mgombea angekuwa wa CCM si ajabu angeishia kupiga saluti. Huo ndio ukweli ambao nakupa uhuru wa kuupinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…