Mwanongwa
JF-Expert Member
- Feb 15, 2023
- 611
- 567
Hivi ni nani alitoa wazo la kupafanya Stendi ya Daladala ya Kabwe kila ikifika jioni kupageuza Soko?
Moja hili eneo ni chafu kupita maelezo na Wafanyabiashara wamejianzishia Dampo hapohapo.
Yaani huku taka zimejaa lakini pembeni yake unaona mama anaendelea na kuuza Samaki, Matunda, Mboga Mboga n.k.
Maafisa wa Afya wale 'Mabwana Afya' mmetulia kimya kana kwamba hamuoni kinachoendelea maeneo hayo au mpaka Watu waugue kipindupindu ndiyo mtapazuia.
Ukiachana na uchafu pia ikifika jioni Daladala zinapata shida sababu stendi inakuwa imebanwa na Wafanyabiashara, hivyo kusababisha kero isiyokuwa na msingi.
Nao vibaka hawako nyuma kila ikifika jioni wanaingia kazini ukizubaa tu imekula kwako.